Niaminivyo Mimi: Tatizo la fisadi litakoma pale CCM itakapoondolewa madarakani

Nibozali

JF-Expert Member
Oct 15, 2016
572
1,055
Kwanza niweke wazi kuwa mimi ni CCM damudamu ingawa najitambua sana. Wale wanaoamini kuwa ujio wa Rais Magufuli ni suluhisho la kumaliza ufisadi Tanzania wanajidanganya. Rais Magufuli atajaribu kwa kiasi chake ila ufisadi utabaki palepale mathalani CCM bado iko madarakani.

Hivyo mkubali msikubali njia pekee ya kufuta ufisadi Tanzania ni kufuta CCM kwenye Ramani ya Tanzania.

Nawatakia mapambano mema.
 
Kwanza niweke wazi kuwa mimi ni ccm damudamu ingawa najitambua sana. Wale wanaoamini kuwa ujio Wa magufuli ni suluhisho LA kumaliza ufisadi Tanzania wanajidanganya. Magufuli Atajaribu kwa kiasi chake ila ufisadi utabaki palepale mathalani ccm bado iko madarakani

Hivyo mkubali msikubali njia pekee ya kufuta ufisadi Tanzania ni kufuta ccm kwenye Ramani ya Tanzania

Nawatakia mapambano mema

Na kuingia Lowasa na Sumaye?
 
CCM ndio chama pekee ambacho kinaweza tawala Tanganyika kuhusu Ufisadi nadhani unaona jinsi mafisadi wanavyokimbia CCM kwa sasa na kukimbilia kwenye kichaka cha ufipa kinondoni
 
Mi naona kama umelewa. Sasa hao mafisadi wako vyama mbadala wamejaa tele. Tena wale ene uzoefu wa ufisadi kedekede.

CCM ndiyo the cleanest political party in this land ever kwa sasa. Jaribu kufikiria upya sana. Maana hata hao majizi wasingehamia huko, bado kama ni watumishi hawatabadilika. Kwa sasa hakuna mbadala wa CCM kama si siasa za maji taka utakuwa umenielewa. Labda 2099 huko sifahamu.
 
CCM ndio chama pekee ambacho kinaweza tawala Tanganyika kuhusu Ufisadi nadhani unaona jinsi mafisadi wanavyokimbia CCM kwa sasa na kukimbilia kwenye kichaka cha ufipa kinondoni

Nani kautengeza huo ufisadi?

Tukienda nyumba za serikali wakati wa Mkapa

Aliyekuwa waziri wa ujenzi alishiriki kuhujumu majengo yetu nakuyauza kwa bei cheeee mengine kuhonga

Unamfaham?......mtaje

CCM yote mafisadi hakuna msafi
 
Wakati hizo nyumba za serikali zinauzwa waziri mkuu alikuwa nani??

(Sumaye)

Tumia akili kidogo

Anayetumbuliwa sio MAJALIWA NI MHONGO

Yaani waziri ndiye kawajibishwa sio waziri mkuu

Chukuwa kilichofanyika leo badala ya Majaliwa/Sumaye aliyeshindwa yaani fisadi ni waziri....je waziri gani alifisadi nyumba kama mhungo nishati?
 
Kwanza niweke wazi kuwa mimi ni ccm damudamu ingawa najitambua sana. Wale wanaoamini kuwa ujio Wa magufuli ni suluhisho LA kumaliza ufisadi Tanzania wanajidanganya. Magufuli Atajaribu kwa kiasi chake ila ufisadi utabaki palepale mathalani ccm bado iko madarakani

Hivyo mkubali msikubali njia pekee ya kufuta ufisadi Tanzania ni kufuta ccm kwenye Ramani ya Tanzania

Nawatakia mapambano mema
Kwa hiyo sisiemu inatoka alafu anakuja lowassa na wazee wa ngada ndo suluhisho eeh!
 
CCM ndio chama pekee ambacho kinaweza tawala Tanganyika kuhusu Ufisadi nadhani unaona jinsi mafisadi wanavyokimbia CCM kwa sasa na kukimbilia kwenye kichaka cha ufipa kinondoni

acha nyimbo Mkuu, wamekimbia tangy lini? Tatizo ccm mafisadi hawawezi kuisha hata wakimbie kiasi gani wengi wanachipukia kama Magugu shambani
 
Kwa hiyo sisiemu inatoka alafu anakuja lowassa na wazee wa ngada ndo suluhisho eeh!

Mimi napendekeza zao lolote LA ccm lisipewe nafasi kuongoza nchi hii. maana ndani ya ccm hakuna aliye msafi plus wale wote waliokimbia kutoka ccm
 
Nani kautengeza huo ufisadi?

Tukienda nyumba za serikali wakati wa Mkapa

Aliyekuwa waziri wa ujenzi alishiriki kuhujumu majengo yetu nakuyauza kwa bei cheeee mengine kuhonga

Unamfaham?......mtaje

CCM yote mafisadi hakuna msafi
Mkuu kuna vitu unatakiwa kujua Hivi kati ya mtakatifu na mtenda dhambi nani YESU ambae alisema alikuja kwa ajili yake?

watu wanasema mshindi ni yule anayemaliza mbio si yule aliyetangulia wakati wa kuanza mbio CCM walikuwa ni mafisadi kila mtu anajua lakini muelekeo wake unaonyesha wanakwenda wapi pia chadema walikuwa watakatifu lakini mwelekeo unaonyesha wanakwenda wapi ni bora sana kwa mwenye madambi kifo kumkutia mskitini au kanisani kuliko mtakatifu kifo kumkutia Guest house au kwenye madanguro akifanya madhambi
 
Mwanzoni nilifikiri CCM ikiondoka ufisadi utakwisha ila baada ya CHADEMA kumpokea Lowassa siamini tena hivyo.
 
Mafisadi papa yote na watuhumiwa maarufu wa sembe utawakuta kijiweni ufipani
Halafu eti tuyape utawala kweli?? yatasubiri xaanaa

sasa tuchukuwe wapi kiwandani au? maana tukiyachukuwa yakiwa kiwandani neo yanakuja na Makalu kama Hays ya Muhongo yanakata hadi nchi inatikisika
 
Back
Top Bottom