RC Makonda atembelea kituo cha daladala Makumbusho. Ahimiza usafi, aruhusu bodaboda, Bajaji kuingia mjini

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,845
141,767
RC Makonda ametembelea kituo cha daladala Makumbusho na kuzungumza na wadau wa kituo hicho wakiwemo madereva, makondakta, wafanyabiashara na abiria wanaosubiri kusafiri.

Makonda ameahidi zoezi la kupuliza dawa mitaani litakuwa endelevu na kuwataka wananchi wawe na nidhamu kwenye swala zima la usafi.

Wakati huo huo, Paul Makonda leo April 1, 2020 ameruhusu Bajaji na Bodaboda zote kuingia katikati ya Jiji hilo ili kukabiliana na Adha ya Usafiri wanayokabiliwa wananchi katika kipindi hiki cha kupambana na Ugonjwa wa #Corona.

Makonda ameruhusu bodaboda na bajaji kuingia katikati ya Jiji

Makonda amewataka wenye nyumba za kupanga kupunguza kodi kwa 50%

Makonda amesema yeye hana mamlaka ya kuwaamuru Mwendo kasi hilo ni jukumu la waziri Jaffo

Wasiokuwa na shughuli za maana basi wabaki majumbani wasizurure hovyo.

Kama huna safari ya lazima kwenda mkoani basi usisafiri na kama uko mkoani usije Dar kama huna sababu za msingi.

advocate_jebra_20200401_1.jpg

Amesema Ndege moja ya Ethiopia inaingia kwa ajili ya Watanzania ambao wanahitaji kurudi nyumbani, sasa wakishaingia watafikia karantini kwa ajili ya uangalizi kwa hiyo mtu yeyote asiende Uwanja wa Ndege watapokelewa na ofisi ya Mkoa na kupelekwa Karantini kwa siku 14.

“Mungu akipenda tutakuwa na helkopta zitapita kumwaga dawa za kuua wadudu na gari pia zitapita kila sehemu nitatumia mamlaka yangu kufanya kazi". Amesema RC Makomda
 
Hili ni janga fidia ya nini?

Hata jengo la Ufipa mtalipia nusu kodi!
John, nimesema time and again kuwa huwa nakuhisi kama mtu wa busara huko lumumba kwenye wapuuzi watupu.

Naona ulikuwa umejirekebisha, sasa umerudi huko huko! sasa hii ni post gani kutoka kwa mtu kama wewe (ingawa sikujui, ila nahisi una "busara" from your posts....) ....
 
Back
Top Bottom