NIDA kuanzia mwezi huu wataanza kutoza fedha Taasisi zote za Umma na Binafsi ambazo zinatumia taarifa za Mamlaka hiyo kuhudumia Wananchi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,241
MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imesema kuwa kuanzia mwezi huu wataanza kutoza fedha taasisi zote za umma na binafsi ambazo zinatumia taarifa za mamlaka hiyo kuhudumia wananchi

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa NIDA, Geofrey Tengeneza wakati akizungumza na The Guardian Digital

“Kuna wadau ambao wanatumia taarifa zetu kutoa huduma kwa wananchi napenda niwajulishe kuwa kuanzia mwezi huu (Julai, 2020) tunaanza kutoza tozo kwa taasisi zote za umma na binafsi ambazo zinatumia taarifa zetu kuhudumia wananchi mbalimbali”amesema Tengeneza na kuongeza kuwa;

“Kwa mfano makampuni ya simu, NSSF, Bima ya Afya, mabenki na wadau wengine mbalimbali ambao hili waweze kutoa huduma kwa wateja wao wanahitaji kupata taarifa kutoka kwetu ni lazima kuzilipia ili kuendelea kutoa huduma hiyo”amesema

Ameongeza kuwa taasisi hizo zinapaswa kuingia mkataba na NIDA ili kuweza kupata huduma hizo vinginevyo taasisi ambazo zitashindwa kutimiza matakwa hayo watasitisha huduma hiyo mara moja

Ameongeza kuwa tayari wametoa notisi kwa kampuni ambazo azijaingia mkataba na NIDA kufanya hivyo mpaka Julai 31, 2020 na kwa ambazo zitashindwa watasitisha huduma.

“Kampuni 17 tayari tumewatumia notisi kuanzia Agosti Mosi kama watakuwa hawajaleta maombi kwetu ili kuwapatia mkataba tutawakatia huduma pia tunaendelea kufanya upembuzi kujua ni makampuni gani wanatumia huduma zetu,”amesema

Amesema kuwa kwa hatua ya awali wanategemea kuingia mkataba na watumia taarifa za NIDA zaidi makampuni na taasisi 86.

Amesema kuwa utaratibu huo ni maelekezo kutoka kwa Serikali yalioelekeza NIDA kuanza kujitegemea kukusanya fedha kutumia utaratibu huo ili kuondokana na utaratibu wa kupata fedha za matumizi kutoka serikalini.

“Mpaka sasa kampuni 65 zimeleta maombi ya kusaini mkataba na pia tumepeleka mikataba kwa kampuni 36 bado hawajarudisha, pia makampuni 18 wamerudisha mikataba na 12 kati yao tayari tushasaini nao mkataba”amesema
 
Hii nchi ina mambo ya hovyo sana, NIDA wanataka kuanza biashara ya vitambulisho sijui wamekuwa nao SU? mwisho wa siku ambaye atatozwa na hizo taasisi ni mwananchi/rai maskini. waache usanii wa kipuuzi, nini faida ya hivyo vitambulisho sasa?
Exactly...na hapa eti kuna mtu kaja na hili wazo ili liwe chanzo cha mapato....wameshasahau shida wanayopata watu wakifuatilia hicho kitambulisho......hatari sana
 
Taarifa zao NIDA waunge na uhamiaji kupunguza ma documentation wakati wa maombi ya passport wawarahisishie kazi wanaumia sana uhamiaji

Wawachaji tu sawa sababu uhamiaji wata recover kwa waombaji
Naunga mkono hoja yako
 
Exactly...na hapa eti kuna mtu kaja na hili wazo ili liwe chanzo cha mapato....wameshasahau shida wanayopata watu wakifuatilia hicho kitambulisho......hatari sana
Tuna fanya mambo ya hovyo sana bila kuangalia athari zake kisa kumfurahisha mfalme
 
Hii nchi ina mambo ya hovyo sana, NIDA wanataka kuanza biashara ya vitambulisho sijui wamekuwa nao SU? mwisho wa siku ambaye atatozwa na hizo taasisi ni mwananchi/rai maskini. waache usanii wa kipuuzi, nini faida ya hivyo vitambulisho sasa?
✓Kodi ya kichwa imerudi kwa mtindo mwingine
 
Hii nchi ina mambo ya hovyo sana, NIDA wanataka kuanza biashara ya vitambulisho sijui wamekuwa nao SU? mwisho wa siku ambaye atatozwa na hizo taasisi ni mwananchi/rai maskini. waache usanii wa kipuuzi, nini faida ya hivyo vitambulisho sasa?
Huduma nyingi zilipokuwa bure zilikuwa mbovu mno sote mashahidi.maji bure cock tu ikaharibika bomba la jumuiya unaambiwa usubiri bajeti ijayo sababu fungu hamna
Heri tulipie zipatikane haraka wasiwe na visingizio.Cha muhimu bei ziwe affordable

Waunge taasisi nyingi kadri inavyowezekana na taasisi si lazima ziandikiwe mfano kuna nyingi unaulizwa uraia ungeni mfano sasa hivi vyama vya siasa viko michakato ya wagombea maswali ya taarifa kama za NIDA yatatakiwa .VYAMA vya siasa vijiunge au waungwe kwa nguvu isiwe hiari
 
Mnako elekea mtapiga kodi mpaka sadaka la fungu la 10, wanashindwa nini ku-integrate NIDA na mifumo ya taasisi zingine?, mbona TRA na NIDA imewezekana? tumia akili kidogo mkuu
 
kuunga kutapunguza muda wa utoaji huduma kwa wengi hili wazo zuri ila liende haraka

Niwapongeze waliotengeneza mfumo wa malipo ya serikali wa GePG kwa muda mfupi walikamilisha kuunga taasisi nyingi mno zilizokuwa kero na maudhi makubwa kwenye utoaji huduma za binafsi na za serikali
 
Hii nchi ina mambo ya hovyo sana, NIDA wanataka kuanza biashara ya vitambulisho sijui wamekuwa nao SU? mwisho wa siku ambaye atatozwa na hizo taasisi ni mwananchi/rai maskini. waache usanii wa kipuuzi, nini faida ya hivyo vitambulisho sasa?
Now tuko kwenye uchumi wa katikati
 
Gharama zote hapa zinashuka kwa muomba huduma na si taasisi kama usemavyo hapa.

Tatizo ni kila taasisi kutaka kufanya biashara na kukusanya kodi wakati zingine zinafaa zitoe huduma tu
Hili wazo umetuwakilisha wengi, nilikuwa nawaza kuandika hoja inayofanana na hii.
Keywords ni KUTOA HUDUMA siyo kila kitu BIASHARA.
Kwani tunalipa kodi kwa kazi gani ikiwa kila huduma ya serikali iwe ya kulipia? Maana mwisho wa siku gharama hizi tutakuja kutozwa wananchi.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom