Ni wazi sasa CCM imewabana CHADEMA bungeni

Hii ni wazi tunavutiwa na chadema, wajua chadema kaleta changamoto ya ukweli katika kutetea wananchi pia kuisimamia serikali, ivyo wananchi wengi wamekuwa wakivutiwa kuangalia sessions za bunge hasa kusikia watetezi wao (chadema) wakiongea, huku tukifurahi jinsi wabunge wa ccm wenye uelewa mdogo wanavyojigonga na kukomaa mishipa ya shingo kuitetea serikali tunayoifahamu kwa matendo maovu na ya kifisadi. Natumai mmemuona ngeleja alivyopwaya
 
CCM NA UTETEZI WA BAJETI YA KI-FISADI KUTOKA JUU, WAPINZANI NA BAJETI YA WALALAHOI KWA AJILI YA MAENDELEO ZAIDI NA KONGAMANO KIDUCHU

Siku zote Bajeti zisizozingatia MAONI YA WADAU WENGI ZAIDI mwisho wa siku huzaa migomo kibao kila kona ya nchi.

Bajeti ya safari hii ni muhimu ikama SHIRIKISHI ZAIDI na kwa yeyote yule
anayediriki kuita Bajeti ya Mhe Zitto Kabwe 'RUBBISH' you will soon be in for a rude shock toka kwa wadau. Hatupo tayari tena bunge letu kutumika kuwapitishia WAKUBWA bajeti zao binafsi za KIJANJAJANJA kwa ajili ya kuchota kodi zetu na MAENDELEO sifuri kila leo!!!

Wananchi sote kwa idadi yetu,sote tulioelimika na tusioelimika, kwa pamoja tuelekeze akili zetu Bungeni Dodoma TAYARI KWA KUTETEA 'BAJETI YA MLALAHOI' sambamba na viongozi wetu wa upinzani kule bungeni wanavyoendelea kututetea.

Bajeti yetu bungeni safari hii ni sharti itenge fedha kwa ajili ya MAENDELEO kwa asilimia 75 % na fedha kwa ajili ya gharama za UTAWALA, POSHO NA MIKONGAMANI safari hii kamwe isizidi asilimia 25 %.

Fedha kwa ajili ya Mikopo Elimu ya Juu nayo lazima iende juu 4 fold ili Tanzania yetu iweze kuwekeza zaidi katika elimu kuongeza ubora wa watu wetu kushindana kwa tija katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

WaTanzania sote kwa pamoja tuseme HAPANA kwa bajetiiliosheheni mawazo ya viongozi peke yao maofisini huko CCM bila ya kujali kuzingatia maoni yetu kupitia baadhi ya wabunge wetu Bila walio makini sana na maslahi yetu.

Naam, nasema bila 'Bajeti ya Mlalahoi' kwa ajili ya kuleta unafuu zaidi wa maisha, ajira zaidi, na maendeleo zaidi badala y MIPOSHO NA KONGAMANO zisizoisha, HAKUPITISHWI KITU PALE.

Wabunge wa upinzani wote sauti zenu zisiposikilizwa humo ndani ya bunge basi moja kwa moja KATUTUPIENI MPIRA HUKU MITAANI tukamaalize kazi.
 
tusimung'unye maneno CDM ni watetezi wawanyonge wa taifa hata kambi nyingine wanajua kuwa wanachokifanya sicho ila wanajikaza kisabuni kwani wanapaswa kujikaza ili kuficha aibu

tusubiri kimbunga 2015
 
Magamba mpaka wawezeshwe na ndugai ni DHAIFU hvyo keshafel mchezo wao umeshashtukiwa
 
KATIKA GAZETI LA MAJIRA LA LEO, KUNA KICHWA CHA HABARI TFF yazitaka Simba na Yanga kukaza buti!! '' Habari inaanza kwa kusema Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania limezitaka Simba na yanga kuhakikisha zinalibakisha kombe la Kagame, linaloandaliwa na vyama vya mpira wa miguu Afrika Mashariki na kati (CECAFA). Kauli kama hii ni nzuri ila kinachonisikitisha hapa nakuona ni jinsi gani hata viongozi wetu wa soka wamejaa siasa za Simba na Yanga ni Kitendo cha kuzitaka Simba na Yangu tu bila Kuzungumzia Azam!!!. Tunakwenda wapi kwa staili hii. Hivi kichwa cha mwendawazimu kitaaisha. Itakuwaje kwa viongozi wa TFF pale Azam itakapolichukua kombe?. Au Azam si timu ya Tanzania hata isizungumziwe ? Nawaasa viongozi wanguwa tiefu efu acheni hizo. Kichwa cha mwendawazimu kinaanzia kwenu na unazi wa kijinga!
Wazungu wanamsemo ambao wanapenda kuutumia kwa mtu mkubwa mwenye akili ya kitoto au anayefanya utotototo....wanasema '''SHAME ON YOU'''. Namimi nasema shame on TFF


Haya nayo,ni kutokea huko Bungeni?
 
Hakuna kitu hapo. Wanachofanya CCM ni kama kwenye mpira timu inacheza deffeceve bila kushambulia. Kila mpira ukija wanatoa kona au wanasababisha free kick au penalt. Matokeo yake watafungwa goli jingine baada ya lile la jana na mshambuliaji machachari Mnyika.

siku hizi wanasema wamepaki basi
 
Niwazi kabisa mikakati yao inaonesha wazi ni udhaifu wao ndio unawafanya wachanganyikiwa.
 
Back
Top Bottom