Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 3,791
- 3,360
Duuu hapo umempoteza mazima.Mkuu acha mm niotee kuwa banda unalo, ngoja nikupe estimates kutokana na uzoefu wangu mdogo ktk kufanya hii shughuli (hands on experience) ingawa si ya muda mrefu sana.
Assume unanunua layers 250 ambao kama utafanikiwa kuwatunza vizuri tuseme kwa efficiency ya 90% mpaka wakati wa kutaga uwe na kuku hai na wanaotaga kati ya 200 na 220, uwe na uwezo wa kupata angalau trei 7 kwa siku.
Bei (Tsh) nitakazoziweka ni makisio lkn yanayokaribiana na ukweli.
Vifaranga 250@2,300/ = 575,000/-
Chakula Starter
Wiki ya 1 hadi ya 7 mifuko 4 (50kg) @58,000/ = 232,000/-
Chakula Grower
Wiki ya 8 hadi 11 mifuko 11 (50kg) @ 46,000/ = 506,000/-
Wiki ya 12 hadi ya ya 16 mifuko 14 @ 46,000/ = 644,000/
Wiki ya 17 hadi ya 20 jumla ya mifuko ya chakula 14 hapa nachanganya 7 (grower) na 7 (layers)
- 7 (grower) @ 46,000/ = 322,000/
- 7 (layers) @ 50,000/ = 350,000/
Chakula Layers
Wiki ya 21 hadi ya 28 mifuko 34 @ 50,000/ = 1,700,000/-
Assumption ni kuwa by wiki ya 28 kuku watakuwa wameshaanza kutaka na wanajilisha wenyewe.
Jumla yote ni 4,329,000/-
Hapa bado gharama za chanjo na madawa yatakayohitajika pamoja na posho ya mtu atakayekuwa anawahudumia kama si ww mwenyewe.