Nidhamu ya majeshi yetu ni mbovu kuliko kipimo

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
3,737
2,000
Kwa wakaazi wa Dar munafahamu wazi kwamba kuishi karibu na kambi yoyote ya kijeshi ni balaa! Ukiwaondoa magereza, wengine wote ni tatizo la kudumu. Wanatembea mitaani wakinywa pombe wakisaka akina mama na baadaye ni ugomvi hata wa kutumia siraha bila sababu yoyote. Bahati mbaya sehemu kubwa ya watu hawa ni wanaume.

Ajira ktk majeshi yetu ilikuwa ni kwa sifa za misuri na uwezo wa kukimbia. Baadaye usomi umepewa nafasi lakini nidhamu imebaki Kuwa ni sifa isiyopatikana jeshini.

Matukio ya hivikaribuni kwangu Mimi niliyategemea. Jeshi letu Lina waajiliwa wapuuzi kwa kiwango cha juu sana. Askari wa kuuliza ghasia Mara nyingi wamepambana na raia na bahati mbaya akina mama huoni aibu kutaja matukio Kama haya. Vijana wa vyuo vikuu ni shahidi kwamba Mara zote wanapopambana, matukio ya kudhalilisha akina dada imekuwa ni tabia inayotajwa. Sasa kwa watawala hudhani ni sifa kwa muhalifu kudhalilishwa au vyuo vikuu 'kukomeshwa'. Hii ni aibu!

JWTZ pia ni aibu tu. ktk vita ya Uganda, sehemu kubwa ya wanajeshi waliufanyaje baada ya vita kuliko wakati wa vita. Matukio makubwa yakitokana na tabia ya ngono. Walitumia siraha kulazimisha ngono. Waganda wamekufa kwa kupigwa risasi pia wengine kwa sababu tu ya kugoma kuifanya ngono! Walipowahiwa pia wakauwawa.

Msumbiji yalikuwa hayo hayo! Huko pia uporaji uliwalenga wenye pesa. Tumeshuhudia ma-Benz yakishushwa kwenye ndege za jeshi zinazotoka Msumbiji.

Jeshi lenye ubongo wa aina hii utalitumiaje ktk shughuli za kiraia? Bahati mbaya anayesema anapewa zigo la kuambiwa atowe ushahidi badala ya muhusika kuchunguza undani na Kuwatia nidhamu.

Duniani kote matukio haya hutokea lakini uzuri wahusika huchukuwa hatua na kukomesha upuuzi Kama huo. Imekuwaje kwa TZ hata kuzuiya askari kuwapiga majirani imekuwa ni ndoto? Tena ndani ya Dar!

Je, wahusika huvaa kimya kwa sababu hata wao wamewatumia kutimiza upuuzi wao? Pia inawezekana. Tunajua jinsi siasa inavyotumika vibaya kwa kuvitumia vyombo vya dola. Hata bungeni tunayaona. Mwanasheria mkuu wa Serikali amegeuzwa kuwa Mwanasiasa mkuu wa serikali.

Bila vichwa vipya ktk serikali, hatutapiga hatua yoyote. Kwa ujumla tumeruhusu wapuuzi wengi kujiunga siasa na sasa wanaongoza nchi.
 

Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
14,605
2,000
Hili suala la majeshi,serikali imelilea sana sana sana,sasa naona serikali inajibaraguza tu,,,,wanajeshi na polisi wengi wao ni mafedhuli sana,tena sana,polisi wauaji sana tu,hata hao magereza enzi ya mapuri walipiga hovyo watu
 

Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,061
2,000
SEREKALI YA CCM NI MZIGO MZITO!
2015 kwa garama yeyote lazima itoke,wameshidwa kwa miaka 50+
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
12,965
2,000
Uko sahihi Mkuu. Izingatiwe kwamba atomvu wa nidhamu ndani ya JWTZ sio kwa askari wa chini (wapiganaji) tu bali unaanzia ngazi ya juu kabisa ya Jeshi na kuna mifano hai. Kitendo cha Mnadhimu wa JWTZ, Lt. Gen. Abdulrahamani Shimbo kujitokeza hadharani kipindi kile kuwatisha wananchi katika masuala ya kisiasa/kiraia ulikuwa ni utomvu mkubwa nidhamu kwa kiongozi wa hadhi yake.

Kwa nchi zinazozingatia maadili huyu "mwehu" alipswa ku-step down mara tu baada ya "tangazo" lake lile au afukuzwe kazi mara moja. Lakini kama mazuzu, sio wenye mamlaka waliona hatari ya kitendo kile wala wananchi wa kawaidia walioona shida kutokana na ufedhuli ule.

Kama "kiongozi" wa hadhi ile aliweza kuongea vile mchana kweupe bila kukemewa na yeyote unadhani nidhamu za "vidagaa" jeshini ikoje? Mtu wa aina hii, kutokana na ulevi tu wa cheo, hashindwi kuingiza battalion mtaani kupambana na raia and soon yakatokea ya Sudan Kusini! Ee Mola tuepushe.
 

Shekizongoro

JF-Expert Member
Dec 9, 2013
388
195
Uko sahihi japo umekosa uzalendo; Mi nliambiwa Jeshin nidham kwanza, sasa majeshi yanabaka raia hadi JWTZ nao..! Wananyan'ganya watu mali zao...??? UPDF waliwauzia slaha waasi Somalia, KDF wakasachi wahanga wa Westgate.! sa JWTZ wametia aibu. Naomba wataalam jeshin mtueleze hili limetokeaje kama nidham iko mbele.
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
12,965
2,000
Uko sahihi japo umekosa uzalendo; Mi nliambiwa Jeshin nidham kwanza, sasa majeshi yanabaka raia hadi JWTZ nao..! Wananyan'ganya watu mali zao...??? UPDF waliwauzia slaha waasi Somalia, KDF wakasachi wahanga wa Westgate.! sa JWTZ wametia aibu. Naomba wataalam jeshin mtueleze hili limetokeaje kama nidham iko mbele.

Nidhamu inayozungumzwa jeshini ni kutii maagizo kutoka juu na sio nidhamu ya kukujali wewe raia. Ni heri ukutane na dubu wenye njaa kali kuliko kukutana na JWTZ mitaani wakigombea malaya. Kama ulikuwa hujui hilo, ndio hivyo.
 

gen parton

JF-Expert Member
Jan 15, 2013
615
500
Ni tanzania tu mtu kama pinda anaweza kuundelea kuwa waziri mkuu
mmesahau hawa askari wanatokea ktk jamii zetu hivyo kama hawana maadili ni jamii ndio ya kulaumiwa vinginevyo mtalialia humu na mkiingia kwenye anga zao mtakula kisago tu afu hakuna wa kuwasikiliza
 

gen parton

JF-Expert Member
Jan 15, 2013
615
500
Hili
suala la majeshi,serikali imelilea sana sana sana,sasa naona serikali
inajibaraguza tu,,,,wanajeshi na polisi wengi wao ni mafedhuli sana,tena
sana,polisi wauaji sana tu,hata hao magereza enzi ya mapuri walipiga
hovyo watu
nenda kawaulize mtwara gas inatoka au haitoki? wamekula stick na ubishi sasa mvukon chezea hata ukilia lia humu haisaidii nyambafu
 

chikutentema

JF-Expert Member
Dec 10, 2012
7,296
2,000
Mgareza nawapa much respect hata mimi sioni kama wana makashifa kama hao wenge nadhana uongozi wao ni mzuri hata nidham
 

Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
14,605
2,000
Nidhamu inayozungumzwa jeshini ni kutii maagizo kutoka juu na sio nidhamu ya kukujali wewe raia. Ni heri ukutane na dubu wenye njaa kali kuliko kukutana na JWTZ mitaani wakigombea malaya. Kama ulikuwa hujui hilo, ndio hivyo.

sijui wanakuaje,,,ni kama mtu asojua kutongoza,yaan wanawehuka sana
 

Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
14,605
2,000
nenda kawaulize mtwara gas inatoka au haitoki? wamekula stick na ubishi sasa mvukon chezea hata ukilia lia humu haisaidii nyambafu

na kubaka pia mlibaka huko GAS CITY,,,maana ndo inaonesha tabia zenu,mimi silii mdau,ila UKIMWI NDO UNAWALIZA,
WAKAT WA OPERESHEN TOKOMEZA KUNA MWANAJESH ALIKUJA HAPA AKALALAMIKA KUWA WAMEZIMIS FAMILIA ZAO BORA WARUHUSIWE WAKAZIONE,KUMBE NDO MLIKUA MNABAKA
 

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,414
2,000
Huu ndo uozo halisi tunaousema wa miaka 50 ya utawala wa CCM na bado wanang'ang'ana waendelee kutawala,nchi imekosa maadili to the maximum na kwa sasa hata hiki kiaibu kitaisha na mambo yanaelekea kubaya zaidi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom