Nichukue hatua gani?

G8M8

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
432
389
Poleni na mihangaika ya hapa pale ndugu.

Nimeanza kilimo cha bustani hasa mchicha lakini nakutana na changamoto kubwa hivi sasa mchicha wangu upo hatua ya kuvuna una majuma matatu hadi sasa changamoto Kuna ugonjwa umetokea kwenye majani ya mchicha wangu karibia wote niloanza kuupanda.

Majani yametoka ukungu kama unga mkavu meupe chini ya majani kwa juu inaonekana kama mabaka ya njano hivi kwa mbali.. Ushauri nichukue hatua gani nifanye kitu gani maana pia kuna mchicha mwengine nilioanza kupanda now una siku kumi na 2 tu. Situmii dawa sijawahi tumia dawa zaidi ya mbolea na kumwagalia.

Ushauri wandugu maana umenipa stress sana.
 
Picha hizo

IMG_20190807_131500.jpeg
 
Upo mkoa gani? Mbolea ipi unatumia ya kuku? Umejaribu kubadili mbegu?
Hapo unapolima pamewahi kulimwa hilo zao? Je alipata changamoto kama yako?
 
Upo mkoa gani?
Mbolea ipi unatumia ya kuku?
Umejaribu kubadili mbegu?
Hapo unapolima pamewahi kulimwa hilo zao? Je alipata changamoto kama yako?
Nipo tanga ndio nimeanza kulima kwa hiyo mbegu (amaranthus dubious) hajawahi limwa ilo eneo ndio nimelianza mm.. Mbolea kuku mbuzi na N'gombe nilitumia zote...
 
Nipo tanga ndio nimeanza kulima kwa hiyo mbegu (amaranthus dubious) hajawahi limwa ilo eneo ndio nimelianza mm.. Mbolea kuku mbuzi na N'gombe nilitumia zote...
Tumia mbolea ya kuku. Nenda duka la dawa wakushauri dawa gani nzuri. Kwa sababu hapakuwahi limwa mchicha so badae utaacha kutumia dawa pakitengamaa.
 
Kama hujalima eneo kubwa fanya hivi tafuta siku moja ya wiki ambayo utatwanga muarobaini na mbegu zake chuja maji yake kiasi cha kiganja kimoja kwa tuta moja halafu changanya halafu changanya na majivu kama kiganja kimoja nyunyizia wakati wa jioni. Tumia hii mara moja kwa wiki kabla ugonjwa haujaanza. Mimi huwa siweki dawa na kwa njia hiyo nimeondoa wadudu wengi tafuta maua yanaitwa marigold panda kuzunguka matuta yako wadudu hawapendi harufu yake watakimbia pia unaweza kutafuta dawa yenye mkojo wa sungura fwata maelekezo yake hiyo ni kiboko. Dawa nyingine ni alcohol 30% and water 70 ila bado ni ngumu kutoa maana itabdi ugeuze majani ndio upige
 
Jaribu kuangalia maji unayotumia hayana asili ya chumvi. Mm iliwahi nitokea ila maji ndio ilikua sababu
Haya maji yanayo asili ya chumvi kwa sababu ni ya kisima lakini yametokana hasa na mvua... Sijajua kiasi cha chumvi na sasa hivi hadi mchicha wa weak moja unaonyesha haya madhara naona kabisa.. Sipati kitu... ww ulichukua hatua gani baada ya kugungua hilo tatizo mkuu
 
Kama hujalima eneo kubwa fanya hivi tafuta siku moja ya wiki ambayo utatwanga muarobaini na mbegu zake chuja maji yake kiasi cha kiganja kimoja kwa tuta moja halafu changanya halafu changanya na majivu kama kiganja kimoja nyunyizia wakati wa jioni. Tumia hii mara moja kwa wiki kabla ugonjwa haujaanza. Mimi huwa siweki dawa na kwa njia hiyo nimeondoa wadudu wengi tafuta maua yanaitwa marigold panda kuzunguka matuta yako wadudu hawapendi harufu yake watakimbia pia unaweza kutafuta dawa yenye mkojo wa sungura fwata maelekezo yake hiyo ni kiboko. Dawa nyingine ni alcohol 30% and water 70 ila bado ni ngumu kutoa maana itabdi ugeuze majani ndio upige
Asante Sana. Je, ulishawahi patwa na hiyo changamoto kwako ww?
 
Back
Top Bottom