Dunia imesimama na Rais Samia Suluhu Hassan hoja ya Teenage Mothers

Kila mwaka Tanzania zaidi ya wasichana 6,500 waliachishwa|walifukuzwa shule kwasababu ya kupata mimba wakiwa shuleni,

Mwaka 2017 aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt John John Joseph Pombe Magufuli kwa kutumia nguvu ya Rais alikataa watoto hawa kuendelea na masomo.

Benki ya Dunia ikatunyima fedha kiasi cha $300M karibu TZS 6.9BL baada ya kiongozi mkuu wa ACT-Wazalendo Mhe Zitto Zuberi Kabwe kuwataka wafanye hivyo,

Je kulikuwa na haja kwa Hayati Rais Magufuli kufanya hayo?

Sote tunafahamu,Mimba sio ugonjwa, Mimba sio kilema,Mimba sio laana ,Mimba ni dalili ya ukamilifu na utimilifu wa kizazi cha mwanamke,

Lakini pia, Mimba ni baraka ya Uzao toka kwa Mungu iweje iwe laana?

Kwamtazamo wangu,awamu zilizopita zilimchukulia Mwanafunzi aliyepata mimba akiwa shuleni kitofauti sana
1. Zilidhani kupata mimba shuleni ni laana toka kwa Mungu na Wanadamu,

2. Zikamwona kama ni mtoto asiyefaa tena kuishi duniani

3. Zikafikiri ni mtoto asiyetakiwa kupata elimu tena utadhani mimba inafuta kumbukumbu,

4. Zikamwona kama malaya na huenda akipewa nafasi nyingine ya kuendelea na masomo atasambaza tabia hiyo mbaya kwa wanafunzi wengine,

5. Ziliamini kabisa ni mtoto asiyevumilika tena katika kuendelea na masomo yake,

Zitto Kabwe na baadhi ya Wabunge wa CHADEMA kama Esther Matiko na Halima James Mdee pamoja na wanaharakati wengine nguli wa kimataifa kama Maria Tsesai Sarungi,Kigogo,Lissu na Shangazi Fatuma Karume na wengime wengi,

Watu hawa Wote kwa pamoja, walimpinga Hayati Dkt John John Joseph Pombe Magufuli kwa nguvu na kwaakili zao zote,

Wakati huohuo wakiziandikia taasisi mbalimbali za kimataifa hasa UNESCO|SIDA|IMF|WB zisitishe misaada na mikopo ya masharti nafuu kwa Tanzania kwa kukiuka haki hii ya Watoto,

Kwanini tusimpongeza Rais Samia kwa hili
Leo kwa mara ya kwanza toka kwa Rais wa kwanza mwanamke anayetambua kwa mifano kuwa "Mimba si laana wala mimba sio kilema cha akili"

Rais Samia tayari amerejesha furaha iliyopotea kwa miongo mingi kwa waathirika hawa wa mimba za mashuleni,

Leo haijalishi mimba mwanafunzi kaipataje iwe ni kwakubakwa au kurubuniwa cha kwanza mtuhumiwa atakwenda jela miaka thelathini,

Kisha mwanafunzi huyu baada ya kujifungua mtoto atarejea Shuleni kuendelea na masomo kama kawaida,

Tunaposema Rais Samia ni mteule wa Mungu tunamaana hii kwani hakuna mtimilifu mbele zake,

Hebu chukua huu mfano
Martha Karua mwanasiasa nguli tena mwenye ushawishi mkubwa nchini Kenya,

Martha ndiye anayetarajiwa kuwa Mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais kwenye Uchaguzi Mkuu Ujao wa Kenya wa mapema 2022,

Ningumu kuamini ila mama huyu ni muhanga wa "Mimba za Shuleni " aliyepewa nafasi ya pili kuendelea na masomo yake,

Kwa msiofahamu,
Kenya imekuwa na ruhusu kwa Wale wanaopata mimba shuleni kurejea na kuendelea na masomo yao baada ya kujifungua,

Nakwamantiki hii,Huenda Kenya ikapata Makamu wa Rais aliyepewa mimba akiwa bado shuleni,

Tunamengi ya kujifunza ila kwa sasa pongezi nyingi zimfikie Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutambua kuwa mimba sio laana bali ni baraka toka kwa Mungu.
Kwa jinsi ulivyoandika inaonekana hawa mabinti wameruhusiwa ili aliyeruhusu apate "mchongo" wa kupiga pesa za WB na sio kwamba anawapenda hao mabinti!
 
Hili ni Tangazo la watoto wa Vijijini na Maskini Wanaoamini kwenye kuwa na watoto wengi. Town huwezi kuona Mtoto wa shule ana mimba . Akiwa hana mtoto shule kwake ilikuwa ngumu, baada ya kuwa na mtoto atafaulu kweli? Ndio maana wakaweka na Sheria ya Kurudia Mitihani

Mdogo wangu akishika mimba na anasoma tutagawana Majengo ya Serikali. FULLSTOP!
 
unajua hii concept wengi sana inawachanganya..

tumeruhusu wajawazito kurudi shule sawa inawezekana ni uamuzi mzuri, lakini je ni sawa kwa binti mdogo mwanafunzi kupewa ujauzito na kuzalishwa au kufanya ngono?..... hapa ndio kwenye concept na failure za wasomi wetu...

