NICOL iwezeshwe iagize mafuta ili kuokoa upungufu wa mafuta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NICOL iwezeshwe iagize mafuta ili kuokoa upungufu wa mafuta

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Godwine, Aug 8, 2011.

 1. G

  Godwine JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kutokana na makampuni ya kuagiza mafuta kusita na kuendelea kutunishiana misuli na serikali , nadhani itakuwa ni busara kwa serikali kuikopesha NICOL shilingi bil 23 ambayo ni sawa na hisa za kampuni hii ndani ya banki ya NMB (6%) , jambo ili litawawezesha wananchi kuingia na kushika biashara ya mafuta na serikali kuwa salama.

  kutokana na kampuni hii kuingia kwenye soka la biashara ya mafuta itawezesha kuboresha usalama wa nchi kwani mafuta ni bidhaa muhimu na wageni wameanza kuitumia kama zana za kuiteketeza serikali yetu.

  lazima serikali sasa ianze kufikiri mbali na kuanza kuyawezesha makampuni ya kizalendo kushika uchumi wa nchi na kuacha kutegemea wageni kwani kwa hali ya uchumi wa sasa wa dunia , makampuni makubwa yameanza kuziyumbisha na kuzipindua nchi mbali mbali kwa sera za uchumi na udhibiti wa bidhaa na kusababisha mfumuko mkubwa wa bei na kusababisha maandamano ya wananchi na kudondoshwa kwa serikali hizo
   
 2. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,001
  Likes Received: 3,180
  Trophy Points: 280
  Hawa walishatuibia hela zetu za hisa,,unatakatena wapewe dili?
   
 3. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  hivi nicol si ndio wale walishindwa kusimamia miradi waliyoiazisha na kutia hasara mtaji wa wawekezaji wao?nadhani hata kwenye soko la hisa walisimamishwa,kama nimewachanganya na kampuni nyingine natanguliza samahani.
  lakini kwa maoni yangu kama hizo bilioni zipo kwanini wasipewe TPDC waagize hayo mafuta kama ilivyowahi kupendekezwa na bunge?
   
 4. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  Kweli, mkataba na /NICOL utakuwa kama mambo ya IPTL, SONGAS, UDA, nk!
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Aug 8, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,245
  Trophy Points: 280
  nicol wafanye hiyo kazi afu tpdc wafanye nini? na tpdc waliomba kufanya hii,manake wamebakia kusindikiza tu explorers!
   
 6. G

  Godwine JF-Expert Member

  #6
  Aug 8, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  NICOL walishindwa kuwekeza mtaji wao kwenye biashara salama ,lakini ninachopendekeza mimi hakitakuwa na madhara kwa serikali na kwa nicol na wanahisa wake kwani kama serikali wakiipa sh bil 23 na kukalia hisa za nicol ambazo ni asilimia sita 6% HISA za NMB wakishindwa inamaana hisa hizi zitatumika kuziba pengo la fedha za serikali pia fedha hizi ziwe kama stimulas package kwa kampuni hii ili iweze kurudi kwenye nafasi yake ya kawaida
   
 7. G

  Godwine JF-Expert Member

  #7
  Aug 8, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  wafanye kwa ubia na nicol kwani nicol ni kampuni ya kizalendo ambayo inaweza shirikiana na taasisi ya serikali
   
 8. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #8
  Aug 8, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  TPDC should solely monopolize the impotrtation of petrol and its products.
  The forgotten Transport Equalization Fund could be revived this way in order to have a pricing mechanism that is uniform all over Tz - siyo hii biashara uria.
   
 9. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #9
  Aug 8, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  so waliproove failure na katika miaka yote hiyo wamekaa kimya hawatoi hata tathmini ya biashara afu tuwape tena nyingine, yaani kweli wabongo hatujifunzi, ndio maana mtuhumiwa wa ufisadi ana kesi mahakama kuu lakini bado taasisi nyingine ya serikali (ileile iliyompeleka mahakamani) inampa tenda mtu huyo ya kuagiza matrekta ya kilimo kwanza
   
 10. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #10
  Aug 8, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,649
  Trophy Points: 280
  Duh!
  Kweli kuna watu wabishi,Zaidi ya Hizo Hisa za NMB , unaweza ukatuambia mafanikio mengine ya NICOL?
  Je ni niniThamani na mwendo wa hisa zao?
   
 11. G

  Godwine JF-Expert Member

  #11
  Aug 8, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  ata kama TPDC wakiagiza wao wenyewe tatizo litakuwa kwenye usamabazaji nao utasababisha utofauti wa bei, pia si busara kwa taasisi moja kuleta ukilitimba wa uagizaji na usambazaji bali kama shirika hili kwa kushirikiana na nicol wakijiingiza kwenye uagizaji kutakuwa na mafuta ya ziada na hivyo kutaondoa upungufu ambao ni chanzo cha kupanda kwa bei, pia wote tunajua mashirika ya kiserikali yanavyokuwa kama hakutakuwa na share na private sector , tulikuwa na TIPPER ambayo wajanja wachache wameiua
   
 12. G

  Godwine JF-Expert Member

  #12
  Aug 8, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  unajua wakati mwingine matatizo ni yetu sisi watanzania , kwa mfano nadhani wewe ni miongoni mwa wanahisa wa nicol lakini kama utawala wa nicol haufanyi kazi ipasavyo ungeweza kupeleka hoja kwenye mkutano mkuu na kuuondoa utawala uo na wewe kama kijana kuingia kwenye nafasi ya uongozi na kuleta mabadiliko.

  nitasikitika sana kusikia wanachama wa nicol wanalia kuhusu uendeshwaji mbaya wa kampuni hii wakati kwa utafiti wangu nimegundua ndani ya nicol kuna takribani wahitimu wa vyuo vikuu 3000 tena wengine kwenye fani za biashara na mainjinia sasa mnangoja nani aje awakuzie kampuni yenu zaidi ya nyinyi kuchukua ngazi na kuonyesha mfano kwa jamii kuwa kama kampuni ikilegalega nini cha kufanya.

  kuhusu mtaji nicol ina share 6% ya NMB ambayo ni takribani shs bil 23 , kwanini mnashindwa kuleta mfano mwema kwa kizazi chetu, nadhani kwa mtaji huu mnaweza ata kuanzisha benki na kuajiri watu wengi ndani ya kampuni hii


  msitumie muda mwingi kulalamika ni wakati wa vitendo , fanyeni sasa nasi tuige
   
 13. G

  Godwine JF-Expert Member

  #13
  Aug 8, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  NMB inathamani ya takribani bil 380 sasa asilimia sita 6% ni kama sh bil 22.8 hii ni takwimu ya mwezi wa pili
   
 14. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #14
  Aug 8, 2011
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  NICOL kwa sasa ipo kaburini inasubiri kufukiwa tu
  Nashangaa saana wakina Idd Simba, Sara Masasi, Mengi, Felix Mosha, Bomani na wale wote waliotushawishi tukanunua hisa, ilikula kwetu

  someni hii habari hapa

  Two months after being delisted from the Dar es Salaam bourse over financial misconduct, embattled National Investment Company Limited (Nicol) is now asking the High Court to lift an order that froze its bank accounts to save the company from total collapse.

  The public company, which faces expulsion from its Raha Tower Building offices over failure to pay $ 42,000 (about Sh63 million) rent, is pleading with the court to quash a decision by the Capital Markets and Securities Authority (CMSA) to block the sale of its shares in the National Microfinance Bank (NMB) for investment.

  Its landlord has asked the company to vacate the premises by August 21 if by then the debt is not paid.
  The filing of the suit comes five months after CMSA wrote to CRDB, NMB and Exim banks instructing them to block any cash outflows from its accounts to protect the interests of Nicol investors.

  Nicol says the freezing of its bank accounts has halted its operations and that it is likely to sink into more trouble if the orders which would enable it to meet its urgent financial obligations are not granted.

  The company argues that the attachment of its accounts violated Section 22 of the CMSA Act which stated that such bank accounts may be attached only if they are related to proceeds actually involved in violation of any of the provisions of CMSA Act.

  CMSA had, between December 2010 and January this year, carried out investigations into activities by Nicol and uncovered massive irregularities, including failure to maintain proper accounts.

  The authority then suspended its board of directors and chairman Felix Mosha and ordered the company to convene an annual general meeting. The company was also scrapped from the Dar es Salaam Stock Exchange (DSE) after it failed to tell its shareholders that a pharmaceutical company in which it has a 51 per cent stake was put into receivership late last year.

  Source; Citizen
   
 15. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #15
  Aug 8, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Matatizo makubwa zaidi ya watanzania ni kufikiri wewe utawekeza bila kufanta kazi.
  NICOL imekufa hilo kalina ubishi.
  Kwa upande mwingine ni wewe GODWINE kuchukua hii kama oppurtunity ya kufanya kile unachoeleza , kuagiza mafuta kama mtu binafsi.
  Mbona wengine wanafanya, tena kwa faida kubwa.Hivyo tusitegemee kuendelea kiuchumi kwa kupitia mgongo wa watu wengine bila sisis kufanya kazi.
   
