Ni Zaidi Ya Sura

BABA JUICE

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
426
52
Waigizaji wetu wanafikiri ukiwa good looking inatosha kuwa nyota wa filamu.....rewind...ni zaidi ya sura na umbo zuri...talent....na waliosomia tasnia hii..sio unakurupuka tu unataka kuigiza siwasemi kwa majina mnajijua.....karibuni vilamu za xxxxx zitaanza huko tunaitaji sura yako nzuri na muonekano wako....huku waachie wanao jua wanafanya nini....mtazamo
 
Mtu akishindwa u-miss basi anaenda kuigiza. Mtu akishindwa Bongo Star Search anaenda kuigiza. Mtu akijitazama kwenye kioo akajiona ana mwonekano mzuri anaenda kuigiza. Hili ni tatizo kweli.
 
Waigizaji wetu wanafikiri ukiwa good looking inatosha kuwa nyota wa filamu.....rewind...ni zaidi ya sura na umbo zuri...talent....na waliosomia tasnia hii..sio unakurupuka tu unataka kuigiza siwasemi kwa majina mnajijua.....karibuni vilamu za xxxxx zitaanza huko tunaitaji sura yako nzuri na muonekano wako....huku waachie wanao jua wanafanya nini....mtazamo
Wanauza sura hasa ma boyf,lengo wapate usamaria kwa mi mama sukari,ili wakatanue na madem wanaojiita ma supa star
 
Wanatafuta maisha, maisha huyapati bila kazi, na kazi huipati bila elimu na ujuzi.
sasa filamu na muziki ndiko unaweza kwenda kufanya kazi hata bila elimu na ukapata maisha walau ya hali ya kawaida na ikichanganya walau ufike level ya kina Kanumba na Lady JD.

Ni vema tukiwapa mawazo ya kusaidia ili wakiyapata yawasaidie waweze kuifanya hiyo kazi waliyoamua kufanya kwa ufanisi na kutufurahisha zaidi badala ya kuwa katisha tamaa
 
Sanaa ya siku hizi ni kuuza sura , wanaume wanajipodoa, wanawake wanajipodoa , hakuna tofauti kati yao. Waigizaji hawako realistic, Mtu anaigiza umaskini lakini kajipodoa na kichwani katengeneza nywele za sh.50,000! ridiculous! Mtu kanunua pamba yake ya kichina kkoo anaona pa kuionyeshea ni kwenye filamu. Sina uhakika watu wa make up kazi yao ni nini lakini nadhani ni kutengeneza muonekano wa muigizaji ili aweze kuuvaa uhusika ipasavyo. Waigizaji kama kina waridi, bishanga, monalisa hao ndio wasanii wa kweli. Akilalamika utafikiri kweli, akilia utafikiri kweli, lakini siku hizi kazi kuuza sura, magari ya kifahari, na majumba ya watu! Kuna wengine wanadiriki kusema" MIMI UKINICHEZESHA HOUSE GIRL SICHEZI"!!!!!!!:eek: Hhahahahahaha! Puuu! Mi nilishaachaga kuangalia huu upuuzi.
 
Kuna wengine wanadiriki kusema" MIMI UKINICHEZESHA HOUSE GIRL SICHEZI"!!!!!!!:.
Hakuna muigizaji humo... huyo anarekodiwa tu...
Anadhani wanofanikiwa katika hiyo sanaa ni wale wanoigiza wako matawi ya juu pekee...
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom