Ni zip Tofauti kati ya VRN na TIN,je kunafaida gani ya kuwa na VRN? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni zip Tofauti kati ya VRN na TIN,je kunafaida gani ya kuwa na VRN?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ruhazwe JR, Sep 22, 2012.

 1. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wasalamu,
  hizi ni terminology za TRA.nafahahamu TIN lakin VRN sifahamu wala sijui faida za kuwa nayo wala hasara za kutokua nayo.naomba kupewa shule jaman!
   
 2. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,105
  Likes Received: 7,363
  Trophy Points: 280
  VRN-VAT Registration Number,
  Hii anakua nayo yule alieandikishwa kulipa VAT tu, jua kua sio kila business person analipa VAT.

  TIN-Taxpayer Identification Number.
  Hii anakua nayo mlipakodi yoyote hata kama halipi VAT. Sasa basi hata yule pale juu kwakua VAT ni kodi so anatakiwa pia kua na hii.

  Note;
  Kwenye neno yoyote hapo juu, naomba mfanyakazi usimuweke ingawa analipa kodi.
  Kwanini? SIJUI!!!!
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  VAT nakumbuka inachajiwa kwa wafanyabiashara wenye mapato/mtaji ya zaidi ya mil20(Civics ya form One) kama sijakosea(mwanzo walikua wanatoza 20% now ni 18%)
   
 4. UBISHI

  UBISHI Member

  #4
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mapato yanayozidi 40,000,000 kwa mwaka.......VAT 18%
   
 5. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Shark kwa hiyo,kama unanzisha kampuni yako si lazima uwe nayo na hasa kama mapato yako ni chini?na kama ukiwanayo nini faida za kuwa nayo
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. wehoodie

  wehoodie JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 783
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 80
  TIN - hii ni muhimu kwa kila mlipa kodi kwa kuwa ni reference number yako kwa TRA. Hata ukitafuta leseni/au ku-import gari unapaswa kuwa na TIN ili kodi unayolipa iwe na reference. hii kila mlipa kodi anayo na pia hutolewa bure na TRA.

  VRN ni kwa walipakodi wanaojihusisha na biashara inayohusisha kodi ya VAT. Ikiwa unafanya biashara yenye kodi ya VAT unapata/tarajia kupata mapato ya tzs 40m kwa mwaka au zaidi unapaswa kujisajili na VAT ili upate VAT regustration number.

  Faida:


  • Ukiwa kama mfanyabiasha unayejihusisha na biashara yenye uwepo wa kodi ya VAT, basi ni muhimu kwa kuwa utakuwa unatii sheria hivyo kupeuka faini na matatizo na idara husika;


  • Unapokuwa na VRN unaweza ku-claim VAT ulizolipa katika manunuzi yako na hivyo hiyo VAT kuwa sio gharama yako bali ya mtumiaji wa mwisho;


  • Kama biashara yako inahusisha kampuni kubwa, kampuni hizi hupendelea kushiriki biashara na watu wenye VRN kwakuwa wataweza kurejesha kiasi cha VAT walichotozwa kwenye hawala zao na pia wanatii sheria kwa kujishughulisha na mtu ambae ni mtii sheria pia; na
  • Unasaidia nchi kukusanya kodi na kuwapa kwa VAT unazotoza katika biashara yako.

  Hasara/Challenges:


  • Gharama kubwa za kuweka rekodi zako za kibiashara katika mfumo unaokubalika na TRA ikiwa ni pamoja na kuwa na accounting department etc (compliance burden); na
  • Gharama za kuandaa na kupeleka ripoti za VAT kila mwezi katika TRA na kulipa VAT ulizokusanya.

  NB: Ikiwa umetimiza vigezo vya kuwa na VRN inapswa kuipata maramoja, kinyume na hapo ni kosa kisheria linalopelekea faini.
   
 7. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  wehoodie tunashukuru sana kwa kuja na maelezf mazur ya kina,natumai mleta mada atakua amepata majibu,labd nikuulize swali la nyongeza,mfano nimesajil kikampuni changu cha kazi mchanganyiko kulingana na memart itakavyokua inaeleza na nina TIN tayari naanza na kabiashara kamtaji wa ml3 kastationary ka kawaida,Lakini marengo yangu ni kupanua mtaji,na kuweza kuwekeza ktk majumba,mahotel na ukandarasi,je ni lin ntajitambua kuwa kwa sasa nimekua natakiwa kujisajir na VRN?nauliza hivyo kwakua naweza kuwa na mtaji Umekuwa had ml20 naenda kuomba tenda za mli 50 au 30 Je nili ntatakiwa kujijua kua nimequlify kwa na VRN?Je nikisajilir VRN wakati mtaji wangu ni ml3 Kuna tatizo?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Wakati tunasoma ilikuwa mil20 na 20% kumbe now ni 40mil na 18%
   
 9. wehoodie

  wehoodie JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 783
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 80
  Mkuu Ruhazwe, unatakiwa kujisajili pale ambapo umepata aua unatarajia kupata pato (sales/revenue/turnover) ya TZS 4Om kwa kipindi cha miezi 12 mfulullizo (mwaka 1) au tzs 10 kwa kipindi cha miezi mitatu. Hivyo pale ambapo umepata hiyo tenda ambayo unajua malipo yake yanazidi hizo benchmark unatakiwa katika kipindi cha siku 30 ujiandikishe na VRN.

  VRN inaangalia mapato na sio mtaji, sijui kama kuna uhusiano wa karibu kati ya pato na mtaji.
   
 10. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu wehoodie nimekupata vilivyo.ahsante sana kwa sasa sina swali
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #11
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,105
  Likes Received: 7,363
  Trophy Points: 280
  Wazungumzia ipi sasa Madabhali Jnr ??
  TIN ni lazima uwe nayo so long as unafanya biashara.

  But VRN ni kama mauzo yako (sio faida) yanafikia 40Million kwa mwaka, au kuna miezi mitatu ambayo hua yanafikiaga 10Million.
   
Loading...