Jana katika pita pita yangu nimejikuta nikiwa Mbagala. Kuangalia pembeni nikamuona Mabene Mbunge wa Geita -CCM. Nikatambulishwa na kumsalimu kwa jina Buzwagi . Akacheka akasema kijana haya ni mambo makubwa. Nikamuuliza kuna nini Buzwagi akasema ni shwari kabisa .Nikamkazia macho na maswali lukuki ndipo akasema , wao kama wabunge wanafungwa na Katiba ya CCM na Lowasa ndiyo maana wanashindwa kusimamia maslahi ya Taifa. Akasema ukienda kinyume Lowasa anakumaliza na akasema Mawaziri hawaelezei bajeti ila ndiyo wametumwa na JK kufukia mashimo. Akasema kama ni Bajeti sisi ndiyo wa kuiongelea. Nilimpiga maswali hadi akasema CCM kuna uongo wa hali ya juu na akasema hata ukiwa safi ukiingia CCM lazima ujifunze kusema uongo. Anakiri kwamba Wapinzani wanawapeleka puta ila anasema hawatakaa wakakubaliana na wapinzani hata kama jambo ni la ukweli maana haya si matakwa ya Lowasa na JK .
Ameshangaa Mawaziri kupita mikoani kwa jina la kuelezea bajeti lakini akasema najua Serikali imeshikwa pazito.Hapa ni kujibu tuhuma za Zitto na yeye akasema nimwache achape karata zake anangoja kula then wakati wa Bunge.
Nikamuuliza mbona hakupiga kelele juu ya Buzwagi akasema ni ngoma nzito wao wanaitwa na kuambiwa pitisheni. Hatupendi kijana lakini tunapewa amri . Ni bora kuna na kitu mbadala badala ya kugombea kwenye Chama .Ila wapinzani hatuwezi kukubaliana nao hata wakiwa sahihi .
Nikamwacha aendelee na karata zake .