Nianzie wapi kutafuta ajira kwa Dar es salaam

Hornet

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
23,385
2,000
Naomba mwendelezo ili kesho alfajiri niamkie hapo. Yaani mm nipo mbagala nataka kufika ilala je ni ilala ya wapi na kwenye nn naomba nimalizie mkuu

Ilala sokoni unashukia pale
Kuna kushusha mizigo kubeba

Kama una kamtaji unaweza kuchukua Macao kwenye gari ukauza chini
Au mtaani
 

IGUDUNG'WA

JF-Expert Member
Oct 22, 2011
2,072
2,000
umetokea mwanza sehemu gani? maana hako kakauli kakupuna tumekatumia sana mwanza enzi za utoto
Umemshauri vizuri sana....lakini huko nako lazima akutane na purukushani sio rahisi kihivyo...


Na hapo bado hajakutana na Dadaz' wa mjini...watampuna hela zote asipokuwa makini....
 

Kamera

Senior Member
Sep 27, 2018
167
250
Uza hio smartphone uanzishe biashara ndogondogo kulingana na mazingira yako unayoishi. unaweza kuchoma maindi maana msimu wa mvua upo karibu au kuuza pweza maana inanyweka sana pia hata kuuza karanga.

Jitahidi kusoma alama za nyakati usije ukajiingiza kwenye biashara ya kuuza juice au maji baridi msimu huu wa kuelekea mvua. karibu sana sana mjini na haiitaji PHD ili kuishi mji huu ni ujanjaujanja tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom