NIDA nakuja kuchukua kitambulisho changu

MfalmewaKiha

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
1,191
1,228
Takriban mwaka mmoja ulio pita Niliahidi kumshikisha au kuwasilisha Maafisa wa uhamiaji kwenye mikono ya sheria baada ya kuwa na uhitaji wa Hati ya kusafiria

Ukisoma kwenye website yao inasema na kutoa maelezo na gharama za kupata Hati ya kusafiria ambayo bei yake ni shilingi 150,000 ila pamoja na hayo ukweli ni kwamba huwezi pewa kwa bei hiyo

Nilianza mchakato huo wa kuomba ila dalili za wao kutaka hela zilikuwa wazi walihitaji 350,000 kwa kifupi sikuwapa mwisho mmoja wao aliambulia kutiwa nguvuni.

Sasa basi Siku chache zilizo pita nilipoteza kitambulisho cha NIDA, KWENYE MTANDAO WAMESEMA ILI NIPATE KIPYA LAZIMA NILIPE SH 20,000

Ila cha ajabu nimekwenda ofisini kwao wameniambia gharama ni shilingi Elfu 50.

Sasa basi ni hiyo 50 ntawapa ila iweni makini siwatishi ila hiyo hela itaondoka na mtu.

NB: Uhamiaji Singida na yenyewe mhhhhh.(ngoja nisiseme)
 
Maelezo yao haya hapa
Screenshot_20210304-161820.jpg
 
We jamaa ungekua na kajinafasi mahali kitengo flani ungetesa sana binadamu wenzako.
 
Utawakosa hapo kwenye maelezo "au kiasi utakachoelekezwa na afisa wa nida" hiyo fifte ndio itaangukia hapo
Bro,Bro,Bro nimekuita mara 3, Nipo makini sana kuliko unavyo dhani,Ninacho jua hela zote au malipo Yote ni control number Basi,Na term hii nta record video za tukio mwanzo mwisho
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom