Ni yapi mazingira ya Serikali ya Mseto?

Mazingira hayo hayapo bayana Tanzania ila ikitokea wagombea urais wakafungana kura mfano 50%/50% inawezekana ikaundwa serikali ya mseto. Pia ikitokea Lissu akashinda 60% lakini akawa na wabunge wachache mno kama vile 90 tu kati ya wabunge 254 ni mazingira ya mseto.

Au ikitokea kura zimekaribiana mfano 52% kwa 48% na kukawa na utata mkubwa katika uhalisia wa matokeo kwa namna ya kutishia amani na mshikamano wa nchi, hayo nayo ni mazingira ya kuunda serikali ya mseto ili kuleta muafaka na amani. Pengine hili la mwisho ndilo linanyemelea.
 
Mazingira hayo hayapo bayana Tanzania ila ikitokea wagombea urais wakafungana kura mfano 50%/50% inawezekana ikaundwa serikali ya mseto. Pia ikitokea Lissu akashinda 60% lakini akawa na wabunge wachache mno kama vile 90 tu kati ya wabunge 254 ni mazingira ya mseto.
Hivi ni tume ndy inayoamua au mahakama?
 
Magufuli ni mental case.Sisi chadema hatuwezi kuunda serekali ya mseto na mtu kama yule.Serekali ya chadema haitakuwa ya mseto.
 
Wakuu Salaam:

Ni yapi mazingira ya Serikali ya Mseto?

Nimeuliza makusudi tu nataka niyajue!

Nimemaliza.
Hahahaàaaaaaaa tulijua upigaji kura ukikaribia mtaanza ndoto za alinacha.Subirini 2025 mjaribu bahati wachochexi nyie.Nani awashikishe magaidi kwenye serikali
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Wakuu Salaam:

Ni yapi mazingira ya Serikali ya Mseto?

Nimeuliza makusudi tu nataka niyajue!

Nimemaliza.
Kwanza mseto na nani ? Unakuwa na mseto na watu wenye akili.Siyo chama kina mgombea anakuambia ataweka rehani mali asili zenu ili apewe mkopo halafu ufikirie kuingia naye mseto.Kwa kifupi hakuna mseto hapa.Anayeshinda achukue nchi na anayeshindwa akae pembeni asubiri miatano tena.
 
just get your books and pen.put on,yo school uniform trh 29 ni shule utailewa hyo serikali ya mseto
 
Tanzania Bara hiyo kitu ni ngumu sana kutokea, Katiba yetu haijaweka hiyo kitu bayana, hivyo utekelezwaji wake utahitaji utashi wa wahusika kwa kiasi kikubwa na kwa ubinafsi wa CCM sidhani kama hilo litawezekana.

Katiba ya Znz inaruhusu hicho kipengele na nadhani hiyo sheria ilipitishwa na Baraza la Wawakilishi wakati ule kutokana na uwiano wa wabunge kwenye baraza la wawakilishi, CCM na CUF ile ya Seif walikuwa na idadi ya wabunge inayokaribiana, hili likawabana CCM ikabidi wakubali.

Japo CCM walikuja kulazimisha nafasi ya Makamo wa Pili wa Rais iwepo, baada ya Makamo wa kwanza wa Rais kuchukuliwa na Seif, hiyo ya pili akapewa Balozi Seif Ally Idd.

Lakini pia jambo jingine kubwa linalofanya uwepo wa serikali ya mseto kuwa ngumu Bara ni pale ambapo Katiba yetu inatamka mgombea yeyote atakayeshinda nafasi ya Urais, hata kwa tofauti ya kura moja, huyo ndie atakaetangazwa mshindi. Hili linapunguza kwa kiasi kikubwa uwepo wa serikali ya mseto Tanzania Bara.
 
Back
Top Bottom