Nianze na kuku wa aina gani kwa mtaji wa Tshs 400000

Mkuu acha mm niotee kuwa banda unalo, ngoja nikupe estimates kutokana na uzoefu wangu mdogo ktk kufanya hii shughuli (hands on experience) ingawa si ya muda mrefu sana.

Assume unanunua layers 250 ambao kama utafanikiwa kuwatunza vizuri tuseme kwa efficiency ya 90% mpaka wakati wa kutaga uwe na kuku hai na wanaotaga kati ya 200 na 220, uwe na uwezo wa kupata angalau trei 7 kwa siku.

Bei (Tsh) nitakazoziweka ni makisio lkn yanayokaribiana na ukweli.

Vifaranga 250@2,300/ = 575,000/-

Chakula Starter
Wiki ya 1 hadi ya 7 mifuko 4 (50kg) @58,000/ = 232,000/-

Chakula Grower
Wiki ya 8 hadi 11 mifuko 11 (50kg) @ 46,000/ = 506,000/-

Wiki ya 12 hadi ya ya 16 mifuko 14 @ 46,000/ = 644,000/

Wiki ya 17 hadi ya 20 jumla ya mifuko ya chakula 14 hapa nachanganya 7 (grower) na 7 (layers)
- 7 (grower) @ 46,000/ = 322,000/
- 7 (layers) @ 50,000/ = 350,000/

Chakula Layers
Wiki ya 21 hadi ya 28 mifuko 34 @ 50,000/ = 1,700,000/-

Assumption ni kuwa by wiki ya 28 kuku watakuwa wameshaanza kutaka na wanajilisha wenyewe.

Jumla yote ni 4,329,000/-

Hapa bado gharama za chanjo na madawa yatakayohitajika pamoja na posho ya mtu atakayekuwa anawahudumia kama si ww mwenyewe.
Duuu hapo umempoteza mazima.
 
Nachojua katika kitu chochote hutakiwi kuanza pakubwa, 400k unaweza kuanza na kufuga ila usiexpect pakubwa mara moja, nunua kuku chotara wa5 au 6 wakubwa mmoja akiwa jogoo, andaa mabanda mazuri na safi, nunua chakula bora pamoja na chakula cha kuboost kuku kutaga, baada ya muda wataanza kutaga kumbuka kuwaandalia mahali pazuri pakutagia kisha collect mayai kila wanapotaga,maana yake kila siku tutakuwa tunaexpect mayai matano au 4 ambapo kwa ck 6 ni 30 au 24,peleka kutotolesha ukipata vifaranga andaa mabanda yakuwalea wew mwenyew....

Cycle io itaendelea na kujikuta baada ya miez almost 6 mpk mwaka ukawa na zaidi ya kuku 150+
 
Mkuu Hongera kwa Jitihada kwanza. Pili kwa huo mtaji ili ku Break even au kupata faida itakuchukua muda mrefu sana.

Na pia kama ndo unategemea hiyo basi itakuwa shida sana.

Kwenye Biashara ya Kuku tusema Value Chain yake kuna mambo mengi sana.

1. Wauza madawa ya kuku
2. Wauza vifaa vya kuku kama Drinker na kadhalika.
3. Wanunuzi wa kati.
4. Wauza vifaranga
5.Wauza vyakula
6. Waongeza thamani na kadhalika.

So kwa mtaji huo unaweza sio lazima na wewe ufuge unaweza anzia pale ambapo wenzako wameisha.
Wenzako si wanaishia kwenye kufuga basi anzi pale. Au kwenyr mayai anzia pale wanapo ishia wao.

Unaweza ukawa unanunua mayai na ku resale hata ukipata faida sh 1000 kila trei bado ni kubwa sana make hukuwa nayo hiyo 1000.

Hii inaweza kuza mtaji zaidi. Kufuga ni Changamoto na ili upate faida unahitaji mtaji mkubwa sana

Ni hayo tu
Mkuu uko nondo sanaa
 
soko unalo ?, soko ndio kila kitu.., to wet your feet kama unaweza na margin ipo anza kwa kununua na kuuza uone kama biashara inakufaa.., na utakapoanza anza kidogo kidogo kama learning curve.., usije ukaingia mazima ukaua mtaji...

Kuna wafugaji wa kutosha wamefanikiwa..., pia kuna waliojaribu kufuga wengi tu wakalia kilio cha kusaga meno.., ili kujua wewe ni yupi kati ya hao anza kidogo kidogo
 
Huu uzi wako nimeuona tangu siku uliyopost ila sikuwa na muda wa kutoa mchango wangu, naomba leo nikujibu.
Iko hivi, kwanza ili kuamua uanze na kuku wa aina gani lazima uamue kufanya tathmini ya soko lako.
  1. Wateja unaowalenga ni wenye kuhitaji aina gani ya kuku au mayai?
  2. Eneo la kufugia likoje? Kama uko sehemu inayobana itabidi uwafugie ndani tu kwenye banda, hivyo ni busara ufuge chotara au wa kisasa (broilers au layers). Kama uko sehemu ya wazi kama vile shambani eneo kubwa nakushauri fuga kienyeji utafaidi sana. Maana utawaachia tu nje muda mwingi wanajitafutia chakula wakirudi utawaongezea kidogo,.
  3. Kuna gharama za banda kwa ajili ya usalama, sijui kama umejipangaje. Wafugaji wengi wanapenda kujenga mabanda ambayo ni gharama nafuu lakini inawagharimu sana baadaye kwa kuku kuibiwa. Mfano banda la mabanzi au bati na nyavu tuu. Kuna mtu alifuga kuku wakafikia 40 alafu wakachukuliwa wote kwa usiku mmoja. Ni vyema ukajenga banda imara lenye usalama wa 98% kama ilivyo nyumba yako ya kuishi.
  4. Ufugaji wa kuku ni progresive project ambayo inakua kwa spidi ya haraka. Kwa hiyo ni bora ukaanza kidogo sana. Kama ni kienyeji pure breed anza na hata kuku kumi tu au pungufu na jogoo mmoja. Nikupe uzoefu wangu. Nilianza na tetea mmoja na jogoo mmoja mwezi january mwaka huu. Mwezi wa 3 nikaongeza tetea 2, mwezi wa nne nikaongeza zingine 2, mwezi wa tano nikaongeza tena 2, na june nikaongeza 2. Sasa hivi vifaranga wa kwanza kabisa wameshakuwa wakubwa na wanatetea tayari kwa kuanza kutaga. Huku nina vifaranga vingine takriban 50 kutokana na hao tetea ambao idadi yao ni chini ya 10. Hao ninaosema ni vifaranga wengine mwezi ujao wataanza kutetea, wengine mwezi mwingine na kuendelea. Sasa hivi wengine wanne wanalalia, kwa maana nyingine baada ya wiki 2 zijazo idadi ya vifaranga itafikia 90. Bada ya muda mfupi ujao idadi itapanda na kufikia mara tatu au nne kwa muda mfupi sana. Ukuaji huu unatakiwa uendane na upanuzi wa miundo mbinu. Faida niliyo nayo nina eneo kubwa sana la kuwalishia kwa hiyo asubuhi wanatoka huko nje wanazurura na kuokota mchwa, wadudu wengine na pia majani. Wakirudi nawarushia mikono mikono miwili ya mahindi na mkono mmoja wa ngano au mtama. Baada ya hapo nawawekea hydroponics ambazo nimetengeneza mwenyewe kutokana na ngano. Then wanarudi tena kwenye mizunguko yao. Ni burudani tuu.
  5. Muhimu kuzingatia chanjo na daa za minyoo kwa wakati. Usidharau, hata kama una kuku 10 tuu, wape chanjo sahihi kwa wakati sahihi. Pia dawa ya minyoo itasaidia sana uzalishaji usishuke.
  6. Muombe Mungu akupiganie,
  7. Jitahidi kudhibiti wanyama hatarishi kama mwewe na vicheche (kama ufugaji wako ni huria).
Niishie hapo kwa leo
Kwa kukazia tu hapo ni kweli kabisa kuku wa kienyeji kama hutakuwa makini kwenye vifaranga utaishia kuwaona kuku wakubwa tu, handling ya vifaranga 50 is not a joke kama hujaweka sawa mazingira
 
Haya mkuu, ngoja nipambane. Nitakuja na mrejesho maana nimejiwekea lengo by december niwe na kuku zaidi ya 400. Na siongezi kununua, nacheza na hawa hawa wazaliane. Nimeweka lengo by december 2020 nitakuwa na kuku 1000. Hapo sitataka wazidi hapo, nitakuwa napunguza kwa kuwauza.
Mkuu shukrani kwa mchango wako hapa, nimepitia threads zako zote za zamani , ulikua na visa sana na mabalaa . Siku hizi umepunguza sana kuandika humu jukwaani
 
Huu uzi wako nimeuona tangu siku uliyopost ila sikuwa na muda wa kutoa mchango wangu, naomba leo nikujibu.
Iko hivi, kwanza ili kuamua uanze na kuku wa aina gani lazima uamue kufanya tathmini ya soko lako.
  1. Wateja unaowalenga ni wenye kuhitaji aina gani ya kuku au mayai?
  2. Eneo la kufugia likoje? Kama uko sehemu inayobana itabidi uwafugie ndani tu kwenye banda, hivyo ni busara ufuge chotara au wa kisasa (broilers au layers). Kama uko sehemu ya wazi kama vile shambani eneo kubwa nakushauri fuga kienyeji utafaidi sana. Maana utawaachia tu nje muda mwingi wanajitafutia chakula wakirudi utawaongezea kidogo,.
  3. Kuna gharama za banda kwa ajili ya usalama, sijui kama umejipangaje. Wafugaji wengi wanapenda kujenga mabanda ambayo ni gharama nafuu lakini inawagharimu sana baadaye kwa kuku kuibiwa. Mfano banda la mabanzi au bati na nyavu tuu. Kuna mtu alifuga kuku wakafikia 40 alafu wakachukuliwa wote kwa usiku mmoja. Ni vyema ukajenga banda imara lenye usalama wa 98% kama ilivyo nyumba yako ya kuishi.
  4. Ufugaji wa kuku ni progresive project ambayo inakua kwa spidi ya haraka. Kwa hiyo ni bora ukaanza kidogo sana. Kama ni kienyeji pure breed anza na hata kuku kumi tu au pungufu na jogoo mmoja. Nikupe uzoefu wangu. Nilianza na tetea mmoja na jogoo mmoja mwezi january mwaka huu. Mwezi wa 3 nikaongeza tetea 2, mwezi wa nne nikaongeza zingine 2, mwezi wa tano nikaongeza tena 2, na june nikaongeza 2. Sasa hivi vifaranga wa kwanza kabisa wameshakuwa wakubwa na wanatetea tayari kwa kuanza kutaga. Huku nina vifaranga vingine takriban 50 kutokana na hao tetea ambao idadi yao ni chini ya 10. Hao ninaosema ni vifaranga wengine mwezi ujao wataanza kutetea, wengine mwezi mwingine na kuendelea. Sasa hivi wengine wanne wanalalia, kwa maana nyingine baada ya wiki 2 zijazo idadi ya vifaranga itafikia 90. Bada ya muda mfupi ujao idadi itapanda na kufikia mara tatu au nne kwa muda mfupi sana. Ukuaji huu unatakiwa uendane na upanuzi wa miundo mbinu. Faida niliyo nayo nina eneo kubwa sana la kuwalishia kwa hiyo asubuhi wanatoka huko nje wanazurura na kuokota mchwa, wadudu wengine na pia majani. Wakirudi nawarushia mikono mikono miwili ya mahindi na mkono mmoja wa ngano au mtama. Baada ya hapo nawawekea hydroponics ambazo nimetengeneza mwenyewe kutokana na ngano. Then wanarudi tena kwenye mizunguko yao. Ni burudani tuu.
  5. Muhimu kuzingatia chanjo na daa za minyoo kwa wakati. Usidharau, hata kama una kuku 10 tuu, wape chanjo sahihi kwa wakati sahihi. Pia dawa ya minyoo itasaidia sana uzalishaji usishuke.
  6. Muombe Mungu akupiganie,
  7. Jitahidi kudhibiti wanyama hatarishi kama mwewe na vicheche (kama ufugaji wako ni huria).
Niishie hapo kwa leo
Asante hata mm nimepata kitu kutoka kwako .barikiwa sana
 
Mkuu post yako nimeielewa vizuri.
Ila Niko na swali moja,ufugaji Kama ambao unafanya wewe mtu anatakiwa awe na eneo la kuanzia ukubwa gani?
Kwa mfano Mimi kaeneo kangu kana ukubwa wa mita 13x15.
Eneo kama hili linafaa zaidi kwa ufugaji wa kuku wa aina gani?
 
Mkuu acha mm niotee kuwa banda unalo, ngoja nikupe estimates kutokana na uzoefu wangu mdogo ktk kufanya hii shughuli (hands on experience) ingawa si ya muda mrefu sana.

Assume unanunua layers 250 ambao kama utafanikiwa kuwatunza vizuri tuseme kwa efficiency ya 90% mpaka wakati wa kutaga uwe na kuku hai na wanaotaga kati ya 200 na 220, uwe na uwezo wa kupata angalau trei 7 kwa siku.

Bei (Tsh) nitakazoziweka ni makisio lkn yanayokaribiana na ukweli.

Vifaranga 250@2,300/ = 575,000/-

Chakula Starter
Wiki ya 1 hadi ya 7 mifuko 4 (50kg) @58,000/ = 232,000/-

Chakula Grower
Wiki ya 8 hadi 11 mifuko 11 (50kg) @ 46,000/ = 506,000/-

Wiki ya 12 hadi ya ya 16 mifuko 14 @ 46,000/ = 644,000/

Wiki ya 17 hadi ya 20 jumla ya mifuko ya chakula 14 hapa nachanganya 7 (grower) na 7 (layers)
- 7 (grower) @ 46,000/ = 322,000/
- 7 (layers) @ 50,000/ = 350,000/

Chakula Layers
Wiki ya 21 hadi ya 28 mifuko 34 @ 50,000/ = 1,700,000/-

Assumption ni kuwa by wiki ya 28 kuku watakuwa wameshaanza kutaka na wanajilisha wenyewe.

Jumla yote ni 4,329,000/-

Hapa bado gharama za chanjo na madawa yatakayohitajika pamoja na posho ya mtu atakayekuwa anawahudumia kama si ww mwenyewe.
Kama na hivi naacha kufuga aises
 
Mkuu post yako nimeielewa vizuri.
Ila Niko na swali moja,ufugaji Kama ambao unafanya wewe mtu anatakiwa awe na eneo la kuanzia ukubwa gani?
Kwa mfano Mimi kaeneo kangu kana ukubwa wa mita 13x15.
Eneo kama hili linafaa zaidi kwa ufugaji wa kuku wa aina gani?

Hilo eneo dogo kwa free range. Kama unawafugia wenye banda space inatakiwa mita moja ya mraba kuku wanne.
 
Huu uzi wako nimeuona tangu siku uliyopost ila sikuwa na muda wa kutoa mchango wangu, naomba leo nikujibu.
Iko hivi, kwanza ili kuamua uanze na kuku wa aina gani lazima uamue kufanya tathmini ya soko lako.
  1. Wateja unaowalenga ni wenye kuhitaji aina gani ya kuku au mayai?
  2. Eneo la kufugia likoje? Kama uko sehemu inayobana itabidi uwafugie ndani tu kwenye banda, hivyo ni busara ufuge chotara au wa kisasa (broilers au layers). Kama uko sehemu ya wazi kama vile shambani eneo kubwa nakushauri fuga kienyeji utafaidi sana. Maana utawaachia tu nje muda mwingi wanajitafutia chakula wakirudi utawaongezea kidogo,.
  3. Kuna gharama za banda kwa ajili ya usalama, sijui kama umejipangaje. Wafugaji wengi wanapenda kujenga mabanda ambayo ni gharama nafuu lakini inawagharimu sana baadaye kwa kuku kuibiwa. Mfano banda la mabanzi au bati na nyavu tuu. Kuna mtu alifuga kuku wakafikia 40 alafu wakachukuliwa wote kwa usiku mmoja. Ni vyema ukajenga banda imara lenye usalama wa 98% kama ilivyo nyumba yako ya kuishi.
  4. Ufugaji wa kuku ni progresive project ambayo inakua kwa spidi ya haraka. Kwa hiyo ni bora ukaanza kidogo sana. Kama ni kienyeji pure breed anza na hata kuku kumi tu au pungufu na jogoo mmoja. Nikupe uzoefu wangu. Nilianza na tetea mmoja na jogoo mmoja mwezi january mwaka huu. Mwezi wa 3 nikaongeza tetea 2, mwezi wa nne nikaongeza zingine 2, mwezi wa tano nikaongeza tena 2, na june nikaongeza 2. Sasa hivi vifaranga wa kwanza kabisa wameshakuwa wakubwa na wanatetea tayari kwa kuanza kutaga. Huku nina vifaranga vingine takriban 50 kutokana na hao tetea ambao idadi yao ni chini ya 10. Hao ninaosema ni vifaranga wengine mwezi ujao wataanza kutetea, wengine mwezi mwingine na kuendelea. Sasa hivi wengine wanne wanalalia, kwa maana nyingine baada ya wiki 2 zijazo idadi ya vifaranga itafikia 90. Bada ya muda mfupi ujao idadi itapanda na kufikia mara tatu au nne kwa muda mfupi sana. Ukuaji huu unatakiwa uendane na upanuzi wa miundo mbinu. Faida niliyo nayo nina eneo kubwa sana la kuwalishia kwa hiyo asubuhi wanatoka huko nje wanazurura na kuokota mchwa, wadudu wengine na pia majani. Wakirudi nawarushia mikono mikono miwili ya mahindi na mkono mmoja wa ngano au mtama. Baada ya hapo nawawekea hydroponics ambazo nimetengeneza mwenyewe kutokana na ngano. Then wanarudi tena kwenye mizunguko yao. Ni burudani tuu.
  5. Muhimu kuzingatia chanjo na daa za minyoo kwa wakati. Usidharau, hata kama una kuku 10 tuu, wape chanjo sahihi kwa wakati sahihi. Pia dawa ya minyoo itasaidia sana uzalishaji usishuke.
  6. Muombe Mungu akupiganie,
  7. Jitahidi kudhibiti wanyama hatarishi kama mwewe na vicheche (kama ufugaji wako ni huria).
Niishie hapo kwa leo
Hapo kwenye dawa na chanjo na Hydroponic kuna udadavuzi kidogo unaweza toa....?
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom