Bwana Bima
JF-Expert Member
- Jul 29, 2014
- 418
- 885
Kumeanza kuibuka wimbi la utolewaji wa ripoti za fedha za miradi ambazo zimekuwa na mashaka makubwa sana na hasa zinaumiza walipa kodi, kuna harufu ya rushwa na ibadhirifu mkubwa tu tena kwa miradi ambayo haina msingi sana.
Mfano bajeti ya ukarabati tu wa ofisi ya makamu wa rais ambayo imeonyesha zaidi ya 1.7 Bilion imektumika. Ukiachilia hilo mradi wa ujenzi wa mnara wa mashujaa ambao inadaiwa awamu ya kwanza tu bajeti ni bilioni 1 maana yake hapo bado kuna fedha zingine zinatafutwa.
Hapo hapo ripoti imetoka leo serikali ikipatiwa mamilion ya fedha za mkopo kutoka IMF. Hii ni hatari sana kwa taifa. Ni wazi kwamba pesa zote zinatafutwa kwa ajili ya kampeni za uchaguzi wa 2025. Hii haina utofauti na uchaguzi uliopita zaidi ya bilion 10 zilitolewa kabla kwa ajili ya ukarabati wa viwanja vya mpira tena vya CCM.
Nchi shida sana hii watu wanahangaika na njaa mtaani watu wanatafuna tu pesa!