NIDA: Namba za Utambulisho (NIN) Milioni 6 bado hazijatumika kusajili laini za simu

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imesema kuwa inaendelea na zoezi la usajili na utambuzi wa watu, uzalishaji wa namba za utambulishi wa taifa na vitambulisho na ugawaji wake kwa wananchi ili waweze kuvitumia kusajili kadi (laini ) za simu kwa alama za vidole na huduma nyingine.

Katika kurahisisha upatikanaji wa namba za utambulisho wa taifa, NIDA imebuni njia mbalimbali zitakazowasaidia wananchi kupata namba zao na kupunguza msongamano mkubwa katika ofisi zao.

Njia hizo ni kwenda kuchukua namba katika ofisi za vijiji husika ambazo zitakazopelekwa na NIDA, kutumia USSD *152*00# na kufuata maelekezo, au kutuma ujumbe mfupi wa simu kwenda namba 15096.

Mwombaji anapochagua kutumia njia ya kutuma ujumbe mfupi atatakiwa kuandika jina la kwanza na jina la mwisho, tarehe ya kuzaliwa, jina la kwanza la mama, na jina la mwisho la mama. Huduma hii ni bure.

Aidha, wananchi wanaweza kupata namba na vitambulisho vyao katika ofisi za NIDA au vituo vya muda vya mamlaka hiyo vilivyo karibu nao.

Hadi Januari 15, NIDA ilikuwa imezalisha idadi kubwa ya namba za utambulisho wa taifa ambapo kati ya hizo namba za utambulisho 6,806,096 hazijatumika kusajili laini za simu kwa alama za vidole.

Mamlaka hiyo imewasihi wananchi ambao tayari wamepata namba kuzitumia kusajili laini zao ili wasifungiwe ifikapo Januari 20, mwaka huu kwani sio lazima kuwa na kitambulisho ndipo uweze kusajili.

Chanzo: TBC

1579245986149.png


1579246003122.png
 
WANANCHI MSIKUBALI KUFANYWA WAJINGA NA NIDA ETI WAKUPE NAMBA TU BILA KIKADI KATAA KABISA HIYO NI SAWA NA KWENDA AMERICA VISA UMEIACHA NYUMBANI UKITEGEMEA UTAINGIA.
.
WATAWASUMBUENI SANA KUPATA HIZO KADI
 
Kwani hao NIDA wanasajiri wananchi Kwa ajiri ya laini za Simu? Kuna watu wamesoma lakini wanashindwa kutumia Elimu yao vizur, Watu wanajisajiri kupata vitambulisho vya utaifa sio kwa ajiri ya kusajir Simu bhana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Njia hizo ni kwenda kuchukua namba katika ofisi za vijiji husika ambazo zitakazopelekwa na NIDA, kutumia USSD *152*00# na kufuata maelekezo, au kutuma ujumbe mfupi wa simu kwenda namba 15096.
Hizi njia zote nimejaribu lakini hawa jamaa hawajibu chochote.
BASIASI
 
Wakuu hii takwimu sijaelewa wanaposema kuwa kati waliosajiliwa na NIDA ni milioni nne hawajaenda kusajili laini zao, wanagunduaje?

Maana wengine huwa na laini tatu na hutumia kitambulisho hicho hicho, wengne hawana simu, sasa hii takwimu imewapiga chenga au ni mimi sielewi?

Maana mfano mimi nimesaji laini nne kwa kitambulisho chao kimoja hicho hicho, huenda wangesema takwimu za laini ambazo hadi sasa hazijasajiliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nida wanajitetea tu japo.....mfumo kweli unasumbua server ila kazi nyingi kwa sasa zinafanhika kimadili sana

sent from toyota Allex
 
Assumption ni kila line ina simu..., kwahio kutakutakuwa kuna namba 4m ambazo hazijapata simu...,

Sio kwamba nafanya kazi nida ila hio ni assumption yangu..., sidhani kama kuna mwananchi mwenye National ID ambaye hana simu, ukizingatia simu imekuwa kama middle name kwa binadamu wa sasa
 
Walichosema namba Million 6 ndiyo ambazo hazijatumika kusajili lain yoyote kati hyo kadhaa ambazo zimetolewa kwa wananchi! Hiyo mbona simple kuigundua wakishirikiana na TCRA?
 
Back
Top Bottom