Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Kuna vitu vinaudhi sana. Serikali ya CCM walifanya mbwembwe nyingi kusema wanafufua huduma ya treni kwenda Arusha na Tanga. Na tukumbuke walitumia fedha yetu ya kodi, sio fedha za CCM.
Sasa ni wazi kwamba yote haya walifanya kwa ajili ya kampeni waliyotaka kufanya ya maendeleo ya vitu, ili kuwashawishi watu wa kanda ya Kaskazini ambako CHADEMA imeotesha sana mizizi. Hivi hizo treni walizosema zinarudi ziko wapi, mbona hatuzioni?
Na sasa hizi reli zimekuwa kero ya faini za trafiki. Askari wa trafiki wanakaa karibu na reli zinapokatisha barabara halafu wanapiga watu faini eti unatakiwa sio tu upunguze kwendo unapovuka reli bali usimame kabisa kwa sekunde kadhaa. Juzi nimegombana na trafiki kwa ajili ya hili nikamuuliza, kwani leo zimepita treni ngapi, au mara ya mwisho treni imepita hapa lini, na ikipita huwa inapita saa ngapi?
NIliona polisi wameweka hata kibanda cha trafiki karibu na hiyo railway crossing, labda wameona faini ni nyingi sana. Serikali ituambie kama kweli walikuwa na lengo la kurudisha huduma za treni au ilikuwa ni mbwembwe tu za kampeni. Na pia tuelezane basi kama fedha iliyotumika kurekebisha hizi reli mnataka irudi kwa njia ya faini za trafiki!
Jamani tumechoka na hizi faini za trafiki za kulazimisha, mnataka tufanye nini?