Ni wiki ya uchaguzi wa Meya jijini Dar es salaam

jigoku

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
2,411
733
Salaam kwenu wana bodi,

Ni asubuhi njema ya Jumatatu ya tarehe 1/2/2016, Ni wiki ya kuelekea uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es salaam, ambao kama hautaahirishwa tena baada ya kushindwa kufanyika mara mbili hivi, basi umepangwa kufanyika tarehe 8 February, 2016 ktk ukumbi wa Karimjee.

Nimeona niweke hapa bandiko ambalo litatoa fursa kwa wanabodi, viongozi wa vyama, viongozi wa serikali, vyama vya hiari, vyombo vya ulinzi na usalama, hasa polisi, mtapata nafasi ya kusoma na kujifunza kitu ambacho kitasaidia ufanyike uchaguzi wa kumpata Meya wa Jiji kwa misingi ya haki, kidemokrasia, uchaguzi wenye amani na utulivu kwa maslahi ya wana Dar es salaam na taifa kwa ujumla.

Aidha mawazo mazuri, ya wapenda haki, na wanaopenda utawala wa sheria watachangia thread hii pasipo ushabiki, uchama, chuki na aina nyingine ya upofu wa uhalisia wa misingi ya uchaguzi.

Nimekuwa nikitafakari sana kwamba kwanini chaguzi hizi zimekuwa na figisufigisu, kiasi kwamba zimepelekea kuvunjika kwa amani, ukiukwaji wa sheria na Kanuni, matumizi ya polisi kudhalilisha baadhi ya wajumbe na hata kufanikisha ushindi wa chama tawala.

Kwa mujibu wa kifungu cha 19 (4) cha sheria namba 8 ya 1982 ya serikali za mitaa, iliyorekebishwa na sheria namba 6 ya 1999, inaelekeza muundo wa halmashauri ya jiji kuwa na;
•Meya wa Jiji na Naibu wake
•Madiwani 3 wa kuchaguliwa kutoka kila halmashauri za manispaa
•Mameya wote
Na Mkurugenzi wa Jiji ambae ndio katibu.

Kwa maana hiyo ili tukamilishe muundo wa Jiji na kuifanya lianze kazi baada ya kutokupatikana kwa muda sasa, ndio maana sasa tunasema uchaguzi na ufanyike kama ilivyopangwa hiyo tarehe 8 February.

Aidha tupeane angalizo kwa mstakabali wa kufanyika uchaguzi huru na wa haki.
Yaliyotokea katika uchaguzi wa Meya jijini Tanga hayajasahaulika mioyo ni na masikioni mwa watanzania wapenda haki, ilikuwa ni tarehe 19 Dec 2015 pale ambapo kama kawaida ya wa kurugenzi kuharibu uchaguzi ama kwa utashi wao kwa kuwa wengi wao ni sehemu ya chama tawala, ama ni kwa uoga wao wa kupoteza ajira zao na ndio maana kutekeleza mashinikizo ya wakubwa wao na chama tawala.

Tuliona jinsi Daud Mayeji ambae ni mkurugenzi wa jiji la Tanga alivyokuwa chanzo cha vurugu, ambazo kimsingi zilikuwa zimepangwa zitokee ili kuhalalisha ushindi wa chama tawala maana naamini uchaguzi wa haki na huru, uchaguzi wenye uwazi na usiokuwa na chembe ya ubinafsi hakuna vurugu zinaweza kutokea.

Maandalizi ya kupora ushindi tunayasoma kupitia viashiria mbali mbali ikiwemo ku deploy idadi kubwa ya polisi eneo la uchaguzi, na wao kuwa sehemu ya uchaguzi wakati wao polisi si wahusika.Ukiangalia idadi wa wajumbe wa kikao hicho cha uchaguzi kule Tanga, ni kwamba UKAWA wana idadi kubwa ya madiwani, takwimu zinasema jiji la Tanga lina madiwani 20 wa UKAWA wakati CCM wana 17 tu.

Mfano Mwingine ni hivi juzi takribani wiki moja sasa imepita kule Kilombero serikali imevuruga tena uchaguzi kupitia mkurugenzi ama kwa vitisho kutoka kwa wakubwa wake au na yeye ni sehemu ya chama tawala.

Kilichofanyika mkanganyiko aliosema haukuwa kosa la wajumbe bali ni serikali na Tume ya uchaguzi badala yake alichokiona yeye ni kile kile ku deploy idadi kubwa ya polisi ambao waliishia kudhalilishwa kwa Mbunge wa Kilombero Lijualikali bila weledi ilikuwa ni matumizi ya dola na wala sio msingi wa vikao ambavyo huongozwa kwa hoja.
Uchaguzi Kilombero umeahirishwa lakini mpaka sasa idadi ya wajumbe ni 37, huku UKAWA wako 19 na ccm 18, wangali wakisubiri siku nyingine ya uchaguzi.

Uchaguzi wa mameya kwa Kinondoni, Ilala na Temeke ulishafanyika lakini tofauti na Yaliyotokea Tanga na Kilombero, ni manispaa ya Temeke tu ambako kimsingi idadi ya madiwani ni 49, huku UKAWA wakiwa na madiwani 18 na CCM wakiwa na madiwani 31, uchaguzi wa Temeke haukuwa na figisufigisu, wala deployment ya nguvu kubwa ya polisi haikuwepo, hii ina maanisha nini? Ni kwamba ukawa ni wastaarbu, hawana fujo wa vurugu pale ambapo wanajua walizidiwa kwa haki, pale ambapo kweli wana idadi ndogo ya madiwani kwa kulinganisha na CCM.

Lakini kwa Ilala na Kinondoni nyote mnajua kilichotokea, ni uchaguzi wa kihuni, ujanja ujanja, kulazimisha na mengine mengi ili mradi kuvuruga uchaguzi.
Takwimu za idadi ya madiwani katika manispaa hizi mbili ni Kinondoni jumla ni 58, CCM 20 na UKAWA 38 wakati Ilala, UKAWA 38 na CCM 23.

Chaguzi za manispaa mbili hizi zilikuwa na matatizo sana, mara mahakamani, mara vurugu mara polisi nk lkn ni kwa sababu idadi ya madiwani wa CCM ni ndogo kuliko wa ukawa. Ndio maana hata wa Zanzibar waliletwa waje kuingia Mabaraza ya madiwani huku bara bila kujali TAMISEMI sio suala la Muungano.Hata hivyo baada ya haki kutamalaki uchaguzi ulifanyika na Kinondoni na Ilala wakaptikana mameya na naibu meya wa UKAWA.

Kwenye hili la Jiji ambapo uchaguzi ni wiki hii tunatoa angalizo kwa wahusika, hasa Mkurugenzi wa Jiji asikubali kukiuka sheria na Kanuni za uchaguzi, hata kama yeye nae ni sehemu ya chama tawala lakini ni bora akubali maamuzi ya wananchi, tayari walishafanya kupitia uchaguzi mkuu na ndio maana kwa idadi madiwani ni wengi kuliko wa CCM hapa Dar es salaam.

Historia haijafutika juu ya mkurugenzi wa Jiji ndugu Wilson Kabwe, tunajua alikopita na aliyowahi kutenda kwa picha moja tu inayohusu utumishi wake akiwa mkurugenzi katika majiji ya Mbeya, Mwanza na sasa Dar es salaam tafsiri yake ni kwamba huyu ni mbia wa chama tawala, au la ni mshirika wa karibu na vigogo/kigogo huko TAMISEMI.

Historia hiyo inaleta kutiliwa mashaka kwa sababu ni lazima angeshachukuliwa hatua za kinidhamu kufuatia tuhuma zake, lakini kinyume chake amezidi kupandishwa cheo. nimuombe tu wakati huu apende kutenda haki kwenye uchaguzi huu maana nae ni mshirika mkubwa.

Pia kama rais atakuwa mwenyekiti wa kikao hiki basi nae asimamie haki uoga wa kuogopa mashinikizo kutoka juu au kuvuruga uchaguzi kwa kuwa nao ni sehemu ya chama tawala waache mara moja.

Ni wiki ya kuelekea uchaguzi wa Meya jiji la Dar es salaam tunahitaji uchaguzi huru na haki kumpata meya, ambapo kimahesabu atakuwa ni meya kutoka UKAWA ndugu Isaya Mwita Charles.

Nawasilisha
 
Wanakusanya nguvu baada ya mechi ya mchana kushindwa, sasa wameingia gizani msoga kupewa kitchen party ila sijui ukawa hawana?
 
Back
Top Bottom