Juhudi gani kali tumefanya sasa kuwalinda hawa mabinti na ujauzito na kufanya haya matukio kuwa negligible.......iko wapi mikakati kutoka ustawi wa jamii, elimu, mambo ya ndani nk kuhakikisha hawa mabinti wanakuwa salama katika kila nyanja kuanzia kitabia na kimaadili..?
Wenzio wanataka pesa toka World Bank. Hawana mipango ya kuumiza kichwa hivyo.

Team Omba Omba hawatakuelewa.
 
Hili ni Tangazo la watoto wa Vijijini na Maskini Wanaoamini kwenye kuwa na watoto wengi. Town huwezi kuona Mtoto wa shule ana mimba . Akiwa hana mtoto shule kwake ilikuwa ngumu, baada ya kuwa na mtoto atafaulu kweli? Ndio maana wakaweka na Sheria ya Kurudia Mitihani

Mdogo wangu akishika mimba na anasoma tutagawana Majengo ya Serikali. FULLSTOP!
Mjini watu wanatoa mimba kirahisi sana tofauti na kijijini.

Mjini mtoto akipata mimba anaweza asijulikane kwa upesi hadi anaitoa.

Kijijini akitema mate tu ya kuashiria mimba kijiji kizima kinajua. Ni aibu pia kuitoa bora azae tu.
 
Jengeni mabweni wanafunzi wote wa kike wakawe bweni, hakikisheni maji yanapatikana majumbani mwa watu, malizeni umaskini. Watoto wengi wanaopata mimba katika umri mdogo ni wa maskini.
Acheni ngonjera nyingi.
unajua hii concept wengi sana inawachanganya..

tumeruhusu wajawazito kurudi shule sawa inawezekana ni uamuzi mzuri, lakini je ni sawa kwa binti mdogo mwanafunzi kupewa ujauzito na kuzalishwa au kufanya ngono?..... hapa ndio kwenye concept na failure za wasomi wetu...

Juhudi gani kali tumefanya sasa kuwalinda hawa mabinti na ujauzito na kufanya haya matukio kuwa negligible.......iko wapi mikakati kutoka ustawi wa jamii, elimu, mambo ya ndani nk kuhakikisha hawa mabinti wanakuwa salama katika kila nyanja kuanzia kitabia na kimaadili..?
 
Upuuzi mtupu,
To hell na maadili yako.
Naziona shule za kanisa zinarudi kwenye ubora wake kana tegemeo pekee la kuzalisha watoto Wenye maadili na wanaozingatia shule tu Kama agenda kuu wakiwa shuleni

Shule za kanisa ndizo pekee zitakazomokoa mtoto na mmomonyoko wa maadili mtoto akiwa anasoma kuwa asiwaze kidume Wala kijike hata kiwe na pesa kuliko Bakhresa agenda kusoma tu Hadi kieleweke

Shule za kanisa jiandaeni kupokea mafuriko ya wanafunzi darasa la kwanza mwakani

Wazazi msiopenda vitoto vyenu kubeba mimba vikiwa shule vipelekeni shule za kanisa hizo zingine waachieni wazazi wapendao vitoto vyao ruksa kubeba mimba
 
Kwanini Zitto na Chadema walimshambulia Sana Hayati Dkt John Pombe Magufuli kwenye hili?View attachment 2022705

AFRICA KENYA : WANAFUNZI WAKIELEKEA CHUMBA MAALUMU CHA KUNYONYESHEA
View attachment 2022703
ULAYA : MWANAFUNZI AKINYONYESHA MTOTO KWENYE MAHAFALI BAADA YA KUSOMA AKIWA NA MTOTO,
Hiyo ni chuo hata kwetu ipo na wapo niliosoma nao na wakazaa huku wakiendelea na masomo. Lete ya shule ya msingi au sekondari ya huko unapopasifia, nikupe mali zangu zote ikiwemo za urithi...
 
Mjini watu wanatoa mimba kirahisi sana tofauti na kijijini.

Mjini mtoto akipata mimba anaweza asijulikane kwa upesi hadi anaitoa.

Kijijini akitema mate tu ya kuashiria mimba kijiji kizima kinajua. Ni aibu pia kuitoa bora azae tu.
Nimecheka sana kwa sauti allo,
 
Kwa hili namuunga mkono SSH, wapewe adhabu kali ikiwemo fine au kazi ngumu ila wasinyimwe haki ya kusoma.

However kma aliempa mimba ni under 18 basi miaka 30 iwe substituted na kifungo cha nje. Itakua win win situation.
Zitto nikupongeze pia kwa hili
 
Hiv unajua muandishi huna akili hata za kuombea maji hiko nyuma kabla ya hayati magufuli walikuwa wanaruhusiwa kusoma au mnapenda pesa watu wana ongoa point za msingi maisha yamekuwa ghari sana mfumuko wa bei uko juuuu ww unaongelea mimba khaaaa kweli NDIO MAAANA JUA KALI ACHA LIWAKE
 
Wewe jamaa bana. Anyway ni Mawazo Yako. Nakuuliza hivi.
Unajua matokeo ya hilo jambo?
Unaujua mfumo wa Dunia wa sasa na Uelekeo wake?

Acha kupenda kushabikia mambo usiyojua kwa undani.
 
Kizazi cha uzinifu kinahalalishwa halafu tunaomba MUNGU atupe Mvua, Umeme, Afya n.k labda kama ni miungu ya zamani hapo sawa
 
Wewe jamaa bana. Anyway ni Mawazo Yako. Nakuuliza hivi.
Unajua matokeo ya hilo jambo?
Unaujua mfumo wa Dunia wa sasa na Uelekeo wake?

Acha kupenda kushabikia mambo usiyojua kwa undani.
Hebu fafanua sasa,
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom