Dunia imesimama na Rais Samia Suluhu Hassan hoja ya Teenage Mothers

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
2,542
2,172
Kila mwaka zaidi ya wasichana 6,500 wa Kitanzania waliachishwa|walifukuzwa shule kwasababu ya kupata ujauzito wakiwa shuleni,

Mwaka 2017 aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt John John Joseph Pombe Magufuli kwa kutumia nguvu ya Rais alikataa watoto hawa kuendelea na masomo.

Benki ya Dunia ikatunyima fedha kiasi cha $300M karibu TZS 690BL baada ya kiongozi mkuu wa ACT-Wazalendo Mhe Zitto Zuberi Kabwe kuwataka wafanye hivyo,

Je kulikuwa na haja kwa Hayati Rais Magufuli kufanya hayo?
Sote tunafahamu,Mimba sio ugonjwa, Mimba sio kilema,Mimba sio laana ,Mimba ni dalili ya ukamilifu na utimilifu wa kizazi cha mwanamke.

Lakini pia, Mimba ni baraka ya Uzao toka kwa Mungu iweje iwe laana?

Kwamtazamo wangu,awamu zilizopita zilimchukulia Mwanafunzi aliyepata mimba akiwa shuleni kitofauti sana
1. Zilidhani kupata mimba shuleni ni laana toka kwa Mungu na Wanadamu,

2. Zikamwona kama ni mtoto asiyefaa tena kuishi duniani

3. Zikafikiri ni mtoto asiyetakiwa kupata elimu tena utadhani mimba inafuta kumbukumbu,

4. Zikamwona kama malaya na huenda akipewa nafasi nyingine ya kuendelea na masomo atasambaza tabia hiyo mbaya kwa wanafunzi wengine,

5. Ziliamini kabisa ni mtoto asiyevumilika tena katika kuendelea na masomo yake,

Zitto Kabwe na baadhi ya Wabunge wa CHADEMA kama Esther Matiko na Halima James Mdee pamoja na wanaharakati wengine nguli wa kimataifa kama Maria Tsesai Sarungi na Shangazi Fatuma Karume na wengime wengi,

Watu hawa Wote kwa pamoja, walimpinga Hayati Dkt John John Joseph Pombe Magufuli kwa nguvu na kwaakili zao zote,

Wakati huohuo wakiziandikia taasisi mbalimbali za kimataifa hasa UNESCO|SIDA|IMF|WB zisitishe misaada na mikopo ya masharti nafuu kwa Tanzania kwa kukiuka haki hii ya Watoto,

Kwanini tusimpongeza Rais Samia kwa hili
Leo kwa mara ya kwanza toka kwa Rais wa kwanza mwanamke anayetambua kwa mifano kuwa "Mimba si laana wala mimba sio kilema cha akili"

Rais Samia tayari amerejesha furaha iliyopotea kwa miongo mingi kwa waathirika hawa wa mimba za mashuleni,

Leo haijalishi mimba mwanafunzi kaipataje iwe ni kwakubakwa au kurubuniwa cha kwanza mtuhumiwa atakwenda jela miaka thelathini,

Kisha mwanafunzi huyu baada ya kujifungua mtoto atarejea Shuleni kuendelea na masomo kama kawaida,

Tunaposema Rais Samia ni mteule wa Mungu tunamaana hii kwani hakuna mtimilifu mbele zake,

Hebu chukua huu mfano
Martha Karua mwanasiasa nguli tena mwenye ushawishi mkubwa nchini Kenya,

Martha ndiye anayetarajiwa kuwa Mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais kwenye Uchaguzi Mkuu Ujao wa Kenya wa mapema 2022,

Ningumu kuamini ila mama huyu ni muhanga wa "Mimba za Shuleni " aliyepewa nafasi ya pili kuendelea na masomo yake,

Kwa msiofahamu,
Kenya imekuwa na ruhusu kwa Wale wanaopata mimba shuleni kurejea na kuendelea na masomo yao baada ya kujifungua,

Nakwamantiki hii,Huenda Kenya ikapata Makamu wa Rais aliyepewa mimba akiwa bado shuleni,

Tunamengi ya kujifunza ila kwa sasa pongezi nyingi zimfikie Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutambua kuwa mimba sio laana bali ni baraka toka kwa Mungu.
 

Attachments

  • waraka wa kuwarudisha wanafunzi waliopata mimba shuleni.pdf
    1.5 MB · Views: 25

Tanzania to allow students to attend school after giving birth​

===
Government reverses controversial 2017 policy instituted by the country’s late leader, John Magufuli.

RTXJE6D5-1.jpg

Samia Suluhu Hassan has sought to break away from some of Magufuli's policies [Hannah McKay/Reuters]
Published On 24 Nov 2021


The Tanzanian government has said it will allow teenage mothers to continue with their studies after giving birth, reversing a heavily criticised policy implemented by late former President John Magufuli.

Human rights campaigners accused Tanzania of discrimination after Magufuli in 2017 endorsed the expulsion of pregnant girls from state schools and their prevention from returning to class after giving birth – a policy dating back to 1961.

Unaweza kusoma hapa pia​

In Tanzania, Gurnah’s Nobel Prize win sparks both joy and debate

Tanzania main opposition party says several members arrested

Tanzania secures nearly $600M from IMF for COVID relief


Following Magufuli’s death earlier this year, his successor Samia Suluhu Hassan has sought to break away from some of his policies.

On Wednesday, Education Minister Joyce Ndalichako said that “pregnant school girls will be allowed to continue with formal education after delivery”.

“I will issue a circular later today. No time to wait,” she said at a ceremony in the capital, Dodoma.

Magufuli had pledged that no student who became pregnant would finish their studies under his watch, saying it was immoral for young girls to be sexually active.

“I give money for a student to study for free. And then, she gets pregnant, gives birth and after that, returns to school. No, not under my mandate,” he said in mid-2017.

Tanzania's teenage mums: Government bans mothers from school

The decision was widely criticised by human rights groups and international donors, who cut their funding to the country in response to Magufuli’s policies.

At the time, Human Rights Watch (HRW) published a report saying school officials in Tanzania were conducting pregnancy tests in order to expel pregnant students, depriving them of their right to an education.

World Bank froze a $300m loan for girls’ education in protest against the ban. According to the institution, more than 120,000 girls drop out of school annually in Tanzania, 6,500 of whom were due to pregnancy or having children.

“This important decision underscores the country’s commitment to support girls and young women and improve their chances at receiving a better education,” the World Bank said in a statement later on Wednesday.

Sweden, which also cut its funding to Tanzania last year citing shrinking freedoms, hailed the move.

“This is a welcome step for many girls, allowing them to unlock their full potential,” the Swedish embassy in Dar es Salaam said on Twitter.

Opposition party Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo) said their push to reverse the policy had paid off.

“We did it! A clear example of one struggle, many fronts. Everyone who was involved did something towards this achievement,” said ACT Wazalendo leader Zitto Kabwe.

Magufuli, a COVID-sceptic, died of a heart condition on March 17 after a mysterious three-week absence. His political opponents insisted he had coronavirus.

In the weeks after her swearing-in, his successor Hassan reached out to Tanzania’s political opposition, promising to defend democracy and basic freedoms, and reopening banned media outlets.

But hopes that Hassan would usher in a new era were dented by the arrest of a high-profile opposition leader on terror charges and a crackdown on independent newspapers.

SOURC: Aljazira

>>>fungua hapa >>>>


#Tanzania nakupenda sana
 
Unajua hii concept wengi sana inawachanganya.

Tumeruhusu wajawazito kurudi shule sawa inawezekana ni uamuzi mzuri, lakini je ni sawa kwa binti mdogo mwanafunzi kupewa ujauzito na kuzalishwa au kufanya ngono? Hapa ndio kwenye concept na failure za wasomi wetu.

Juhudi gani kali tumefanya sasa kuwalinda hawa mabinti na ujauzito na kufanya haya matukio kuwa negligible, iko wapi mikakati kutoka ustawi wa jamii, elimu, mambo ya ndani nk kuhakikisha hawa mabinti wanakuwa salama katika kila nyanja kuanzia kitabia na kimaadili?
 
Mimba sio ugonjwa, Mimba sio kilema,Mimba sio laana ,Mimba ni dalili ya ukamilifu na utimilifu wa kizazi cha mwanamke

Mimba ni baraka ya Uzao toka kwa Mungu "walisikika wanaharakati wakimzonga Hayati Dkt John John Joseph Pombe Magufuli.
Hizo mimba wakipew na walimu wao kwa "excuse" zinazoletwa hapo tegemeeni lolote
 
Naziona shule za kanisa zinarudi kwenye ubora wake kana tegemeo pekee la kuzalisha watoto Wenye maadili na wanaozingatia shule tu Kama agenda kuu wakiwa shuleni

Shule za kanisa ndizo pekee zitakazomokoa mtoto na mmomonyoko wa maadili mtoto akiwa anasoma kuwa asiwaze kidume Wala kijike hata kiwe na pesa kuliko Bakhresa agenda kusoma tu Hadi kieleweke

Shule za kanisa jiandaeni kupokea mafuriko ya wanafunzi darasa la kwanza mwakani

Wazazi msiopenda vitoto vyenu kubeba mimba vikiwa shule vipelekeni shule za kanisa hizo zingine waachieni wazazi wapendao vitoto vyao ruksa kubeba mimba
 
Mimba sio ugonjwa, Mimba sio kilema,Mimba sio laana ,Mimba ni dalili ya ukamilifu na utimilifu wa kizazi cha mwanamke

Mimba ni baraka ya Uzao toka kwa Mungu "walisikika wanaharakati wakimzonga Hayati Dkt John John Joseph Pombe Maguful.
Zidumu saaana fikra na tamaduni za weupeeee. Ila umasikini na ulaaniwe kabisaaaa. Sijui kwa nini sisi Mungu aliona tuwe masikini wa kila kituuu?
 
Back
Top Bottom