NIA TUNAYO NA NGUVU TUNAZO ZA KUPAMBANA NA UMASIKINI

wanawake live

Member
Apr 18, 2013
10
26
Msingi wa kufanikiwa katika jambo lolote ni kujiamini, lazima ujiamini wewe mwenye kabla mtu mwingine aja kuamini. Hii ni muhimu sana kwani hakuna atae weza kukuamini kama wewe mwenyewe hujiamini, hakuna mtu anaye weza kuwekeza kwako kama ujiamini. Ata kwenye BIASHARA zako kujiamini ni silaha kubwa sana itakayo ifanya biashara yako ilete manufaa.

Lazima uwe na mipango mkakati mizuri itakayo weza kukusaidia kufanikisha malengo yako. Ebu angalia WANAWAKE maarufu waliofanikiwa utaona kuwa walikuwa na mipango mizuri iliyosababisha wao wafikie mafanikio waliyo nayo.

Mafanikio hayaji pasipo kujiandaa, ni kama wanajeshi awawezi kwenda kupigana na maadui bila kufanya mazoezi ya kutosha. Mafanikio haya wezi kuja tu eti kwasababu wewe ni mrembo, lazima uyatafute mafanikio kisha mafanikio yatakufuata.

Nimejifunza kuwa waliofanikiwa zaidi ni wale ambao hawakuteteleka pindi walipokuwa wanakutana na changAmoto zilizokuwa zinawarudisha nyuma. Hivyo kabla hujaanza safari ya kutafuta mafanikio kaa ukijua kuwa kuna kushindwa pia na ujifunze jinsi ya kukabiliana na KUSHINDWA.

Kuna muda unaweza kutamani kuwa kama OPRAH WINFREY, MARY KAY AU COCO CHANEL lakini unaweza kushindwa kutambua ni atua ipi ya kwanza itakayo kufikisha kwenye mafanikio. Lazima utoke hapo ulipo uanzishe kitu kitakacho kuinua.


JOYCE.jpg


#WANAWAKELIVETZ tumeandaa program ya Kufundisha ujasiriamali, DARASA hili la UJASIRIAMALI litatolewa bure kabisa, mtaweza kujifunza
  • Ufugaji, kilimo na biashara.
  • Utengenezaji wa sabuni ya mche.
  • Utengenezaji wa sabuni ya maji ya kuogea, kufulia na chooni
  • UTENGENEZAJI WA BATIKI
DARASA hilo litatolewa na walimu wenye ujuzi wa kutengeneza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu. WOTE MNAKARIBISHA SANA.
DARASA ilo litafanyika Dar-es-salaam Tegeta, Nyuki {ukitokea sehemu yoyote ya Dar-es-salaam panda magari yanayoenda Tegeta, Nyuki kisha shuka mwisho wa gari. Harafu utapiga simu 0783137777 ili upewe maelekezo ya kufika.
KWA MAWASILIANO PIGA 0783137777
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom