Ni zipi Haki za Abiria? Basi la Super Feo limekalisha abiria hapa Chalinze tangu asubuhi, hakuna msaada wa Mamlaka au Mmiliki

Trebla84

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
459
1,000
Msaada kwa wenye uelewa wa jambo hili.

Jamaa yangu amepanda gari la Super Feo kutoka Dar kuenda Songea asubuh, kufika Chalinze eneo la mlimani ajari ikatokea kati ya basi na boda.

Wakaja polisi gari ikageuza kurudi kituoni Chalinze ilikuwa ni saa tatu na dakika zake.

Tokea saa tatu mpaka navyoandika thread saa nane bado wapo tu abiria wamekaa hapa kituoni.

Hatupewi ushirikiano na polisi wala wamiliki wa gari.

Wanahitaji msaada mana kama abiria hawana haki.

Bosi wa Super Feo pamoja na polisi wanawanyanyasa abiria.

Tuwasaidie hawa watu bado wapo Chalinze na hawana dalili ya kutoka.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
10,949
2,000
Kisheria, ajali inamhusu dereva labda kama gari limeathirika kutokuweza kuendelea na safari.

Dereva pia ana haki ya kupewa dhamana.

Wa kulaumiwa kwenye dhahama hilo kwa mujibu wa maelezo yako, ni polisi ambao pengine wako ki kubrashi viatu zaidi.
 

Trebla84

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
459
1,000
Kisheria, ajali inamhusu dereva labda kama gari limeathirika kutokuweza kuendelea na safari.

Dereva pia ana haki ya kupewa dhamana.

Wa kulaumiwa kwenye dhahama hilo kwa mujibu wa maelezo yako, ni polisi ambao pengine wako ki kubrashi viatu zaidi.
Gari halijahathirika lipo sawa kuendelea na safari wao walikuwa wanamtaka dereva aliyekimbia lakini dereva nae alishafika lakini hakuna kinachoendelea.

Abiria wamekaa tu pale kama mizigo.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
10,949
2,000
Gari halijahathirika lipo sawa kuendelea na safari wao walikuwa wanamtaka dereva aliyekimbia lakini dereva nae alishafika lakini hakuna kinachoendelea.
Abiria wamekaa tu pale kama mizigo.
Pana namba za wakuu wa polisi wa mikoa zilikuwamo humu jamvini. Maeneo hayo ni Pwani. RPC Pwani ana husika.

Hata hivyo katika kila kituo pana namba wazi wazi za OCS, OCD, RTO, RPC na hata IGP.

Haki haiombwi. Muda wenu wa kusimama na kuidai haki yenu kistaarabu na kwa kuanzia kwa kupitia maongezi na ikibidi kwa simu ni sasa.

Msiipoteze fursa hii, yote mema yako upande wenu.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
10,949
2,000
Mi ningeshuka nitafute usafiri

Ajali inawahusu nini abiria. Latra na polisi wajibu wao ni kusumbua abiria?

Kwani OCS, OCD, RTO na RPC wanasema je kuhusiana na hii kadhia ya kubumba bumba na waliopaswa kuwa walinda amani?

Acha ukondoo simamia haki zako.
 

smarte_r

JF-Expert Member
Nov 8, 2013
2,165
2,000
Msaada kwa wenye uelewa wa jambo hili.

Jamaa yangu amepanda gari la Super Feo kutoka Dar kuenda Songea.....


....bado wapo tu abiria wamekaa hapa kituoni.

....Hatupewi ushirikiano na polisi wala wamiliki wa gari.
.

mbona unajichanganya sana ndg?. si useme tu ni wewe ni mmoja ya abiria badala ya kumuhusisha jamaa yako. acha uoga.

anyway pole sana kwa kadhia hiyo. taarifa itakuwa tayari imeshafika kwa mamlaka husika kwa hatua zaidi.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
10,949
2,000

Hata kama ni yeye. Si yeye, wala yeyote anayestahili uonevu wa wazi kama huo kwa jina la JMT.

Au nawe ndiyo polisi wenyewe mnaowatesa abiria hao wasioweza kuzisimamia haki zao?

Acheni dhuluma uchwara hizo.
 

iam Lucha

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
2,409
2,000
Kama gari imeumia bas mmiliki atawajibika kuwatafutia gar lingine pamoja na Dereva mwngne muendelee na safari ila Kama gari haijaharibika bas mmiliki atawatafutia dereva mwingine
Yule alisababisha ajali hawez kuachiwa kma hiyo ajali ni kubwa kwa usalama wake na wenu.
Ukishapanda gar likapata ajali kma kugonga mtu kma gari halina dereva wa akiba ni lazma mtachelewa tu
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
10,949
2,000
Dhuluma zisizo uchwara si ndio hatari zaidi?

Dhuluma uchwara ni pale dhulumati ana dhulumu hali hana ubavu wa mpambano hadi mwisho. Huyu anapigika vizuri tu.

Wengi wa namna hii wanatumia mgongo tu wa mamlaka kujaribu kujinufaisha. Ukikomaa ana mwaga mbio:


Hawa makelele tu ya hao, hao, .., hao kama vibaka vile yanatosha sana kuwamudu. Hawa ni wa kuwanyorosha asubuhi asubuhi kama hivi tunavyo fanya. Tulipo tunasubiria mrejesho.

Wenye dhuluma konki wa nini jombi?

Si walisema ni kheri ya nusu shari?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom