Nianze na kuku wa aina gani kwa mtaji wa Tshs 400000

Mkuu nipe iyo laki nne nipige mzigo forex Nina uhakika ndani ya wiki tatu tu nitapata faida zaidi ya Mara tatu yake ..nakupa laki nne yako na kamisheni kidgo kwa jinsi tutakavyo kuwa tumekubaliana..
 
Nadhani umeweka hukumu kwa kuzingatia unachofahamu tu. Huenda ikawa zaidi ya hapo. Mtu aweza fanikiwa kwa kufuga hao chotara au kienyeji na akafanikiwa vilevile. Na mwingine aweza fuga hao "wa kibiashara" na asifanikiwe.

Mafanikio hutokana na mambo mengi ambayo kwa sehemu kubwa yanamhusu mjasiriamali/mfugaji mwenyewe;

1. Malengo. Kuwa na lengo sahihi linalotekelezeka. Usifuge kwa kuwa tu umepata mtaji wa hiyo laki nne kwa mfano. Je unapenda ufugaji?

2. Utafiti. Fanya utafiti kuhusu mradi/lengo lako ili ubaini ikiwa lengo lako linatekelezeka. Tambua 'breed' sahihi ya kwenda nayo kwa kuzingatia malengo yako.

3. Maarifa. Hakikisha unafanya rejea ya kutosha juu ya mradi wako. Usiishie tu kujua ABC's za ufugaji, utafeli vibaya. Tafuta A, B, C, mpaka Z.

4. Msukumo, kujiamini, mtazamo, na sifa nyingine binafsi za mjasiriamali. Hakikisha hizo zote unazo au unakuwa nazo.

Narudia. Hufanikiwi kwa kuwa tu unafanya kitu ambacho ndiyo habari ya mjini (broilers & layers). Unafanikiwa kwa kuwa una mipango thabiti. Kila kitu ni mipango (planning).
Pia umetaja aina za kuku.

Kumbuka kuku wa Biashara ni wawili tu.
1. Brouler
2. Layers.

Hao ndo kuku kwa ajili ya biashara au kwa ajili ya kupata pesa

Kuku chotara na kuku wa kienyeji ni kwa ajili ya kuondoa umasikini tu.
 
Nadhani umeweka hukumu kwa kuzingatia unachofahamu tu. Huenda ikawa zaidi ya hapo. Mtu aweza fanikiwa kwa kufuga hao chotara au kienyeji na akafanikiwa vilevile. Na mwingine aweza fuga hao "wa kibiashara" na asifanikiwe.

Mafanikio hutokana na mambo mengi ambayo kwa sehemu kubwa yanamhusu mjasiriamali/mfugaji mwenyewe;

1. Malengo. Kuwa na lengo sahihi linalotekelezeka. Usifuge kwa kuwa tu umepata mtaji wa hiyo laki nne kwa mfano. Je unapenda ufugaji?

2. Utafiti. Fanya utafiti kuhusu mradi/lengo lako ili ubaini ikiwa lengo lako linatekelezeka. Tambua 'breed' sahihi ya kwenda nayo kwa kuzingatia malengo yako.

3. Maarifa. Hakikisha unafanya rejea ya kutosha juu ya mradi wako. Usiishie tu kujua ABC's za ufugaji, utafeli vibaya. Tafuta A, B, C, mpaka Z.

4. Msukumo, kujiamini, mtazamo, na sifa nyingine binafsi za mjasiriamali. Hakikisha hizo zote unazo au unakuwa nazo.

Narudia. Hufanikiwi kwa kuwa tu unafanya kitu ambacho ndiyo habari ya mjini (broilers & layers). Unafanikiwa kwa kuwa una mipango thabiti. Kila kitu ni mipango (planning).
Nimepata kitu hapa
 
Nimechelewa lakini ushauri wangu ni huu: kama banda lipo tayari, basi nunua kuroila wa angalau mwezi mmoja, kwa hiyo 400K nashauri utumie 250K kwa kununua majogoo 50 tu, anza kufuga mwezi angalau wa 6, hapa lengo ni mwezi wa 12 msimu wa sikukuu, utauza kila jogoo sh. 20,000×50=1,000,000, ile 150K iliyobakia kwenye mtaji ndio uitumie kwa ajili ya chakula cha kuku.Kwa maana hiyo sales itakua Mil 1 toa cost of good sold 400,000 utabakbna gross profit ya laki sita.
 
Asante kwa mchango makini
 
Haya mkuu, ngoja nipambane. Nitakuja na mrejesho maana nimejiwekea lengo by december niwe na kuku zaidi ya 400. Na siongezi kununua, nacheza na hawa hawa wazaliane. Nimeweka lengo by december 2020 nitakuwa na kuku 1000. Hapo sitataka wazidi hapo, nitakuwa napunguza kwa kuwauza.
Mkuu hebu tupe mrejesho, washafika wangapi huko?
 
Unataka nikutajie idadi au nisindikize na picha kabisa ili uamini.
Endeleeni kulalamika kwenye keyboard na kukatishana tamaa
Sina hakika kama alikua na nia mbaya (negativity). Wewe ni kioo kwetu wafugaji wadogo.
 
Numbers don't lie. Mpe number muulizaji then nia zake zote alizokuwa nazo ktk swali lake zitapata jawabu sahihi.
 
Sina hakika kama alikua na nia mbaya (negativity). Wewe ni kioo kwetu wafugaji wadogo.

Mimi nafuga free range system, maana aneo linaruhusu, lakini nawalisha pia.
nilinunua tetea 1 na jogoo 1 mwezi January. Mwezi march nikanunua tetea 2, April- 2,Mei-2 na June-2. Ukihesabu jumla ni 9. Nilichofanya nilikuwa natafuta tetea ambaye hajawahi kutaga lakini aliyekaribia sana kutaga, ndani ya mwezi mmoja anataga.
Nimeshuhudia kumwekea kuku mmoja mayai 14 akatotoa 12, mwingine namwekea 10 anatotoa 9, mwingine namwekea 10 anatotoa yote. Mwingine namwekea 9 na anatoa yote. Unamwekea kuku mayai ya kulalia kulingana na umbile la kuku.
Mwezi wa nane tulipata changamoto mimi na mke wangu wote kutokuwepo nyumbani kwa muda kutokana na social problems, pakatokea vifo vya vifaranga kama 15 hivi kwa ajili ya baridi na mafua.
Ila maendeleo ni mazuri maana nina kuku 120 sasa hivi. Nina tetea kama 60 ambao bado hawajaanza kutaga na ambao kati ya november na december watakuwa wanataga. Muda si mrefu nitakuwa nakusanya mayai 40 kwa siku. Nitaendelea kuwapa feedback. Ila si njia rahisi, wakitotolewa vifaranga 12 au 10 kwa kuku mmoja jiandae kisaikolojia kupoteza kati ya 2 hadi 4 kwa sababu mbali mbali. Pasingetokea kifo chochote cha kifaranga leo hii ningekuwa na 150, ila lazima ujue hakuna kazi isiyo na changamoto.
 
Mungu akubariki sana. Tutawasiliana maana naanza kufuga, nimepata eneo (150, 000)
 
Important tips.
  • Kuku anapotaga usisogeze mayai ukayaweka kwenye tray. Acha yakae hapo hapo.
  • Kuku hutaga mayai kuanzia 10 na kuendelea kabla hajalalia. Inatakiwa alalie mayai yaliyotagwa ndani ya siku 10 ndiyo yana ubora zaidi.
  • Kuna kuku wanataga mayai hadi 20 mpaka 30 ndipo alalie. Jifunze kuweka alama kila yai linalotagwa kwa kuandika namba au tarehe, ili yakifika zaidi ya kumi kama bado anaendelea kutaga, yai la kwanza kutagwa unaweza kula, uza au kama kuna kuku mwingine analalia mwekee, ili huyo atakapokuwa analalia umwekee ambayo ni recent.
  • Mayai yenye shape ambazo siyo nzuri kama round, au dogo sana au ambalo ganda lake haliko vizuri, au ni chafu sana lisilaliwe.
  • Kiota cha kutagia, ambacho ndicho cha kulalia kiwe na privacy, lisiwe eneo la wazi
  • Kiota kisiwe eneo la flat kama sakafuni, tengeneza kwa namna ya kuhakikisha mayai hayatawanyiki, katikati kibonde kidogo, pembezoni nyanyua kidogo ili kuku anapolalia aweze kuyafunika vizuri mayai yake na joto lisipotee. Unaweza kutumia udongo au material mengine.
  • Kuku wapate chakula kizuri, maji masafi, chanjo kwa wakati na madawa pale unapoona dalili mapema
  • Dhibiti vifaranga wasichukuliwe na mwewe, vicheche, na magonjwa ya baridi
  • Usafi wa banda muhimu sana
 
Asante sana mkuu
 
Kubwa la kujifunza ni namna ya kulea vifaranga. Mwezi uliopita nimepoteza takribani vifaranga 35, iliniuma sanaaaa! Mwisho niligundua makosa yangu kwani niliwatenga na mama zao mapema mno wiki 2 hivi nikawaweka kwenye box huku niwawashia chemli.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom