Ni wazi Jakaya Kikwete anahitaji kuombewa kama sio kufanyiwa tambiko...!!

Sajenti

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
3,651
412
Nilisikiliza hotuba ya Kikwete jana katika TV katika utaratibu wake wa kuhutubia wananchi kila mwisho wa mwezi. Kwa maoni yangu kwa muda wote wa hotuba yangu sikuona jambo jipya alilozungumza na kuonyesha yeye kaka mkuu wa nchi ana muelekeo wa kuchukua hatua na hasa kwa mambo yanaoonekana wazi kuwachosha watanzania. Suala la mgao wa umeme, Dowans, mfumuko wa bei, kupanda kwa gharama za maisha anazumgumzia katika mtazamo wa kuwaonea huruma wananchi wake badaa ya kuonesha nini atafanya yeye kama raisi.

Lakini kubwa zaidi alilonishangaza ni juu ya lawama zake kwa CHADEMA. Kuwa chama hiki kinamuelekeo wa kuleta chuki, vurugu na kutaka kuitoa serikali iliyoko madarakani kwa nguvu. Nadhani Kikwete anakimbia kivuli chake mwenyewe. Kinachofanywa na CHADEMA kwa mtazamo wangu ni kuwaamsha watanzania juu ya utendaji mbovu wa serikali ya CCM na pia kuiamsha serikali hiyo kuwa mnakolipeleka taifa sio.

Mambo mengi yaliyokuwa yakitokea ndani ya serikali ya CCM wanatanzania wasingeyajua kama si wabunge na viongozi wa CHADEMA kuyaweka hadharani.Na mengi ya mambo hayo ni yale yaliyopeleka kuingiza nchi katika wakati mgumu kabisa.

Sasa kiongozi wa nchi anapotoa hotuba ya kuonyesha masikitiko kwa wananchi wake badala ya kutoa njia za kutatua matatizo yanayojitokeza napata mashaka na uwezo wa kiutendaji wa huyu bwana.

Nadhani umefika muda sasa watanzania wote bila kujali itikadi zetu za vyama, dini, kabila kufanya maombi kama sio matambiko ili kumuomba mungu amsaidie huyu bwana kuliongoza taifa letu katika njia iliyo sahihi kwani kwa sasa gari limepoteza mwelekeo kabisa.
 
imekaa vizurui naomba niwe kiongozi wa waganga maana kwa tatizo la Kikwete mimi ndo naweza kumsaidia.... ni .... tu
 
imekaa vizurui naomba niwe kiongozi wa waganga maana kwa tatizo la Kikwete mimi ndo naweza kumsaidia.... ni .... tu
...Thanks mkuu kwa offer yako nina imani wadau wataifanyia kazi......Kwa kweli mkuu wa kaya hajatulia kabisa..:A S 13::A S 13::A S 13:
 
Aendelee tu kwa Sheikh Yahya, akiombewa mapepo yatayotoka kichwani mwake yatasababisha mtikisiko mkubwa kuliko ule wa mabomu ya Gongo la mboto.
 
...Thanks mkuu kwa offer yako nina imani wadau wataifanyia kazi......Kwa kweli mkuu wa kaya hajatulia kabisa..:A S 13::A S 13::A S 13:
ni kweli mkuu jamaa kapoteza dira kabisaa! nadhani hata msaada hana Mungu amwongoze kwakweli!
 
Unajua JK na CCM yake wanashangaza sana! Wabunge wa CHADEMA walitoka nje ya Bunge kupinga mabo fulani kwa amani wao wakalalamika kwamba huo sio uungwana! Chadema Wakaenda Arusha kupinga uhuni wa kupiga kura za Meya wakala mkongoto! Chadema Wameenda kanda ya ziwa kuhamasisha siasa sasa " wanatishia amani!" This is what we call changing goal posts!! Kilichobaki Chadema wataambiwa waombe ruksa kwa JK waseme nini kwa wananchi! CCM is scared stiff na wajilaumu na kujiombea bila kuchoka.
 
Huwa anaspin ,kwanza alisema CDM inaeneza udini, hiyo haikuleta impact na sasa kaja na hii CDM wanaleta vurugu . Hivi alimaanisha vurugu ipi haswa? Asubiri aone peoples power ::::::
 
alianza pinda kaja anne makinda sasa president mwenyewe au wanalia kwa sababu uongo wao kwa watanzania sasa haufanyi kazi? na bado hiyo ni rasharasha mvua yenyewe yaja
 
JK anahitaji kuombewa.ni matatizo wanayoyapata wale woote wanotegemea waganga na wachawi katika uongozi.tunatakiwa tujifunze kutoka kwa JK.alitegemea waganga eti ndo wamuongoze,alitegemea akina sheikh yahya eti ndo washauri wake..sasa ndo haya yanayompata.wamechukua ufahamu wake wote wamemuacha mtupu..msimuone vile ni mwili tu,lakini akili yake na medula oblangata walishaichukua.tumuombee rais wetu mpendwa.hivi unategemea kuzungukwa na makamba,tambwe hiza na rostam halafu ukatoka salama?!?!RAIS HAYUKO SALAMA.NI VYEMA AKAJIUZULU KABLA MAMBO HAYAJAWA MAMBAYA ZAIDI
 
aah... presidaaaaaaaaaaa...!! president is crying!
....Si ndio hapo. Father house analia sijui watoto wafanye nini?? Hayati Mwl. Nyerere alisema ikulu ni pagumu na sio mahali pa kukimbilia. Kiongozi makini hawezi kukimbili ikulu....Sasa huyu Mr. Presidaaaaaaaaaaaaaa mh!
 
Alifikiri ikulu ni mahali pa kupiga soga akapakimbilia sasa maji yanazidi unga na bado unajua yeye alifikiri uchaguzi umekwisha sasa ni kulala usingizi mpaka uchaguzi unaokuja kumbe wenzan CDM hawalali mpaka kieleweke.
 
hivi president kwenye ile speech amepromise atafanya nini kabla ya speech ya mwezi ujao?......maana mi sikuangalia......au mwezi ujao ataupotezea?

Maana nimesikia tu matatizo na malalamiko......solutions ni nini?....au solutions atazitoa mwezi ujao?
 
Jamen mi mwanzoni kabisa nilitoa rai kwa JK nikasema iviiiii! Kikwete umeamua kuchukua kura za Dkt Slaa, rais aliyechaguliwa na wananchi wa TZ kwa kumwamini wewe ukazifanya kuwa zako na kuingia madarakani kwa nguvu ya wizi. sasa watanzania mara zote hawatagombana na wewe kwa kukutoa bali wanamwamini Mungu wao sana na kuamini kuwa yeye mwenyewe atapambana na wewe. Nikajaribu kufanya tathimini bubu kwa baadhi ya wakaaji wa Tanzania na washika imani za dini zao ikaoneakana na nikagundua kua kikwete hautambuliki kama wewe ni raisi halali wa wa Tanzania, na wengi wao wanaomba Mungu apishe mbali uongozi wako, na wengi wetu hatuombi kuwa Mungu akupe HEKIMA na BUSARA ya kuingoza nchi yetu bali tunaomba Mungu akupe adhabu ili ujifunze kutokuiba na kuwadanganya watu wake. SASA tunayoyaona sasa ivi yakimtokea JK ni kwamba Mungu kamnyima hekima na Busara kama walivyo viongozi wengine wa nchi, amebaki ni wa kulalamika na kulaumu na kukosa akili juu ya kutatua matatizo na changamoto zinazojitokeza ndani ya Taifa! na tusdhani ni kawaida bali ni laana na adhabu ambazo watu na watumishi wa Mungu wamemwachia, waganga na wachawi kama akina Yahya hawawezi fanya lolote mbele ya hasira ya BWANA, Kikwete jaribu kujifunza na usome habari za Farao kpindi kile amekataa kuwaruhusu wana wa Israel kwenda kumtumikia Mungu wao Kanaan, usje ukatupa shida kwa sababu ya moyo wako kuwa mgumu, achia Nchi please, watu wakamtumikie Mungu kwa raha na Amani ya moyoni na rohoni!. Cha msingi ni Kikwete kuomba radhi na kutubu kwa Mungu na mbele ya Umma wa Tanzania kwani umekosa na CCM nzima!, la sivyo tutakushuhudia wenyewe JK ukienda kuwa kama mfalme Nebkadreza.
Yangu macho!
 
Hivi wale viongozi wa dini(mbalimbali)waliomfuata slaa(PhD)baada ya uchaguzi kumsihi akubali matokeo leo hii wamepotelea wapi?kwa nini wasimshauri mkwere aachie ngazi kunusuru uhai wa taifa hili?
 
Naomba nimpe ushauri baba yangu Kikwete. CDM kwenye kampeni zao wkt wa uchaguzi mwaka jana walihaidi kama wangepata ridhaa ya kuongoza nchi hii wangeunda serikali yenye baraza dogo la mawaziri wasiozidi 20. Jk na CCM yake wasiongoze kwa mazoea, kwa sababu Mwl. Nyerere alikuwa na baraza kubwa la mawaziri wkt huo basi na mimi mkwere nifanye hivyo hivyo. Jk punguza baraza lako la mawaziri ili na matumizi yapungue, kusanya kodi kwa nguvu zote usiwaonee huruma wafanyabiashara wa kiasia hata kama walikuchangia kwenye kampeni, wabane wakurugenzi wa halmashauri wasitabanye fedha unazowapa kwa ajili ya maendeleo. Na wewe mwenyewe punguza kuwa Sinbad baharia.
 
Back
Top Bottom