LadyRed
JF-Expert Member
- Mar 19, 2016
- 9,636
- 11,449
Tunakoelekea tutachunwa hadi ngozi🤦🏼♀️Hahahahaaaaaaq
Voda
Tigo
Airtel na wegine
Watakomaa
Ila.nao watatuumiza kwenye vifurushi kinomaaaa
Tunakoelekea tutachunwa hadi ngozi🤦🏼♀️Hahahahaaaaaaq
Voda
Tigo
Airtel na wegine
Watakomaa
Ila.nao watatuumiza kwenye vifurushi kinomaaaa
Taasisi za umma zimejivika joho la wakusanya mapato badala ya watoa huduma.Hili wazo umetuwakilisha wengi, nilikuwa nawaza kuandika hoja inayofanana na hii.
Keywords ni KUTOA HUDUMA siyo kila kitu BIASHARA.
Kwani tunalipa kodi kwa kazi gani ikiwa kila huduma ya serikali iwe ya kulipia? Maana mwisho wa siku gharama hizi tutakuja kutozwa wananchi.
Kama ni hivyo NIDA pia watulipe kwa "kuuza" taarifa zetu kwa watu wengine? Kwa nini wanataka kufanyia biashara taatifa zetu?
Na mwananchi ambaye ndiye chanzo cha taarifa hizo mnamlipaje? Maana bila mimi taarifa zangu hamuwezi kuzipata. Sasa naona mnataka kupiga hela kupitia mgongo wa mwananchi.MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imesema kuwa kuanzia mwezi huu wataanza kutoza fedha taasisi zote za umma na binafsi ambazo zinatumia taarifa za mamlaka hiyo kuhudumia wananchi
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa NIDA, Geofrey Tengeneza wakati akizungumza na The Guardian Digital
“Kuna wadau ambao wanatumia taarifa zetu kutoa huduma kwa wananchi napenda niwajulishe kuwa kuanzia mwezi huu (Julai, 2020) tunaanza kutoza tozo kwa taasisi zote za umma na binafsi ambazo zinatumia taarifa zetu kuhudumia wananchi mbalimbali”amesema Tengeneza na kuongeza kuwa;
“Kwa mfano makampuni ya simu, NSSF, Bima ya Afya, mabenki na wadau wengine mbalimbali ambao hili waweze kutoa huduma kwa wateja wao wanahitaji kupata taarifa kutoka kwetu ni lazima kuzilipia ili kuendelea kutoa huduma hiyo”amesema
Ameongeza kuwa taasisi hizo zinapaswa kuingia mkataba na NIDA ili kuweza kupata huduma hizo vinginevyo taasisi ambazo zitashindwa kutimiza matakwa hayo watasitisha huduma hiyo mara moja
Ameongeza kuwa tayari wametoa notisi kwa kampuni ambazo azijaingia mkataba na NIDA kufanya hivyo mpaka Julai 31, 2020 na kwa ambazo zitashindwa watasitisha huduma.
“Kampuni 17 tayari tumewatumia notisi kuanzia Agosti Mosi kama watakuwa hawajaleta maombi kwetu ili kuwapatia mkataba tutawakatia huduma pia tunaendelea kufanya upembuzi kujua ni makampuni gani wanatumia huduma zetu,”amesema
Amesema kuwa kwa hatua ya awali wanategemea kuingia mkataba na watumia taarifa za NIDA zaidi makampuni na taasisi 86.
Amesema kuwa utaratibu huo ni maelekezo kutoka kwa Serikali yalioelekeza NIDA kuanza kujitegemea kukusanya fedha kutumia utaratibu huo ili kuondokana na utaratibu wa kupata fedha za matumizi kutoka serikalini.
“Mpaka sasa kampuni 65 zimeleta maombi ya kusaini mkataba na pia tumepeleka mikataba kwa kampuni 36 bado hawajarudisha, pia makampuni 18 wamerudisha mikataba na 12 kati yao tayari tushasaini nao mkataba”amesema
mwisho wa siku ambaye atatozwa na hizo taasisi ni mwananchi/rai maskini.
Halafu anasimama mtu anajidai kusema hii ni serikali ya wanyongeeeGharama zote hapa zinashuka kwa muomba huduma
Ni kweli ni ya wanyonge sababu anawanyoga haswaHalafu anasimama mtu anajidai kusema hii ni serikali ya wanyongeee
Ulijiandikishia wapi na mwaka gani?huduma gani NIDA wenyewe wa hovyohovyo tangu 2017 hadi leo watu tunafuatilia vitambulisho vya NIDA tunapigiwa tu kalenda,benki ukipeleka namba ya nida wanataka copy ya kitambulisho na watu hawana