Mmeanza zamani sana kuandikisha vitambulisho vya Taifa. Hali ilipamba moto mwaka 2017 pale watumishi wa umma walipolazimika kujiandikisha kwa lazima.
Tuliwaona jinsi vituo vyao vya kazi vilivyokuwa vinafungwa ili waende kuhakikiwa. Hongera zao, hakuna mtumishi wa umma asiye na kitambulisho cha NIDA.
Shida inakuja kwetu wa kijijini. Walileta fomu tukajaza (fomu zenyewe zilikuwa zinauzwa). Fomu zilikusanywa ila hawajawahi kuja kutupiga picha.
Kwahiyo namba za NIDA hatuna. Achilia mbali vitambulisho.
Hata mkifanya kazi masaa 24, bado raia wa kijijini hamuwezi kuwafikia. Tuseme hivi, usajili wa laini ni kwa watumishi wa umma na wananchi wa mjini.
Mnaenda kuvunja mahusiano ya watu ambayo yalitegemea mawasiliano ya simu. Pia mnarudi pale pale mtu mmoja kusajili laini zaidi ya kumi.
Kwa mfano, hapa kijijini kuna mwalimu kutokea mkoa mwingine kaoa kwenye familia moja. Kwakuwa hawana namba za simu amelazimika kusajili laini zake tatu, laini mbili kwa mke wake, na zingine kwa baba mkwe, mama mkwe na mashemeji wawili.
Hata ukisajili mtandao mmoja laini zaidi ya moja, HAIKATAI, INAKUBALI.
Naona bado kuna tatizo