Nia ya kuwekeza Mtwara

muhinda

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
348
234
wapendwa, mimi ni mtanzania ambaye nimeamua sitawaachia wawekezaji wa nje peke yao wafaidike na utajiri wa nchi yangu. ivi karibuni nilipata kuongea na rafiki yangu ambaye ni foreigner na amefika Mtwara, akanisisitizia sana kama nina pesa kidogo nielekee mtwara nianzishe biashara ya malazi yaani B&B. akanihakikishia kuwa watu wengi wanafika mtwara lakini wanakosa sehemu ya kuridhisha ya kulala, na kama wakipata basi bei ni kubwa mno.

sasa basi kwakuwa natambua JF ni kisima cha fikra na watu mbalimbali wenye mitazamo tofauti, naomba kama kuna mtu ana uzoefu na mji huu wa mtwara anisaidie kunipa info ambazo zinaweza nisaidia kwenye nia yangu.

Je ni kweli kuna uhaba wa malazi safi?
vipi upatikanaji wa ardhi? mtwara mjini au hata nje kidogo ya mji sio mbaya
au je, naweza pata nyumba iliyojengwa tayari nikaifanyia matengenezo kukidhi matakwa yangu bei zikoje?
maelezo mengine yeyote yanayoweza saidia yanakaribishwa
THE BIG SHOW najua wewe ni mdau wa mtwara, tafadhali kama una la kuchangia nitashukuru sana.

asanteni
 
Last edited by a moderator:
Nimezaliwa na kukua mtwara,
Huduma kama hizo zipo na bei zinatofautiana kulingana na hadhi ya sehem husika ...kikubwa ni kwamba,kutokana na kasi ya ongezeko la watu mtwara inasapelekea ionekane huduma hizo ni chache na zinahitajika kuongezwa pia kutokana na uchache huo pia unafanya wawekezaji wajivune na kupandisha bei kwasababu wanajua wahitaj ni wengi...

Kuhusu maeneo kwasasa kazi ipo? Kwa maeneo ya mjini kumvua mtu ni kati ya 10ml hadi 25ml kulingana na ukubwa wa eneo.

SIFA YA MTWARA.
Ni pazuri sana hakuna mfano...ki-biashara panalipa kupindukia pia ..
Karibu sana Mtwara (strategic city)
Japo kwasasa naishi dar es salaam ila naipenda mtwara.
 
Asante sana isack raphael kwa ufafanuzi.
je nikitaka kutoka nje kidogo ya mji let say umbali kama 10 minutes drive kwenda mjini nawezapata shamba kama la acre 5 ivi? Maana kwa biashara hii sidhani kama ni lazima nikae katikati ya mji cha muhimu ni kutoa huduma safi watu watafuata. Bei za mashamba zipi vipi?

vipi gharama za kulala hotel hapo Mtwara zinarange kwenye kiasi gani?
asante sana
 
Last edited by a moderator:
wapendwa, mimi ni mtanzania ambaye nimeamua sitawaachia wawekezaji wa nje peke yao wafaidike na utajiri wa nchi yangu. ivi karibuni nilipata kuongea na rafiki yangu ambaye ni foreigner na amefika Mtwara, akanisisitizia sana kama nina pesa kidogo nielekee mtwara nianzishe biashara ya malazi yaani B&B. akanihakikishia kuwa watu wengi wanafika mtwara lakini wanakosa sehemu ya kuridhisha ya kulala, na kama wakipata basi bei ni kubwa mno.

sasa basi kwakuwa natambua JF ni kisima cha fikra na watu mbalimbali wenye mitazamo tofauti, naomba kama kuna mtu ana uzoefu na mji huu wa mtwara anisaidie kunipa info ambazo zinaweza nisaidia kwenye nia yangu.

Je ni kweli kuna uhaba wa malazi safi?
vipi upatikanaji wa ardhi? mtwara mjini au hata nje kidogo ya mji sio mbaya
au je, naweza pata nyumba iliyojengwa tayari nikaifanyia matengenezo kukidhi matakwa yangu bei zikoje?
maelezo mengine yeyote yanayoweza saidia yanakaribishwa
THE BIG SHOW najua wewe ni mdau wa mtwara, tafadhali kama una la kuchangia nitashukuru sana.

asanteni
nakushauri ukitaka kuwekeza mtwara hakikisha unawekeza shangani East or west. Kwingine may be ni kule banadrini. Yakupasa ufahamu kuwa mtwara kuna vibaka Wengi sana. So kuna maeneo hata ujenge ghorofa hutoona mtu wa kupangisha.
 
nakushauri ukitaka kuwekeza mtwara hakikisha unawekeza shambani East or west. Kwingine may be ni kule banadrini. Yakupasa ufahamu kuwa mtwara kuna vibaka Wengi sana. So kuna maeneo hata ujenge ghorofa hutoona mtu wa kupangisha.

Nashukuru sana kwa angalizo, nitazingatia.
 
Asante sana isack raphael kwa ufafanuzi.
je nikitaka kutoka nje kidogo ya mji let say umbali kama 10 minutes drive kwenda mjini nawezapata shamba kama la acre 5 ivi? Maana kwa biashara hii sidhani kama ni lazima nikae katikati ya mji cha muhimu ni kutoa huduma safi watu watafuata. Bei za mashamba zipi vipi?

vipi gharama za kulala hotel hapo Mtwara zinarange kwenye kiasi gani?
asante sana

Nje kidogo unaweza kupata hata hapo mjini pia unaweza kupata muhimu ni kupata dalali wa kuaminika.
Pia naomba nirekebishe kauli ya mchangia mada hapo juu alivoongelea vibaka, usitishike kwahilo kwani naamini hata huko unakoishi sasa vibaka wapo muhimu ni kuwa makini pia kuwekeza si kwamba shangani ni bora zaidi hapana ..kwa sasa mji umepanuka sana hivyo popote utafanya biashara cha kuzingatia ni huduma mzuri za kuvutia,utafanikiwa.
Kuhusu hoteli bei zake ni kuanzia 45,000-60,000 per day
Mwisho nakuombea mafanikio mazur ya kuwekeza mtwara naamini utafurahia sana kuwekeza mtwara.
 
asante sana kwa ufafanuzi
 
Karibu Mtwara,kabla ya kufanya chochote kuhusu biashara za malazi,kunakitu nitakushauli muhimu sana,nyumbani ni Mtwara via Lindi,ila nimetembea mikoa mingi sana,nataka nikupe Case study pia
 
Hii post nimeweka hapa ili watu wengi zaidi wapate elimu. Ingekuwa vizuri kama uneweka info ulizonazo kwa f aida ya jamvi. Asante
 
mkuu in next 3yrs mtwara itakuwa paradiso na kutakuwa kuna mzunguko wa fedha sana na biashara zitaenda, ila kuna mdau mmoja kasema maeneo ya shangani yanafaa hapo mkuu kama unavijisenti fanya haraka sana utapiga hela kuna sehemu napajua watu wanalipa USD 100 per day halafu pakaWAIDA Sana.
 
Kwakweli nimepata moyo sana. Ila kuna watu humu wanabania info. Ningependa watu wafunguke zaidi humu humu. Asanteni
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom