amba.nkya
JF-Expert Member
- Jan 7, 2010
- 446
- 131
Nina nia ya dhati kabisa ya kuanzisha Tawi la chama cha CHADEMA ili kuimarisha chama from Grassroot level. Nimesukumwa kufanya hivyo kutokana na ukweli kuwa ninaishi eneo ambalo lina matawi mengi ya CCM lakini sijaona ofisi ya Tawi hata moja la CHADEMA. Nimejaribu kufanya utafiti kama wazo la kuanzisha tawi litakubalika nimebaini kuwa kuna wakazi waliotayari kuanzisha Tawi la CHADEMA kwenye eneo hilo na kujiunga na Chama hiki. Nimejaribu pia kutafuta ofisi ya muda nashukuru imepatikana sehemu nzuri karibu na barabara ambapo inatakiwa kulipia pango kwa mwaka.
WanaJF wenye nia njema na nchi hii naomba msaada wa mambo yafuatayo:
WanaJF wenye nia njema na nchi hii naomba msaada wa mambo yafuatayo:
- Namna ya kumpata Mbunge wetu John Mnyika maana Tawi hili litakuwa kwenye jimbo lake la Ubungo ili niweze kumuona na kuzungumza naye kuhusu nia ya kuanzisha Tawi na aweze kuja kuonana na wakazi wake ambao wana hamu ya kumuona Mbunge wao. Nimejaribu kumpigia Mh Mnyika kwenye simu yake ya kiganjani iliyoko kwenye mtandao wa CHADEMA huwa haipatikani.
- Utaratibu wa kupata fedha za kulipia pango la ofisi ya Tawi.