NIDA kutoa utambulisho kwa watanzania wote ifikapo 31/12/2016

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA imesema kufikia mwezi Disemba mwaka huu itahakikisha kila mtanzania amepatiwa namba ya utambulisho itakayowezesha kupata Kitambulisho cha Taifa pindi mchakato huo wa utoaji wa vitambulisho vya taifa utakapo anza kwa mara nyingine tena.

Wamesema watatumia vifaa na namba kutoka kwa tume ya uchaguzi ili kuwarahisishia zoezi hilo na vitambulisho vitakuwa vya aina tatu, vya wenyeji, wageni na wakimbizi.

Mbona naona hapa kwenye habari wanasema kazi zikitoka hawa vijana 500 watawapa kipau mbele ilihali walipowatoa walisema hawana ufanisi,, sasa Leo wanasema watawapa nafasi coz wana uzoefu,, hii inanifanya nipate mashaka kuwa walionewa kwa sababu za kisiasa tu kama hawa wanafunzi wa udom
 
Umeonaeeeeee?
 
Kwa nini tusitumie hivyo hivyo vya NEC? Kwa nini tuwe na multiplicity of Ids? Kwa nini Database isiwe integrated (Kuunganishwa) ili TRA Biometric, Nida Biometric, NEC Biometric, Passport Biometric, Birth Certificate Biometric ziweze kushare data? I mean ukienda katika Taasisi mojawapo kati ya hizo iwe tosha kuwezesha database sharing.
 
Vitamvualisho vya nec havina uwezo wa kuhold hy integration.... waswas wangu pia ni matumizi ya data za nec tulizo ona mpaka pikipiki, viwanja, ofisi zikiwa zimepigwa picha..... ukifika na kujieleza wakati wa usajiri wa nec basi unapewa
kitambulisho... tusipo kuwa makini data za nec zitaua maana ya kuwa na kitambulisho cha taifa kilicho na data halisi.....
 
Vizuri ila time line waliojiwekea ni muda mfupi mno sidhani kama watamaliza kama wanaielewa jiografia ya nchi yetu
 
Ole wao waje na likitambulisho LIKUUUBWAAA hata haliingii kwenye wallet!!
Afu tunataka kiwe MAGNETIC kama vya Benki. Cha LUBUVA ile rangi inayo ng'aa changu imetoka yote!!
 
Kwa nini tusitumie hivyo hivyo vya NEC? Kwa nini tuwe na multiplicity of Ids? Kwa nini Database isiwe integrated (Kuunganishwa) ili TRA Biometric, Nida Biometric, NEC Biometric, Passport Biometric, Birth Certificate Biometric ziweze kushare data? I mean ukienda katika Taasisi mojawapo kati ya hizo iwe tosha kuwezesha database sharing.

Halafu anasema fomu ya NEC ina maswali machache, je ina maana vya NEC havina ubora sana wakati ndio muhimu kwa uhai wa taifa?
 
Back
Top Bottom