kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Kauli aliyotoa Makamu wa kwanza wa Rais alipokuwa Pemba ilikuwa kauli nzito iliyoashiria kuvunjika kwa mashirikiano yaliyopo. Kauli ile ilieleza wazi dhamira yake ya kutoendelea na madaraka kwenye kundi la watu wasioridhika na ambao hawana uchungu na watu kufa, kuwa vilema nk. Alihoji watu wanatafuta madaraka ya Nini? Wameua na kuumiza watoto ikiwemo ubakaji lakini bado awajaridhika, Wakati vidonda vikiwa vibichi watu wale wale kwa kutumia tume ile ile wanakwenda tenda kwa wahanga walewale wakuiba uchaguzi. Wanatafuta Nini?
Bila kuficha hisia zake aliwaomba waislam wakae na watafakari namna ya kuponya majeraha na kwamba anakubaliana na Serikali ya Kitaifa kwa 100% ila yeye hatokuwa sehemu ya Serikali hiyo.
Naamini kauli ile kwa uzito wake na kwa ninavyo mfahamu ndugu yangu Zitto haikuwa kauli ya chama Bali msimamo binafsi na kwa kutambua hilo Zitto amekaa kimya kwa muda mrefu bila kuwa na harakati za siasa mitandaoni kama kawaida.
Lakini waliosumbuka zaidi ni Chama cha Mapinduzi na kupelekea kuitana kwa dharura na kisha kumwelekeza mgombea aliyepita bila uhalaali ajiuzulu Jambo ambalo amelitekeleza. Lakini kwa upande mwingine ili kuficha uchafu wa tume ya uchaguzi na uchafu wa CCM barua iliyotolewa na kiongozi wa CCM ndugu Shaka inadai Mbunge huyo amejiuzulu kwa sababu za kifamilia na wananchi wawe wavumilivu.
Unajiuliza huyo Mbunge kaongeza Mke, kashikizwa na familia au kafanyaje. Haya ni mambo yasiyopaswa kufanywa na watu waliopewa dhamana, usanii tunaoona ndio unaoendelea Hadi kwenye miradi ya maendeleo na mikataba ya rasilimali zetu. Kila Jambo wizi tu.