Nianzaje kumwambia mke wangu mtarajiwa idadi ya watoto nilionao?

Hongera itakuwa una pesa sana wewe, watoto tisa kuwahudumia ipasavyo yataka uwe na pesa sana.
Kuzalisha unazalisha lakini kuzalisha zalisha tu kwa mademu dizaini ya mademu wa mwananyamala lazima wakusumbue mkuu
 
Unataka kusema hubebi wajibu??? Na unaona nisawa ww kutobeba wajibu. Angalia usije kuwa ni mzazi tu na si baba.
Shida ni kwamba wengi wanabeba majukumu yasiyo yao,
Mwanamke ukizaa nae haimaanishi kwamba umtunze na yeye pia,
Wewe jukumu lako ni mtoto.

Shida inakujaje kuna wanawake wengine ukizalisha basi atakufanya kitega uchumi wa kumuhudumia yeye pamoja na mtoto wako.

Hapo lazima upagawe
 
Hakuna siri chini ya juu mwambie ukweli kabla hujafunga nae ndoa aujue anaingia kwenye ndoa na Mwanaume wa aina gani.Mwambie hivi mtarajiwa mwenzio nilikuwa kicheche zipuu haifungi nina mbegu tisa nilipanda zimechipua uone atalipokea vipi.
Na vipi nikimpoteza mkuu?
 
Unajuaje kama wote hao ni watoto wako HUJABAMBIKIWA? Umefanya DNA?
 
Unataka kusema hubebi wajibu??? Na unaona nisawa ww kutobeba wajibu. Angalia usije kuwa ni mzazi tu na si baba.
Now unaona ni sawa ila ukishaoa hao mama zao watakupa shida utajuta.
Icho mi mwenyewe nakiona,
Wanawake wengi wa nje huanza usumbufu mhusika anapooa.

Lengo wakuharibie mkose wote
 
DNA yenyewe ya bongo wanatoa majibu kulingana na Factor.
Ukienda kwa mkemia, 90% utaambiwa Ni Wako kuepusha Lindi la watoto wa mitaani.

Hapa serikali naiunga mkono,

maana ata Kama ukiujua UKWELI, Ku-uishi huo UKWELI kwenye nafsi yako utakua Ni mtihani sana japokua najua wengi hawawezi kulikiri hili.
 
Back
Top Bottom