Ni Waziri gani alikwenda gerezani kumshawishi Freeman Mbowe?

Mto wa mbu

JF-Expert Member
Aug 8, 2021
2,195
3,007
Hope mko poa wakuu, hii habari sio maneno yangu, ni siri iliyotobolewa na mjumbe wa kamati kuu ya Chadema, Godbless Lema.

Lema amesema kuna waziri ndani ya serikali ya SSH, alienda gerezani kumtembelea Mbowe, waziri huyo alifanya kikao na Mbowe gerezani, na alimshawishi vitu vifuatavyo.

Mama hana shida na Mbowe, na yuko tayari kumrudishia vitu vyake vyote alivyonyanganywa kama Billicanas, pesa zake alizonyanganywa na mali zote.

Lema ameongeza kuwa SSH, hataki stress so Mbowe aachane kabisa na wabunge wa Covid-19, hasiwaongelee kabisa.

Mwisho achane kabisa na katiba mpya, yaani hasilizungumzie ilo la Katiba Mpya, na mbeleni wangeweza kukaa mezani na kutengeneza katiba ya kufanya kazi kwa pamoja (hapa walitaka wa negotiate Power).

Lema ameongeza kuwa Mbowe alimpigia simu akiwa na hasira sana, na alikataa mapendekezo yote yaliyoletwa na huyo waziri, alimjibu waziri huyo kuwa yuko tayari kufia magereza lakini hawezi negotiate masuala ya haki.

Nimeshtuka sana kusikia maneno ya Lema, yaani sisi tunaumia na Mbowe kuwa gerezani, lakini Mbowe hata haogopi kitu, na ni wazi serikali wanachanganyikiwa huyu mtu huu msimamo mkali anautoa wapi.

Finally ni waziri gani huyo aliyeenda kumrubuni Mbowe anegotiate na watawala.

Source: Godbless Lema jana
 
Hii dhambi ya kumuweka Mbowe gerezani wakati ikijulikana wazi hana hatia yoyote, itamsumbua sana Samia na utawala wake.

Hata afanye jema lipi, hili la Mbowe ni doa kubwa katika utawala wake..

Tulimsema sana JPM hapahapa JF na utawala wake usio wa haki, utawala wa mabavu wa kuteka-teka watu na kuuwa watu ovyo, na March 17 Mwaka 2021 MUNGU akajibu, tulirudi kati na kuanza upya..

Hili la Mbowe kuwekwa jela pasipo haki halitoiacha hii serikali salama..

MUNGU hadhihakiwi kwa namna yoyote ile hata mara moja..

Ee Mwenyezi MUNGU, ni wakati wa kutenda sasa.
 
Back
Top Bottom