Nia Ipo, Sababu Zipo na Uwezo Upo kwa Slaa Kuwa Rais, Lakini.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nia Ipo, Sababu Zipo na Uwezo Upo kwa Slaa Kuwa Rais, Lakini....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlalahoi, Jul 22, 2010.

 1. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kila Mtanzania mwenye akili timamu,na mwenye uchungu wa dhati kwa nchi yetu anatambua kuwa miaka mingine mitano kwa JK ni mithili ya kuisukuma nchi yetu kwenye tanuru la vurugu na mchafuko.Yah,tunaambiwa Tanzania ni kisiwa cha amani na utulivu,lakini hata visiwa huwa vinakumbwa na vimbunga.Na hiki kinachotengenezwa na CCM sio natural disaster bali cha makusudi.

  Miongoni mwa mambo yaliyonisikitisha sana kuhusu JK na CCM yake ni dharau kwa Watanzania.Naita "dharau" kwa vile wao na sie tumekuwa tukiishi nchi moja katika miaka mitano inayoelekea ukingoni japo maisha yao na yetu yana tofauti kubwa.Kwa vile sote tumekuwa tukiishi pamoja ni dhahiri kuwa wanafahamu fika matarajio ya Watanzania wengi ni yapi na wao wamefanya nini katika ku-meet matarajio hayo.Na hata tukiweka kando matarajio yetu,JK na CCM yake walitoa mlolongo wa ahadi zilizoendana na matarajio yetu (which indicates walikuwa wanaelewa tunataka nini).Wanafahamu pia kuwa asilimia kubwa ya ahadi hizo zimebaki kuwa ahadi tu pasipo dalili yoyote ya utekelezaji.

  Basi angalau wangekuwa waungwana kwa kukiri mapungufu yao.Wangeweza kabisa kutumia "lugha ya kuombea kura" kwa kutuambia kuwa "wao ni binadamu kama binadamu wengine,na makosa ni sehemu ya ubinadamu".Au wangeweza pia kujaribu kutulainisha na kauli kama "kutenda kosa si kosa bali kurejea kosa".Lakini kwa vile wanatuona wapumbavu,all they have been saying ni mafanikio ya takwimu zisizoendana na hali halisi.Laiti mtu ambaye haijui Tanzania vyema akisikia "mafanikio ya awamu ya nne" anaweza kuhisi Tanzania iko hatua chache kuingia kwenye kundi la nchi zilizoendelea.JK anapigia debe mafanikio yake katika kila eneo.Hakuna mahala alipokosea,hakuna mapungufu katika utekelezaji wala,na hili ndio kubwa,tatizo la ufisadi ambalo kwa hakika ndio legacy ya serikali ya JK.

  Kwa vile wanatudharau,hawaoni umuhimu wa japo kutuomba samahani.Wanaamini wako sahihi,either kwa vile akili yao ni ndogo sana kutambua mabaya waliyotufanyia au kwa vile wanaamini kuwa Watanzania wameshazowea kupelekeshwa (sugu wa shida) na wanafurahia kuona nchi yao ikigeuzwa shamba la bibi.Ndio maana unaona majambazi wa Richmond wanapewa fursa kwenye TBC-taasisi inayoendeshwa kwa fedha za walipakodi-kuchokonoa kidonda ambacho hakijapona kwa kudai "hawajutii walivyotufanyizia".Huwezi kuwalaumu sana kwa vile mwenye mamlaka ya kuwaadhibu anaelekea kuwaunga mkono.Na kwa hakika,ujambazi huo wa Richmond kama ulivyo wa EPA,Kiwira,Meremeta,Tangold,nk ni sehemu muhimu ya utawala wa Jakaya Kikwete.Ni kwa vile tu vyombo vyetu vya habari "vinaumauma maneno" that JK hajawa fully implicated kwenye skandali hizo.

  Naamini kwa asilimia nyingi tu kuwa Watanzania wana NIA ya kuona nchi yao ikielekea mahala inapostahili,na wana SABABU ya kuondoa vikwazo vyote vinavyokwaza mafanikio katika safari hiyo,na wana UWEZO wa kufanikisha safari hiyo kwa njia ya KURA hapo Oktoba.

  Kikwazo kikubwa kwa Dokta Slaa kuwa Rais wetu hapo Oktoba ni HUJUMA.Lakini kabla ya kukizungumzia kikwazo hiki nigusie pia kile nachokiona kama kosa la kiufundi kwa Chadema.Muda uliobaki unaonekana kuwa mchache sana kufanikisha zoezi hili zito la kumwondoa Kikwete madarakani.Pamoja na kuheshimu taratibu za Chadema katika kupata mgombea wake,walipaswa kutambua uzito na ugumu wa jukumu katika kuking'oa chama cha kifisadi ambacho kimekuwa madarakani kwa takriban nusu karne.Sina hakika kama miezi miwili inatosha kukamilisha zoezi hilo japo wasiwasi huo haumaanishi kuwa haiwezekani.

  Kwenye suala la hujuma,hofu yangu kubwa ni hawa mashushushu ambao kwa hakika wako bize zaidi kuhakikisha CCM inatawala milele sio kwa vile huo ndio usalama wa taifa bali kwa sababu usalama wa o (mashushushu hao) na maswahiba wao mwafisadi unategemea sana uwepo wa CCM madarakani.Ni muhimu kwa Chadema kufahamu kuwa taasisi hii imekuwa kikwazo kikubwa sana kwa demokrasia katika nchi nyingi ambazo utawala wa sheria/utawala bora ni wa kinadharia zaidi ya vitendo.Pasipo kutambua adui huyu asiyeonekana,Chadema itaishia kushangaa kwanini Watanzania wengi walionekana kuwasapoti lakini mwisho wa siku JK na CCM yake "wanaibuka na ushindi wa kishindo".

  Pengine katika muda huu mchache uliosalia ni muhimu kwa Chadema kuhamasisha presence ya wasimamizi wa kimataifa kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki.Nasema hivyo kwa vile once "kura za CCM zisipotosha" mashushushu wataingia mtamboni kurejea uhuni uleule walomfanyia Seif Shariff huko Zenji.

  Ni katika hofu hiyo ya hujuma ndio maana baadhi yetu tumepatwa na mshtuko kusikia Mabere Marando ametangaza kujiunga na Chadema "sasa".Kwanini sasa?Because yeye na CCM wanafahamu kuwa Dkt Slaa ni serious contender,na anaweza kabisa kutoa upinzani wa dhati kwa JK.CCM bado wana kumbukumbu ya namna Dkt Slaa alivyokuwa mwiba mkali katika kipindi chote cha utawala wa JK.Wanatambua pia kuwa mwanasiasa huyo anaweza kujenga hoja vizuri na kueleweka kuliko huyo Mkwere anayeendekeza mipasho majukwaani.Kikubwa zaidi,wanafahamu kuwa Watanzania wengi wanaamini kinachosemwa na Dkt Slaa kwa vile kinaendana na ushahidi na hali halisi tofauti na takwimu za kupikwa za JK na CCM yake.

  Nimalizie kwa kuikumbusha Chadema na Dkt Slaa kuwa nia ipo,sababu zipo na uwezo upo kumg'oa JK hapo Oktoba,lakini ili hilo liwezekane ni muhimu kutambua "nguvu za giza" za viumbe wanaolipwa mamilioni ya fedha za walipakodi kushughulikia usalama wa taifa letu lakini raslimali hizo zinatumika kulinda ustawi wa mafisadi.Chadema ikimudu kudhibiti hujuma lukuki zinazoandaliwa dhidi yake basi tunaweza kufungua ukurasa mpya wa Tanzania yetu hapo Oktoba.Adui mkubwa kwa Dkt Slaa katika uchaguzi huu ni hao mashushushu hasa pale dalili zitakapoanza kuonyesha kuwa mgombea huyo wa Chadema sio "wa kawaida" kama katika chaguzi zilizotangulia.

  All the best Dkt Slaa,naamini utaruka vikwazo na kutufanya tutangaze "Uhuru wa pili" hapo Oktoba.
   
 2. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Yale yaleeee! CHADEMA tayari tumeshaanza kuja ni visingizio vya kushindwa hata kabla uchaguzi haujafika.

  Tunaongelea hujuma bila kwanza kujipa tathmini ya mtandao wa CHADEMA mikoani na vijijini kwenye wapiga kura wengi

  Tunaongelea hujuma bila kujadiri athari za mwonekano wa kidini na kikabila unaoisakama CHADEMA miaka nenda rudi

  Nadhani kuongelea hujuma ni rahisi, ni sababu ambayo kila mwenye mdomo na sauti anaweza kuitoa mara hasipokubaliana na matokeo. Lakini tukae tukijuwa kwamba mamilioni ya wapiga kura wako mikoani, wilayani na vijijini na sio hapa JF au kwa Michuzi. Vile vile tukae tukijuwa kwamba picha ya udini na ukabila ndani ya CHADEMA inadumaza jitihada za kuindoa CCM. Nearly for the same reason tumeona jinsi CUF inavyofifia Tz bara. Inachekesha kiasi cha kung'oa gego kwa chadema kulia HUJUMA hata kabla uchaguzi haujafika....kwa hili CHADEMA inahalalisha kushindwa!!! Mungu epushia mbali.
   
 3. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  CCM Wanafanya makosa kwa usahihi mkubwa ndio maana hawaombi samahani wala kuonyesha kuna sehemu wameteleza. Kwenye hotuba ya JK ulisikia aliseme
  Hapa nilicheka kwa masikitiko sana nikajua sasa watanzani tutarajie nini

  Kwa kifupi JK ataomba msamaha mwaka 2015 akiwa anaondoka tena ule msamaha wa ku generalise. kama alivyofanya mkapa.
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mlalahoi,
  Shida katika zoezi la kura si usimamizi. Tatizo linakuja katika kuhesabu kura. Hapo hata waangalizi wa kimataifa hawaruhusiwi kuingia na hapo ndipo CCM inajua kufanya rafu zake. Tukipata ufumbuzi katika zoezi la kuhesabu kura tutakuwa tumewapatia Watanzani haki za kura zao.
   
 5. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2010
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  posted more than once due to network problems. Soma post yangu inayofuata
   
 6. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2010
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Yote tisa, lakini hili la Mabere Marando kujiunga na Chadema ni kumi. Hakika Marando si mwanamageuzi bali purely usalama wa Taifa. Kuna wakati alikiri kutaka kummaliza Mrema katika mkutano wa NCCR kule Tanga; Kama si ujanja wa mlinzi kumpiga ngwara mrema, basi ilikuwa ni hatari.

  Katika kesi nadhani ya akina Rugangira kuaka kupindua serikali, yeye alikuwa shahidi upande wa serikali na inaaminika ndiye aliyempiga risasi mtuhumiwa mmojawapo pale fire dsm.

  Kwa kweli Chadema kuweni makini na mtu huyu; Chadema nawaamini, kama waliweza kuvuka la Guninita, hakika na hili la Marando watavuka. Mkakati mlioutumia kwa Guninita utumieni huo huo. Mwacheni awe mwanachama wa kawaida kwa miaka 5 bila madaraka yoyote!
   
 7. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160

  Sababu ya kumchagua tunayo, nia ya kumchagua tunayo na uwezo wa kumchagua tunao.
   
 8. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #8
  Jul 23, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Kamakabuzi,
  Asante kwa observation yako. Tahadhari ni nzuri sana. Lakini napenda kurudia katika siasa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu. Uingereza Conservatives hawakupanga kuingia kwenye Serikali ya Mseto na Lib Dem hadi baada ya matokeo ya uchaguzi. Wanaokuja wanaweza kuja na nia zao na hakuna anayeweza kujua hizo nia kikamilifu labda Mwenyezi Mungu anayeona nafsi za watu. Sisi tutatumia vigezo vya kawaida vya kibinadamu, pamoja na Tahadhari zote. Kabla Chadema haijapokea mtu, hasa anayejulikana kama Marando sitegemei kama watu wanatake for granted kuwa hatujajiridhisha kibinadamu na nia ya mtu huyo. Ninashauri sana katika kipindi hiki tusitafute mchawi, tuunganishe zaidi nguvu za wapambanaji wote, japo kwa tahadhari, na tutafute zaidi yanayotuunganisha kuliko yanayotenganisha. Tukishikamana na kuungana kwa yale yanayotuunganisha pamoja kwa hakika tutashinda. Nadharia ina umuhimu wake, lakini ikichukua asilimia 100 ya mijadala inatupotezea uwezekano wa kufanya yale ambayo jamii inatarajia kutoka kwetu, hasa wasomi ambao kimsing tunapaswa kuonyesha dira. Maoni yote tunayaheshimu na kuyapokea. Tahadhari zinazotolewa nazo zinafanyiwa kazi, lakini tungependa kwenda mbele. Wanabidii wameonyesha dira kwa vitendo, nadhani mijadala inayoenda kwenye hatua ndiyo itatusaidia. Sawa tuangalie tatizo ni kulinda kura, lakini mjadala bila hatua mahususi za kuchukua hazisaidii. Wengi tunajua kuwa hilo ni tatizo. Tufanye nini itatusaidia. Constructive Contribution ni msaada mkubwa. Nawashukuru wanaJamiiforum kwa ujumla kwa kuniunga na wale ambao dhahiri hawakuunga kwa sababu zao nao pia nawashukuru sana kwani maoni yao yamenisaidia kuwa focused zaidi. Michango yote ina maana, na hakuna mchango hata mmoja unatupwa na kudharauliwa, hata kama machoni mwa watu wengine utaonekana hauna maana, wa uchokozi na kadhalika. Mungu awabariki wote, Mungu ibariki Tanzania.
   
 9. MANI

  MANI Platinum Member

  #9
  Jul 23, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Kila la kheri na baraka mpiganaji wa kweli wa nchi hii.
   
 10. B

  Bwassa Member

  #10
  Jul 23, 2010
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 75
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 15
  Jamani,

  Hii hadithi ya Mlalahoi kuwa “Slaa anafaa kuwa Rais wetu…” haiwezi kupita bila ya kupingwa. Anazungumzia Slaa yupi? Ni huyu aliyeshindwa “Kumtumikia Mungu” na akajitumbukiza kwenye Siasa? Mnajua kwa nini alishindwa na kutoka huko kwenye “Utumishi wa Bwana?”. Si ndiye Slaa huyu huyu aliyefumaniwa na Mama watoto wake “red-handed” katika Nyumba ya Kulala Wageni mjini Dodoma, halafu siku ya pili akaita Waandishi wa Habari na kuilaumu CCM kuwa “imemfanyizia”? Ana uadilifu gani? Kama CCM inashinda kwa teknolojia ya kuiba kura na ndiyo maana Seif Sharif Hamad ameshindwa mara tatu Urais wa Zanzibar, vipi CCM, inashindwa kutumia teknolojia hiyo huko Pemba, ambako CUF inashinda Ubunge na Uwakilishi? Na kama CUF wanazilinda sana kura zao Pemba, kwa nini wanashindwa kulinda kura hizo Tanzania Bara na Unguja ambako CUF inalizwa kila uchaguzi? Mbona CUF Bara hawana hata kiti kimoja cha Mbunge wa Jimbo? Mtuletee “Post” za maana, siyo porojo hizi zinazochosha masikioni! Vinginevyo mtaigeuza hii Jamii Forum kutoka kuwa “The Home of Great Thinkers” kuwa Blogu ya “Cheap Propaganda” ya wakereketwa wa Chadema! Inaelekea Mlalahoi, unaielewa Tanzania, ukiwa London, Uingereza, kwa kupitia Blogu na Luninga! Rudi na nenda hadi vijijini, kwa kupitia Barabara za Lami zilizojengwa na kukamilishwa na Serikali ya Kikwete, angalau kutoka Mkoa hadi Mkoa! Umesahau sasa kuwa tulikuwa tunakwenda Mwanza kutoka Dar es Salaam kwa kupitia Nairobi, Kenya, kwa aibu kubwa? Tumepata maendeleo makubwa hayo nayo! Uchumi ulikuwa hasi (below-zero growth) hata unga madukani hakuna na watu wanapanga foleni ya kila kitu “Enzi za Nyerere”, je, kulikuwa na hao mnaowaita Mafisadi?

  Bwassa
   
 11. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Kimsingi hujuma zitakuwa za kila aina na bora awe makini kwa maana anakaribia kitoweo cha watu.
  Na tena watu wenyewe wana nguvu zote physical na hata za gizani pamoja na ujanja.
  Itabidi kila siku kufunga na kuomba kabla ya kazi
  Yaani 1. kuomba haki itendeke 2. wadanganyika wapungue, 3. wenye nia mbaya wasahau 4. Numba zi expire na 5. Njia za hujuma zijianike peupe na watenda hujuma watie aibu.

  Tukiombea hayo basi- Nia, sababu, uwezo, nguvu.... vitafanya maajabu this 2010 election.
   
 12. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Si hivyo tu inatakiwa kumuweka mbali na siri za chama pia:party:
   
 13. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #13
  Jul 23, 2010
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  Bwana BWASA naona sasa unaangalia mapungufu ya kibinadamu ambayo heri ya Slaa alimtumikia Mungu kwa kipindi,je huyo anayeshindana nae ana kashfa ngapi za uzinzi?Ndani ya JF ilisjaandikwa sana kuhusu trip zake za nje.
  Infedility ikitumika hapa africa hakuna kiongozi labda atoke Mbinguni.Tunachoangalia ni ukubwa wa makosa.Aliyezini na mwanamke mmoja na anayetumia dola millioni nne kwa safari moja ya mbili kwa safari moja ya nje wakati waja wazito wanakufa kwa kukosa huduma ni yupi bora?
   
 14. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Wewe Bwassa wewe. Mimi niko Tanzania hii hii nambie barabara inayokwendas vijijini ya lami aliyojenga Kikwete. Huna aibu hatakusema uongo? basi muogope Mungu jamani.
  Mi nakumbuka ni barabara moja tu ambayo amezindua ya kutoka Singida kwenda Arusha. Miradi mingine yote aliachiwa na Mkapa na kwa miaka mitano hajaimalizia badala yake anapandia hiyo kuonyesha mafanikio yake. Shame on you.

  Sasa mmeanza kueleza uongo kumpaka matope Rais wetu ajaye. Sikiliza tunafahamu mengi kuhusu Kikwete upande wa personal life. Lakini hilo silo mjadala wetu leo. Eleza maendeleo aliyoleta Kikwete. Acha bla bla zenu hapa. Nina uchungu sana na nyie.
   
 15. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wewe BWASA, kama unataka tuanze kuanika kashfa za ngono zinazomhusu huyo mgombea wenu mliyempitisha bila kupingwa, patakuwa hapatoshi hapa. Huwezi kumlinganisha Rais wetu mtarajiwa SLAA na JK. Ni watu wawili tofauti! Huyo JK ali-fluke tu akisaidiwa na msukumo wa mahela ya wizi kutoka kwa akina RA. Piga ua Watanzania hawatarudia makosa. Ngoja kampeni zianze uone moto utakaowaka.
   
 16. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,989
  Likes Received: 3,737
  Trophy Points: 280
  Kama muda ungekuwepo wa kutosha kabla ya October tungeweza kushinikiza matumizi ya special technology ambapo a unique agent (bio-marker) ingekuwa inscribed kwenye form za kupigia kura halafu an independent (preferably international) agent asambaze timu yake kufanya random sampling and testing kabla ya kura kuhesabiwa. Am sure ingeweza kufunua "pandora box" kiaina!!
  Most importantly, it would have posed a deterrent effect against wizi wa kura.
   
 17. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #17
  Jul 24, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Bwassa una akili ya kitoto, Dr Slaa anahitajika awe rais wetu maana nchi hii imekuwa haina rais ndani ya miaka miatano iliyopita. JK ana kashfa nyingi kuliko wengine, usiwaudhi watu wakaamua kuanika kila kitu hadharani. Ni akili ya mwana ccm fisadi tu isiyoweza kutambua mchango wa Dr Slaa kwa TZ. Halafu unakuja na upuuzi kuwa jk kajenga barabara, wapi kafanya, anapiga photocopi mafanikio ya Mkapa.

  Dr Slaa Rais anahitajika fot Tanzania
   
Loading...