Ni zipi sifa za mtu kuchaguliwa kuwa Best Student Chuo Kikuu?

Jul 25, 2019
8
6
Habari watanzania, leo nimekuja na hili swali, maana limenichanganya kidogo. Nina mdogo wangu amepata 4.7/5.0 hapo UDBS-UDSM na yeye ndo alikuwa na GPA kubwa kushinda wote hapo cha ajabu hakutangazwa kama BEST STUDENT.

Wadau mliopo kwenye ACADEMIC FIELD naomba mniambie ni vigezo vipi huzingatiwa kumpata BEST STUDENT chuo kikuu,kwa mimi ninavyojua ni GPA iwe kali kushinda wenzako wote.

Ahsanteni
 
Swali zuri sana wanaweza wote wakawa na GPA moja ya juu sawa let say 4.9 sasa ikifikia hapo GPA zinaweza kuwa sawa lakini bado wakatofautiana kwa jumla ya marks.Nikupe mfano mdogo 80 hadi 100 zote zinaweza kuitwa daraja A lakini huyu aliyepata 81 na aliyepata 95 wote wako daraja moja la A na GPA zikawa sawa lakini marks zitakuwa tofauti
 
Chuo kikuu Udsm ni kikubwa mno na college/ School zaidi ya kumi yeye amajuaje kama yeye ndo wa kwanza?

Binafsi sioni pia kama kuna ulazima wa kutangazwa, Chuo kimeisha,ni wakati wa kuja kuprove iyo GPA yake kwa ground.

uzuri wa kwa ground hauna haja kupambana kutangazwa, akiweza kuiprove tutamjua. exceptional people are very few.
 
je iyo 4.7 ni kwa wastani wa miaka yote mitatu/minne?

habari chini ya kapeti, inabidi iwe above or equal 4.8
 
Habari watanzania,leo nimekuja na hili swali,maana limenichanganya kidogo.Nina mdogo wangu amepata 4.7/5.0 hapo UDBS-UDSM na yeye ndo alikuwa na GPA kubwa kushinda wote hapo cha ajabu hakutangazwa kama BEST STUDENT.Wadau mliopo kwenye ACADEMIC FIELD naomba mniambie ni vigezo vipi huzingatiwa kumpata BEST STUDENT chuo kikuu,kwa mimi ninavyojua ni GPA iwe kali kushinda wenzako wote.Ahsanteni

Kimsingi kigezo kikuu cha mwanafunzi bora kitaaluma ni GPA.
Endapo kutatokea mfanano wa GPA basi wanaangalia ''raw marks'' ambapo mwenye nyingi ndiye anapewa ushindi.
Kumbuka kwamba A ya 72 na 95 zina uzito sawa kwenye GPA lakini kwenye ''raw marks'' mwenye A ya 95 anahesabika kwamba ni mkali kuliko yule wa 72.

Maswali yangu kwako:
1. Umejuaje kwamba mdogo wako alikua na GPA kubwa kuliko wanafunzi wengine waliohitimu pamoja nae mwaka huu hapo UDBS ?

2. Mwanafunzi bora wa mwaka huu wa duru ya 4 (cluster 4) inayomuisha UDBS, CoHU, CoSS, SoED, IKS, IDS, UDSoL, SJMC aitwaye Kauthar S. Salum (kutoka UDBS) alipata GPA ya ngapi ?

ahsante.
 
Habari watanzania,leo nimekuja na hili swali,maana limenichanganya kidogo.Nina mdogo wangu amepata 4.7/5.0 hapo UDBS-UDSM na yeye ndo alikuwa na GPA kubwa kushinda wote hapo cha ajabu hakutangazwa kama BEST STUDENT.Wadau mliopo kwenye ACADEMIC FIELD naomba mniambie ni vigezo vipi huzingatiwa kumpata BEST STUDENT chuo kikuu,kwa mimi ninavyojua ni GPA iwe kali kushinda wenzako wote.Ahsanteni
Unajuaje Kama hakuna mwingine main campus, DUCE na MUCE ?
 
Swali zuri sana wanaweza wote wakawa na GPA moja ya juu sawa let say 4.9 sasa ikifikia hapo GPA zinaweza kuwa sawa lakini bado wakatofautiana kwa jumla ya marks.Nikupe mfano mdogo 80 hadi 100 zote zinaweza kuitwa daraja A lakini huyu aliyepata 81 na aliyepata 95 wote wako daraja moja la A na GPA zikawa sawa lakini marks zitakuwa tofauti
Hili ni moja but lingine la maana zaidi wanaangalia average of accumulated figures..Inawezekana mtu kapata 4.7 leo ila miaka ya nyuma alipata 3.8 na 3.9! Wakati mpinzani kapata 4.5, 4.7 & 4.8 respectively.

Utaona kabisa mpinzani kayumba mwaka wa mwisho ila average yake iko juu!
 
Una uhakika gani yeye ndo mwenye kubwa?

yani kusiwepo na 4.8 kweli UDSM
Hilo nalo neno.

Japokua best student huwa hawi mmoja, kila duru (cluster) inatoa best student wake.

Duru ya tatu iliyojumuisha CoAF, CoNAS, CoET na CoICT best student wake alikua na GPA ya 4.8 na alikua ni mhitimu wa ''electrical engineering'' ya pale CoET, anaitwa Daud ...

Mshindi wa ''colleges'' zingine anakua ni best performing student among them (not necessarily awe na GPA ya 4.8)
 
Hili ni moja but lingine la maana zaidi wanaangalia average of accumulated figures..Inawezekana mtu kapata 4.7 leo ila miaka ya nyuma alipata 3.8 na 3.9! Wakati mpinzani kapata 4.5, 4.7 & 4.8 respectively.

Utaona kabisa mpinzani kayumba mwaka wa mwisho ila average yake iko juu!
Mkuu, mwanafunzi aliyehitimisha masomo yake, miaka mitatu au minne n.k GPA yake inayozungumzwa huwa ni ''cumulative GPA'' (GPA jumuishi) inayojumuisha matokeo ya miaka yote.

Kwahiyo anayosema mdogo wake ana 4.7 anamaanisha ni overall GPA.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom