Ni yapi maziwa bora kwa mwanangu, Maziwa ya ng'ombe tumchemshie au Infant formula ?

Liobite

Senior Member
Sep 10, 2013
125
35
Mtoto wangu ana umri wa miezi kumi na moja mpaka tarehe 25 mwezi huu wa 11, 2018 atakuwa na umri wa mwaka mmoja kamili. Kwa Kipindi chote toka amezaliwa mpaka miezi 6 alikuwa ananyonya tu. Toka miezi sita mpaka sasa tulikuwa tumpa uji na vyakula vingine.

Sasa wiki hii mama yake anaanza masomo,hivyo tunatarajia kumwachisha Mtoto kunyonya.

Sasa ninaomba ushauri wenu ni yapi maziwa bora kwa mwanangu kwa umri huu kati ya Maziwa ya ng'ombe tumchemshie au Infant formula (Lactogen)?.

Na kwa hayo yatakayofaa inatakiwa apewe kwa kiwango gani?.

Muhimu: Leo ni Siku ya pili nilikuwa namjaribia kumpa maziwa ya ng'ombe nimeona anakunywa bila shida anapohitaji.

Asanteni endapo mutaonesha ushirikiano kwa hili.View attachment 923329View attachment 923331
 
Mpe tu ya Ng’ombe haina shida, ili mradi unapochukua wawe waaminifu siku ambazo wanamchoma sindano Ng’ombe usipewe maziwa.
 
Back
Top Bottom