jiwe angavu
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 20,009
- 38,302
Madelo Gawiza.
Naomba niende moja kwa moja kwenye mada husika..hali ya uchumi ya nchi yetu iko taabani..hili limejidhihirisha wazi kabisa kupitia hotuba ya leo ya Rais wetu katika uzinduzi wa ulipaji kodi kwa njia ya kielekitroniki.
Ukiisikiliza kwa umakini hotuba ya JPM zile Mbwembwe na maneno makali ya utumbuaji majipu na vitisho..yameshindikana kutumika katika hotuba yake..badala yake kuongea lugha ya upole na usistizaji juu ya ulipaji kodi.
Amezungumza kwa kuyaomba na kuyataka makampuni kulipa kodi..kwa lugha ya upole sana..hii inaonyesha niwazi sasa hakuna namna zaidi ya kuwabembeleza waingie kwenye mfumo wa kielekitroniki ili angalau tupate kodi.
Kuna vishiria vingi vya kueleza hili suala la anguko kiuchumi..hasa pale alipo sisi tiza suala la kutafuta vyanzo vipya ya ukusanyaji kodi..si suala baya ila inafikia hatua rais anaomba tra wabuni hata mbinu ya kutengeneza vitambulisho na kuviuza kwa wamachinga ili iweze kujiongezea mapato.. kwangu mimi hili linaonyesha wazi hali yetu kiuchumi sio shwari kabisa.
Tunakoelekea nadhani si mbali zile kodi za kichwa zitarudi..ili mradi kuirudisha pesa serikalini ili serikali iweze kujiendesha..
Suala pia la kusitisha ajira na kupunguza wa fanya kazi serikalini kwa kisingizio cha kuleta weledi katika utumishi wa umma ni la kisiasa zaidi..ila ukweli ni kwamba serikali imeelemewa kiuchumi.
Ukitizama pia katika bajeti ya mwaka wa fedha unaoisha 2016/2017 bajeti ilishindwa kuvuka hata asilimia 30 kwa baadhi ya wizara..huku wizara zingine zikipata zaidi ya aslimia 150..huu pia ni uendeshwaji mbovu wa serikali kupitia matamko ya JPM bila kuzingatia sera na utawala bora..katika mgawanyo wa bajeti ya serikali.
N.B: naunga mkono juhudi zote za Raisi katika kuleta maendeleo ya taifa hili.. ila naomba azingatie sera,na utawala bora hasa kufuata mwongozo na kanuni za bunge katika utekelezaji wa bajeti..