Ni wazi kwamba Viongozi wa CCM walikuwa na majina yao mfukoni

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
119,539
223,006
Mwaka 2015 Kingunge Ngombale Mwiru , mwanasiasa mkongwe aliyeitumikia ccm kwa kipindi kirefu kwa wakati ule kuliko mwanaccm yeyote aliyekuwa hai , alijivua uanachama wa ccm kwa madai kwamba viongozi wa ccm wa wakati ule akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti Jakaya Kikwete waliingia kwenye vikao vya Chama chao wakiwa na majina ya wagombea wanaowataka kwenye mifuko ya suruali zao, Mungu amlaze mahali pema peponi mzee Kingunge aliyekataa unafiki uzeeni , Maandiko Matakatifu yanasema kwamba , NJOONI KWANGU WOTE MLIOLEMEWA NA MIZIGO YA DHAMBI NAMI NITAWAPUMZISHA.

ukifuatilia maelezo ya Polepole kwa waandishi wa habari kuhusu kuteuliwa kwa baadhi ya wagombea ubunge , utagundua kwamba kulikuwa na matakwa ya viongozi kuhusu nani wa kuteuliwa , kwa mfano , akizungumzia kuteuliwa kwa Mwana FA alisisitiza kwamba waliona ni bora kuchanganya na wasanii kwenye uteuzi wao , kwamba yeye Polepole na viongozi wengine wakaamua tu kumuondoa aliyeshinda kihalali ili kumuweka wamtakaye wao ( jina la mfukoni ) , tena wala hawakusema aliyeshinda kama alikuwa na makandokando , yaani wameamua tu wao watakavyo ! Wajumbe wakapuuzwa !

Ukiacha Mwita Waitara na Dr wa mifugo Mollel , wasaliti wote waliohama vyama vyao waliangukia pua kwenye kura za maoni akiwemo Pauline Gekul na David Silinde , tena waliangushwa hasa , lakini hapa napo wajumbe ambao pia ni wapiga kura majimboni wamepuuzwa , hii ni baada ya waliowakataa kurejeshwa kugombea , haya ni majina ya mfukoni , haifahamiki kama ni mfuko wa Mwenyekiti , Katibu au Polepole .

Wito wangu kwa wajumbe ni kwamba bado mna nguvu kubwa sana ya kuamua huko majimboni , wafundisheni adabu viongozi wenu .
 
Haka kajamaa kanafiki kweli. Mbona nyie mmemtoa dada wa watu aliyeshinda kura za maoni mmeliweka dume John Mrema ambalo alilishinda, hata aibu hamna. Yaani Nyinyi, God forbid, mkipata Dora mnaweza kuwa wabaya mara 100 ya waliopo. Mna tabia ya hovyo Sana ya kulazimisha kila mnalofanya nyinyi hata Kama ni baya lipate justification.
 
Haka kajamaa kanafiki kweli. Mbona nyie mmemtoa dada wa watu aliyeshinda kura za maoni mmeliweka dume John Mrema ambalo alilishinda, hata aibu hamna. Yaani Nyinyi, God forbid, mkipata Dora mnaweza kuwa wabaya mara 100 ya waliopo. Mna tabia ya hovyo Sana ya kulazimisha kila mnalofanya nyinyi hata Kama ni baya lipate justification.
Pole kwa mawe mkuu , Magufuli aliposema hana mgombea alilenga kumdanganya nani ?
 
Kwa upande wangu ninaona siyo vema kumuacha aliyeshika namba moja halafu unamchukua mtu aliyeshika namba tano au sita. Mfano wa Muheza. Kwa kweli huwezi kueleweka.
 
"Na tumfanye mtu kwa sura yetu..." Kama utapata kuielewa vema sentensi hii, ni wazi kuwa utaelewa kwanini Katibu Humphrey Polepole aliyasema hayo kuhusu uteuzi wa Mwana FA.
 
kwani hivi nyie chadema kule jimbo la segerea alishinda nani na ninyi mmemweka nani.
kweli nyani haoni ku......le
 
Back
Top Bottom