Nianze na kuku wa aina gani kwa mtaji wa Tshs 400000

Mr Confidential

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,484
2,327
Habari waungwana. Nawasilisha kama nilivyoulizwa

""Nina Tshs 400000 [laki nne].Ninataka nianze kufunga kuku japo sijui A wala B kuhusu ufugaji.

Je nianze na kuku wa aina gani kati ya wa kienyeji au broiler?

Naomba ushauri kwa kuzingatia gharama za uendeshaji, mtaji wa kuanzia, soko na mengine mengi ambayo siyafahamu.""
 
Mkuu Hongera kwa Jitihada kwanza. Pili kwa huo mtaji ili ku Break even au kupata faida itakuchukua muda mrefu sana.

Na pia kama ndo unategemea hiyo basi itakuwa shida sana.

Kwenye Biashara ya Kuku tusema Value Chain yake kuna mambo mengi sana.

1. Wauza madawa ya kuku
2. Wauza vifaa vya kuku kama Drinker na kadhalika.
3. Wanunuzi wa kati.
4. Wauza vifaranga
5.Wauza vyakula
6. Waongeza thamani na kadhalika.

So kwa mtaji huo unaweza sio lazima na wewe ufuge unaweza anzia pale ambapo wenzako wameisha.
Wenzako si wanaishia kwenye kufuga basi anzi pale. Au kwenyr mayai anzia pale wanapo ishia wao.

Unaweza ukawa unanunua mayai na ku resale hata ukipata faida sh 1000 kila trei bado ni kubwa sana make hukuwa nayo hiyo 1000.

Hii inaweza kuza mtaji zaidi. Kufuga ni Changamoto na ili upate faida unahitaji mtaji mkubwa sana

Ni hayo tu
 
Mkuu kama unataka kufanya biashara kwenye field hii ya kuku na kwa mtaji ulionao basi comment #2 kuna ushauri mzuri sana umetolewa maana pia wadau wamekupa maangalizo mbalimbali ktk coments zilizofatia baada ya hapo.

Lakini kama unataka kufuga kwa ajili tu ya fahari ya macho na mboga ya familia basi hiyo fedha inakutosha, maana utapata kuku wako wazuri tu wa kienyeji wachache na fedha ya chakula na dawa kidogo maisha yataenda na with time ukiwa makini utafurahi kuwaona kuku wako wanaruka na kukimbia kimbia huku na huku.
 
Labda kwa kuongezea inabidi mtaji was kiasi gani ili tuweze ingia katika ufugaji wa kibiashara
 
Habari waungwana. Nawasilisha kama nilivyoulizwa

""Nina Tshs 400000 [laki nne].Ninataka nianze kufunga kuku japo sijui A wala B kuhusu ufugaji.

Je nianze na kuku wa aina gani kati ya wa kienyeji au broiler?

Naomba ushauri kwa kuzingatia gharama za uendeshaji, mtaji wa kuanzia, soko na mengine mengi ambayo siyafahamu.""
Una banda au utawafugia tumboni
 
Mkuu acha mm niotee kuwa banda unalo, ngoja nikupe estimates kutokana na uzoefu wangu mdogo ktk kufanya hii shughuli (hands on experience) ingawa si ya muda mrefu sana.

Assume unanunua layers 250 ambao kama utafanikiwa kuwatunza vizuri tuseme kwa efficiency ya 90% mpaka wakati wa kutaga uwe na kuku hai na wanaotaga kati ya 200 na 220, uwe na uwezo wa kupata angalau trei 7 kwa siku.

Bei (Tsh) nitakazoziweka ni makisio lkn yanayokaribiana na ukweli.

Vifaranga 250@2,300/ = 575,000/-

Chakula Starter
Wiki ya 1 hadi ya 7 mifuko 4 (50kg) @58,000/ = 232,000/-

Chakula Grower
Wiki ya 8 hadi 11 mifuko 11 (50kg) @ 46,000/ = 506,000/-

Wiki ya 12 hadi ya ya 16 mifuko 14 @ 46,000/ = 644,000/

Wiki ya 17 hadi ya 20 jumla ya mifuko ya chakula 14 hapa nachanganya 7 (grower) na 7 (layers)
- 7 (grower) @ 46,000/ = 322,000/
- 7 (layers) @ 50,000/ = 350,000/

Chakula Layers
Wiki ya 21 hadi ya 28 mifuko 34 @ 50,000/ = 1,700,000/-

Assumption ni kuwa by wiki ya 28 kuku watakuwa wameshaanza kutaka na wanajilisha wenyewe.

Jumla yote ni 4,329,000/-

Hapa bado gharama za chanjo na madawa yatakayohitajika pamoja na posho ya mtu atakayekuwa anawahudumia kama si ww mwenyewe.
 
hii hesabu haijaka sawa mkuu

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Habari waungwana. Nawasilisha kama nilivyoulizwa

""Nina Tshs 400000 [laki nne].Ninataka nianze kufunga kuku japo sijui A wala B kuhusu ufugaji.

Je nianze na kuku wa aina gani kati ya wa kienyeji au broiler?

Naomba ushauri kwa kuzingatia gharama za uendeshaji, mtaji wa kuanzia, soko na mengine mengi ambayo siyafahamu.""

Huu uzi wako nimeuona tangu siku uliyopost ila sikuwa na muda wa kutoa mchango wangu, naomba leo nikujibu.
Iko hivi, kwanza ili kuamua uanze na kuku wa aina gani lazima uamue kufanya tathmini ya soko lako.
  1. Wateja unaowalenga ni wenye kuhitaji aina gani ya kuku au mayai?
  2. Eneo la kufugia likoje? Kama uko sehemu inayobana itabidi uwafugie ndani tu kwenye banda, hivyo ni busara ufuge chotara au wa kisasa (broilers au layers). Kama uko sehemu ya wazi kama vile shambani eneo kubwa nakushauri fuga kienyeji utafaidi sana. Maana utawaachia tu nje muda mwingi wanajitafutia chakula wakirudi utawaongezea kidogo,.
  3. Kuna gharama za banda kwa ajili ya usalama, sijui kama umejipangaje. Wafugaji wengi wanapenda kujenga mabanda ambayo ni gharama nafuu lakini inawagharimu sana baadaye kwa kuku kuibiwa. Mfano banda la mabanzi au bati na nyavu tuu. Kuna mtu alifuga kuku wakafikia 40 alafu wakachukuliwa wote kwa usiku mmoja. Ni vyema ukajenga banda imara lenye usalama wa 98% kama ilivyo nyumba yako ya kuishi.
  4. Ufugaji wa kuku ni progresive project ambayo inakua kwa spidi ya haraka. Kwa hiyo ni bora ukaanza kidogo sana. Kama ni kienyeji pure breed anza na hata kuku kumi tu au pungufu na jogoo mmoja. Nikupe uzoefu wangu. Nilianza na tetea mmoja na jogoo mmoja mwezi january mwaka huu. Mwezi wa 3 nikaongeza tetea 2, mwezi wa nne nikaongeza zingine 2, mwezi wa tano nikaongeza tena 2, na june nikaongeza 2. Sasa hivi vifaranga wa kwanza kabisa wameshakuwa wakubwa na wanatetea tayari kwa kuanza kutaga. Huku nina vifaranga vingine takriban 50 kutokana na hao tetea ambao idadi yao ni chini ya 10. Hao ninaosema ni vifaranga wengine mwezi ujao wataanza kutetea, wengine mwezi mwingine na kuendelea. Sasa hivi wengine wanne wanalalia, kwa maana nyingine baada ya wiki 2 zijazo idadi ya vifaranga itafikia 90. Bada ya muda mfupi ujao idadi itapanda na kufikia mara tatu au nne kwa muda mfupi sana. Ukuaji huu unatakiwa uendane na upanuzi wa miundo mbinu. Faida niliyo nayo nina eneo kubwa sana la kuwalishia kwa hiyo asubuhi wanatoka huko nje wanazurura na kuokota mchwa, wadudu wengine na pia majani. Wakirudi nawarushia mikono mikono miwili ya mahindi na mkono mmoja wa ngano au mtama. Baada ya hapo nawawekea hydroponics ambazo nimetengeneza mwenyewe kutokana na ngano. Then wanarudi tena kwenye mizunguko yao. Ni burudani tuu.
  5. Muhimu kuzingatia chanjo na daa za minyoo kwa wakati. Usidharau, hata kama una kuku 10 tuu, wape chanjo sahihi kwa wakati sahihi. Pia dawa ya minyoo itasaidia sana uzalishaji usishuke.
  6. Muombe Mungu akupiganie,
  7. Jitahidi kudhibiti wanyama hatarishi kama mwewe na vicheche (kama ufugaji wako ni huria).
Niishie hapo kwa leo
 
Ubarikiwe sana, Taifa linahitaji watu wa namna yako
 
Pia umetaja aina za kuku.

Kumbuka kuku wa Biashara ni wawili tu.
1. Brouler
2. Layers.

Hao ndo kuku kwa ajili ya biashara au kwa ajili ya kupata pesa

Kuku chotara na kuku wa kienyeji ni kwa ajili ya kuondoa umasikini tu.
Mkuu, usimpotoshe, laki nne, ni mtaji tosha akifanya hivi kwa vifaranga 100 aina ya Sasso:
1. Jenga kibanda cha tofali mbichi za udongo, ezeka kwa nyasi ( 3m x 4m). Sawa na 50,000/=
2. Nunua drinkers na feeders za kienyeji tuu ila ziwe safi sawa na 15,000/=.
3. Nunua vifaranga 100 kwa 130,000/=.
4. Nunua vyakula vyao special kwa 120,000/= na ongeza 45,000/= visivyo special uchanganye. Hiki kitatosha kulisha kwa wiki 10-12.
5. Dawa za chanjo na tiba 20,000/=
6. Dharura 20,000/=.
Jumla 400,000/=
Kuuza.
Uza wote baada ya miezi 2 na nusu hadi 3 bei ya chini ni 6,000/= @ .
Kumbuka 5% wanaweza kufa. Hivyo, 6,000/= * 95 = 570,000/=
Hapo faida ni kuanzia 170, 000/= kwa miezi 2-3 round ya 1. Round ya 2 faida itakuwa kubwa kwa vile hutajenga bands wala kununua drinkers na feeders.
Nimeweka wazi hapa kwa vile Watz wengi hawajui namna ya kuanzisha biashara ndogondogo ndani ya budget constraints ( ugumu wa mtaji au bajeti).
Karibuni kwa maoni.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom