Niagize gari Japan au ninunue used hapa hapa Tanzania!?

JOXRICH

Member
Jan 7, 2012
78
30
Habari gani wadau wa JamiiForums!

Nina hoja kabambe ambayo nina uhakika wengi wetu inatuumiza kichwa hasa ukizingatia kupanda kwa kodi/ushuru wa kuingiza magari kutoka nje.

Kwa ambao mna ushauri au experience ya kutosha au maoni naombeni mtujuze kwa maswali hapo chini:

1. Je, niagize gari kutoka Japan kupeukana na purukushani za ununuaji hapa nchini pia kupata gari ambayo bado ipo imara ndani na nje?

2. Ninunue gari ambayo imeshatumika hapa nchini kwa mtu kuepukana na muda wa kusubiri gari toka Japan pia kupata kwa bei iliyo poa zaidi ya zile za kuagiza?

3. Je, kama nimeamua kununua gari hapa nchini nitumie njia na steps gani kuanzia kutafuta gari, kukagua, kuandikishana mkataba mpaka kulipia ili kuepuka kuuziwa gari bomu au hata kutapeliwa si mnajua hela ishakuwa ngumu

Thanks in advance..

Haya karibuni ndugu tujuzane na kutanuana ubongo.
 
Habari gani wadau wa jamii forums!
Nina hoja kabambe ambayo nina uhakika wengi wetu inatuumiza kichwa hasa ukizingatia kupanda kwa kodi/ushuru wa kuingiza magari kutoka nje.
Kwa ambao mna ushauri au experience ya kutosha au maoni naombeni mtujuze kwa maswali hapo chini:

1. Je niagize gari kutoka Japan kupeukana na purukushani za ununuaji hapa nchini pia kupata gari ambayo bado ipo imara ndani na nje?
2. Ninunue gari ambayo imeshatumika hapa nchini kwa mtu kuepukana na muda wa kusubiri gari toka Japan pia kupata kwa bei iliyo poa zaidi ya zile za kuagiza?
3. Je kama nimeamua kununua gari hapa nchini nitumie njia na steps gani kuanzia kutafuta gari, kukagua, kuandikishana mkataba mpaka kulipia ili kuepuka kuuziwa gari bomu au hata kutapeliwa si mnajua hela ishakuwa ngumu

Thanks in advance
Haya karibuni Ndugu tujuzane na kutanuana ubongo
Angalia mfuko wako, gari aina gani unataka? gharama za usafiri, ushuru kisha fanya maamuzi

Angalia mfuko wako, gari aina gani unataka? gharama za usafiri, ushuru na bandarini then fanya maamuzi.
 
Na mie nangojea sana majibu kwa hoja hii....lets say gari ni Toyoto Rav4 J (V) ya miaka ya 2000 back to 90's...au Subaru Forester. And let us say bajet yangu ikiwa ni 14M
 
Inatosha kuagiza Japan na chenji inabaki be forward mpango mzima
Halafu check calculator ya TRA jumlish port charges,agency fee,shipping line utaona ni kiasi gani cha chenji unayobaki nayo
 
Angalia mfuko wako, gari aina gani unataka? gharama za usafiri, ushuru kisha fanya maamuzi

Angalia mfuko wako, gari aina gani unataka? gharama za usafiri, ushuru na bandarini then fanya maamuzi.

Safi sana mkuu..... Nataka kuagiza gari aina ya Mark X 2006 bei sio mbaya sana CIF inachezea $3000-3500 then mambo ya tra ni kama 8M bandarini pamoja na agency fees kama 1M so ni parefu ukijumlisha na Insurance inaenda mpaka 16M-17M total. Ila kwa hapa nchini naweza pata kwa 12-15M
 
Kwa ambae ana uzoefu na kununua gari mkononi anaweza kutushirikisha kidogo zile taratibu za ununuaji kuanzia kukagua mpka malipo siunajua tanzania wajanja washakuwa wengi unaweza kuibiwa hela zote au ukauziwa gari ambalo ni la ovyo.

Hapa ofisini kuna watu wawili walinunua magari mikononi mwa watu lakini tunavoongea magari yao hayapo barabarani yote mawil yalipinduka mwaka juz lingine mwaka jana, moja lipo garage lingine halitengenezeki ashalisahau na kulisahau
 
Mfano Raum wadau?

Ingia beforward tafuta Raum unayotaka ukimaliza angalia bei yake CIF yake alafu ingia tra kuna calculators kuna vitu unaingiza kama mwaka wa hyo gari kutengenezwa, cc zake watakupa bei yake jumla kwa upande wa ushuru so utajumlisha ile CIF ya beforward pamoja na hii ya tra uliyopata alafu utaongeza na kama 1m hivi ya bandarini pamoja na ya agents wa clearing and forwarding....
Ila all in all Raum haiwezi fika 11M
 
hyo Raum mfano ya 2004 CIF ukienda vizur haizid $2000 ushuru wake ni kama 5.5M ukiongeza na ile 1m ya clearing and forwarding na bandarini unapata jumla ya 10.9M so bwana mkubwa andaaa kitu kama 11M
 
Na mie nangojea sana majibu kwa hoja hii....lets say gari ni Toyoto Rav4 J (V) ya miaka ya 2000 back to 90's...au Subaru Forester. And let us say bajet yangu ikiwa ni 14M
Milioni 14 huwezi kupata RAV4, 16M hapo uhakika ila 14 mkuu hapana labda kwa subaru ambapo sina uzoefu ila kwa RAV4 ni ngumu sana
 
Kwel mkuu RAV 4 zimekuwa hot cake kwasasa hata zile za 1998. Andaa zaidi ya 15M labda ununue kwa mtu humu nchini
 
Wakuu kuna mtu humu ndani anafaham showroom ambayo wana bei nzuri kwa upande wa Dar? Maana naona madalali wamekuwa wengi sana kila mtu anatangaza anauza gari kupatana.com ila ukipiga kumbe ni dalali bora kujihukumu Showroom. Kuna anayefahamu showroom nzuri yenye bei poa za magari!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Be forward. Ukiweza pia port of discharge iwe Mombasa. Ila sijui wewe uko mkoa gani.
 
Ukitumia bandari ya mobasa utachajiwa dola 600 zaidi kwa transit toka mombasa hadi holili au namanga kama upo tz
 
nina uzoefu wa kuagiza mwenyewe kutoka Japan na pia kununua hapa kwa show room. nakushauri nunua hapa kwa show room, bei itapungua kidogo. wauzaji wa magari wanajua wenyewe wanachofanya huko TRA. kwa ushuru wa Magufuli utalipa zaidi.
Nilitaka kuagiza Toyota Ractics (hizi ni gari mpya kidogo hivyo bei yake iko juu hata japan, kama IST), Jumla bei ilifika kwenye 13m mpaka kufika nyumbani, lakini show room hapa I paid 11.5m. Kazi kwako.
Rafiki yangu alinunua show room Toyota ISIS for 12m. Kama angeagiza Japan bei ingekua around 14m
 
Da Asia mchango wako ni wa muhimu sana. Samahani ulipoenda showroom ulibahatika kuona bei ya Toyota Mark X mana showroom nazozijua ni bei sana mpka 18M lakini ukiagiza ni kama 16-17M
 
Back
Top Bottom