x - mas
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 930
- 611
Habari za wakati huu wana jf ! Nimekuwa na ukakasi juu ya nidhamu iliyopo makazini tangu utumbuaji wa majipu uanze.
Binafsi nafikiri nidhamu iliyopo ni ya woga na sihalisi, washabiki na serikali wanaona wamerudisha nidhamu makazini bila kujua inafanya watumishi kushusha thamani ya kazi zao ,kuwaongezea msongo wa mawazo,kuchukia kazi,kudharaulika n.k sidhani kama kwa matokeo haya kutakuwa na ufanisi mzuri wa kazi.
Ushauri wangu ni kwamba serikali ifanye kwanza mambo yafuatayo; itoe nyongeza ya mishahara ya mwaka jana ,ilipe madeni ya watumishi,iweke mgao sawa wa watumishi mjini na vijijini,iwafikirie watumishi waliopo mazingira magumu, ilipe nauli za likizo kwa wakati,iongeze mshahara,ilekebishe mishahara kwa walio panda madaraja ,ijenge nyumba za watumishi,itoe ajira kwa wakati,ikitoa ahadi itimize kwa wakati mfano ile ya kurekebishiwa mishahara ilikuwa ndani ya mwezi mmoja na nusu haitazidi miwili lakini sasa tunakaribia mwaka.
Kwa kufanya hivyo nidhamu halisi itapatikana kwani watumishi watathamini kazi zao hata ukiwadai wawe na nidhamu watakuelewa kwa urahisi na watakusaidia kwa moyo mmoja kuwarekesha wale wasio na nidhamu pia hata wale wasio na nidhamu watashikwa na haya kuona serikali inavyo wajali wao wanazembea hivyo badala ya kuchukia kazi watachukia utovu wao wa nidhamu.
Na kama serikali haina uwezo wa kutimiza hayo basi ni bora itumie hekima kuleta nidhamu halisi makazini na si kushurutisha watu kama watumwa.Ni hayo tu wewe unasemaje kuhusu nidhamu iliyopo sasa makazini?