Ni wenye pesa tu ndo watakaohudhuria mahafali ya 40 UDSM

MBUFYA

JF-Expert Member
Aug 15, 2011
445
68
Kiwango cha pesa kilichowekwa na chuo kikuu cha dar es salaam kwa ajili ya kukodi majoho kwa ajili ya mahafali ambacho ni zaidi ya 45000; kimeonekana kuwa tatizo miongoni mwa wahitimu wengi. mpaka sasa ni zaidi ya rafiki zangu kumi wamesema watashindwa kulipa pesa hiyo kwani ni nyingi mno na wengi ni masikini na mpaka sasa hawajapata kazi.
hivyo utofauti upo kati ya maskini na matajiri udsm
 
Wameshafanya mradi hao..pesa yote ya nini! Kwani watu watarudi nayo nyumbani..ni ufisadi tu huo.
 
Wahitimu na degree kichwani bado wanajihesabu masikini? Kushindwa kumobilize 45,000 ni msiba wa kitaifa wakati tunashuhudia sherehe za mamilioni za mahafali.
 
Mpwa japo ni kubwa lakini sio hio uliotaja, ni sh.42,000 na nimelipia leo kwa Masters labda kama undergraduate ni zaidi ya hapo ila kwa Masters ni kiasi hicho, na sisi tulilalamika sana maana at the same time huwezi kupokea thesis-dissertation yako hadi uwe umemaliza ada! Ni maumivu japo ni investment ya maisha!
 
Jamani hivi ni Master's au Masters degree. Katika hili hata wenye akili timamu wamekuwa mazuzu tu, khaaaaa!
 
Hahahaha..kweli TZ maisha magumu!
Mtu anashindwa kulipia 45k kwa ajili ya mahafali??
 
Hahahaha..kweli TZ maisha magumu!
Mtu anashindwa kulipia 45k kwa ajili ya mahafali??

sijakuona kinachokuchekesha ktk hili, huyajui maisha ya Mtz au umeamua tu kuandika? Usijifanye umemaliza kila kitu ktk hii dunia.
 
Watu wanakufa kwa kukosa 5000 ya matibabu! Nyinyi mnadharau 45000?
 
Wameshafanya mradi hao..pesa yote ya nini! Kwani watu watarudi nayo nyumbani..ni ufisadi tu huo.
ndg yangu hii nchi ukifikiria mambo yake inaboa sana. Imagine pesa zote hizo za nini! Ufisadi tuu! Ila we subiri siku 2kiingia vita vya msituni hayo matunda ya ufisadi hawatayafaidi, make hasira zinapanda kila kukicha!
 
Back
Top Bottom