Nidhamu kwa mwanadamu: Mdomo waweza kujenga na kubomoa

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Nidhamu ni kitu cha msingi sana katika maisha ya binadamu. Nidhamu humpa uwezo binadamu kuongoza mawazo yake na matendo yake katika mkondo unaofaa. Uwezo huu umfanya binadamu kutawala maisha yake vyema.

Bila nidhamu binadamu hatoweza kupata furaha katika maisha yake. Hakuna kitu chochote kitakachoenda sawa kama hatutajifunza kuwa na nidhamu katika maisha yetu. Nidhamu huleta order.

Na ni matendo yetu ambayo hupaswa kuongozwa mara kwa mara na nidhamu ndiyo yanayotufanya tudumbukie katika makosa mara kwa mara na kuumia. Hufanya kushindwa kuongoza familia zetu vyema kwa kushindwa kujitawala kwa kutawala nafsi zetu na hisia.

Katika uongozi huwezi kuwatawala wengine vyema kama wewe mwenyewe huwezi kujitawala. Ni nidhamu pekee ambayo humfanya mtu kutawala maisha yake na kuwa na mahusiano mema na wengine. Ni uwezo wa kutawala mawazo yako, mdomo wako na matendo yako na kuyaongoza katika mkondo unaofaa.

Kama tunavyojua mdomo una madhara makubwa sana kwa binadamu mwenyewe lakini kwa watu wengine pia. Wengi wetu tumeona au tumesikia na kuumizwa na madhara ya mdomo. Kwahiyo, kwa kujua madhara ya mdomo kuna umuhimu wa kuchunga midomo yetu. Kwasababu mdomo una pande mbili unaweza kujenga na kubomoa kabisa maisha ya binadamu.

Kwahiyo nidhamu ni jambo la msingi na muhimu kuwa nalo. Ni nguvu ya akili kuongoza na kutawala mawazo na matendo na kuyaongoza katika mkondo unaofaa, wenye faida kwa mtu binafsi na kwa jamii yake. Bila nidhamu malengo yetu tuliyojiwekea ni vigumu mno kuyafikia.

Mikono yetu, miguu yetu, masikio yetu na macho yetu ni nyenzo tu ambazo akili na mawazo yetu huzitumia kufikia malengo yake yawe hasi au chanya. Tunafikiri kisha mikono, miguu, masikio na macho yanatenda kufanikisha kile tunachofikiri ili kiwe kitu kinachoonekana. Dunia haikuumbwa kwanza na vitu vinavyoonekana. Nidhamu huleta order katika jamii.

Nidhamu ni kujizuia na kutenda yaliyo sahihi na ya haki.
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom