Mtoto wa Shule
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 11,627
- 8,567
Kwa jinsi ulivyoandika inaonekana hawa mabinti wameruhusiwa ili aliyeruhusu apate "mchongo" wa kupiga pesa za WB na sio kwamba anawapenda hao mabinti!Kila mwaka Tanzania zaidi ya wasichana 6,500 waliachishwa|walifukuzwa shule kwasababu ya kupata mimba wakiwa shuleni,
Mwaka 2017 aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt John John Joseph Pombe Magufuli kwa kutumia nguvu ya Rais alikataa watoto hawa kuendelea na masomo.
Benki ya Dunia ikatunyima fedha kiasi cha $300M karibu TZS 6.9BL baada ya kiongozi mkuu wa ACT-Wazalendo Mhe Zitto Zuberi Kabwe kuwataka wafanye hivyo,
Je kulikuwa na haja kwa Hayati Rais Magufuli kufanya hayo?
Sote tunafahamu,Mimba sio ugonjwa, Mimba sio kilema,Mimba sio laana ,Mimba ni dalili ya ukamilifu na utimilifu wa kizazi cha mwanamke,
Lakini pia, Mimba ni baraka ya Uzao toka kwa Mungu iweje iwe laana?
Kwamtazamo wangu,awamu zilizopita zilimchukulia Mwanafunzi aliyepata mimba akiwa shuleni kitofauti sana
1. Zilidhani kupata mimba shuleni ni laana toka kwa Mungu na Wanadamu,
2. Zikamwona kama ni mtoto asiyefaa tena kuishi duniani
3. Zikafikiri ni mtoto asiyetakiwa kupata elimu tena utadhani mimba inafuta kumbukumbu,
4. Zikamwona kama malaya na huenda akipewa nafasi nyingine ya kuendelea na masomo atasambaza tabia hiyo mbaya kwa wanafunzi wengine,
5. Ziliamini kabisa ni mtoto asiyevumilika tena katika kuendelea na masomo yake,
Zitto Kabwe na baadhi ya Wabunge wa CHADEMA kama Esther Matiko na Halima James Mdee pamoja na wanaharakati wengine nguli wa kimataifa kama Maria Tsesai Sarungi,Kigogo,Lissu na Shangazi Fatuma Karume na wengime wengi,
Watu hawa Wote kwa pamoja, walimpinga Hayati Dkt John John Joseph Pombe Magufuli kwa nguvu na kwaakili zao zote,
Wakati huohuo wakiziandikia taasisi mbalimbali za kimataifa hasa UNESCO|SIDA|IMF|WB zisitishe misaada na mikopo ya masharti nafuu kwa Tanzania kwa kukiuka haki hii ya Watoto,
Kwanini tusimpongeza Rais Samia kwa hili
Leo kwa mara ya kwanza toka kwa Rais wa kwanza mwanamke anayetambua kwa mifano kuwa "Mimba si laana wala mimba sio kilema cha akili"
Rais Samia tayari amerejesha furaha iliyopotea kwa miongo mingi kwa waathirika hawa wa mimba za mashuleni,
Leo haijalishi mimba mwanafunzi kaipataje iwe ni kwakubakwa au kurubuniwa cha kwanza mtuhumiwa atakwenda jela miaka thelathini,
Kisha mwanafunzi huyu baada ya kujifungua mtoto atarejea Shuleni kuendelea na masomo kama kawaida,
Tunaposema Rais Samia ni mteule wa Mungu tunamaana hii kwani hakuna mtimilifu mbele zake,
Hebu chukua huu mfano
Martha Karua mwanasiasa nguli tena mwenye ushawishi mkubwa nchini Kenya,
Martha ndiye anayetarajiwa kuwa Mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais kwenye Uchaguzi Mkuu Ujao wa Kenya wa mapema 2022,
Ningumu kuamini ila mama huyu ni muhanga wa "Mimba za Shuleni " aliyepewa nafasi ya pili kuendelea na masomo yake,
Kwa msiofahamu, Kenya imekuwa na ruhusu kwa Wale wanaopata mimba shuleni kurejea na kuendelea na masomo yao baada ya kujifungua,
Nakwamantiki hii,Huenda Kenya ikapata Makamu wa Rais aliyepewa mimba akiwa bado shuleni,
Tunamengi ya kujifunza ila kwa sasa pongezi nyingi zimfikie Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutambua kuwa mimba sio laana bali ni baraka toka kwa Mungu.