 16. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #16
  Aug 8, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  NICOL inakaribia kufa Godwine wazo lako sikubaliani nalo hasa kwakuwa serikali ikiwakopesha NICOL ni kama inachukua pesa na kuzitia into a "sinking fund". Pengine ungelipendekeza shirika jengine au wazalendo wakopeshwe kuanzisha makampuni ya kuagiza mafuta. Tatizo la mafuta nchini linatokana na kukosekana kwa mamlaka ya kulinda watumiaji mafuta na monopolisation ya makampuni ya mafuta kwa kutumia umoja wao wa waagizaji mafuta. Ili kuvunja hii monopolisation lirudishwe shirika la TPDC ambalo litakuwa linaagiza mafuta lenyewe na kusambaza lenyewe kwa wauzaji wanaotaka kuuza mafuta nchini.

  Huo umoja una nguvu sasa hivi kwa kuwa hakuna muagizaji mwengine wa mafuta nchini, na wamekuwa wakilobby kuzuia shirika la TPDC lisianzishwa na mradi wa Bulk procurement usianze. Serikali ikiwa na mkono wa uagizaji na usambazi nguvu ya umoja huu itakufa na watabakia wauzaji mafuta nchini. USA ndio wanavyofanya na wameweza kucontrol vizuri bei za mafuta nchini mwao na sie tufanye hivyo ili kuwadhibiti hawa wezi wanaotumia migongo yetu kujipatia supernormal profit kwasababu tu hatujui bei gani wananunua mafuta yao.

  Pia ianzishwe mamlaka ya kulinda watumiaji wa huduma mbali mbali (Consumer Protection Bureau) na wapewe meno ya kuwashitaki na kuwadai fidia wale wote wanaolangua bidhaa zao au kutumia udanganyifu kufanya biashara. Consumer Protection Bureau ni kitu nimekuwa nakipigia kelele tangu mwaka juzi kuwa kitatusaidia sisi watumiaji dhidi ya wauzaji wasio na imani na tamaa ya kutajirika haraka. Lazima wauzaji wadhibitiwe ama sivyo matokeo yake ni kama haya sasa. Pia wanaathiri na uchumi wa nchi.
   
 17. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #17
  Aug 8, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,674
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  TPDC iagize mafuta,bei ikiwa poa zaidi ya wengine,retailers watanunua na kusambaza.....it's all about who sells what at what price.Let the govt compete with private sector.
   
 18. G

  Godwine JF-Expert Member

  #18
  Aug 8, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  @majoja

  kwa upande wangu nimetumia muda wangu mwingi kutenda kuliko kalalamika na nadhani kwa mwenendo wangu si mbaya lakini tambua kuna kitu wanakiita specilization(base on core activities) kwa hiyo kitendo cha kuachana na shughuli unazozifanya na kurukia zingine husababisha usumbufu wa namna fulani.

  lakini kwa nicol na wengine ambao hawajachagua cha kufanya nadhani ni miongoni mwa fulsa mzuri kuingia kwenye sector hii, kwani risk yake ni ndogo kulinganisha na biashara zingine.

  nitasikitika kama jamii hasa wanachama wa nicol ninawaona wanaendelea kukata tamaa na kupoteza lengo la biashara na kudhani mtaji wao umezama na kuishia kulalamika tu.


  hakika taifa ili linaelekea pabaya kama tukiacha biashara ya mafuta mikononi mwa wageni kwani kadri siku zinapoenda ndio kaburi la nchi hii linaendelea kukamilika,

  ni wakati wa kila mtanzania na kila kampuni ya kizalendo kuhakikisha ya kuwa biashara ya mafuta inakuwa mikononi taifa na wazalendo la sivyo tungoje, machafuko na mfumuko wa bei wa kutisha
   
 19. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #19
  Aug 8, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,391
  Trophy Points: 280
  habari ya uhakika TPDC wameshaonywa wasiingilie biashara ya mafuta kwani makampuni ya mafuta kwa sasa ni ya waheshimiwa mafisadi!hivyo wao waangalie gesi tuu na utafiti wa mafuta!
   
 20. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #20
  Aug 8, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,674
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Why NICOL?
   
Loading...