Ni wasaidizi gani IKULU wanaosababisha Rais Kikwete aonekane kituko katika jamii?

Rutunga M

JF-Expert Member
Mar 16, 2009
1,769
1,382
Kuna matukio mengi sana yanayofanywa na Rais na baadaye kubanika amekosea na inaelezwa kuwa kuna baadhi ya wasaidizi wake pale ikulu wanamfanya Rais wetu aonekane kituko na pengine kutoa matamshi ambayo baadaye inabanika ni uongo mtupu.

Mfano ni suala la TUCTA ambapo inaelezwa kuwa alitoa taarifa ya uongo wakati akiongea na wazee na sasa imebanika kuwa alipotoshwa na wasaidizi wake.

Aidha, hali ngumu ya maisha, hali ya umeme ya sasa n.k vinachangia taifa liendelee kukosa imani na rais.

Ningependa tuwajue wale wanaofanya RAIS wetu awe anakosea kila siku, tujadili uwezo wao nk

Mimi naanza kutaja
1:Salva Rweyemamu
2.........
Endelea kutaja
 
Katika hili utamuonea Salva, hili ni Kapuya na Hawa Ghasia. Lakini pia ulofa wa mkulu mwenyewe, amekuwa mvivu wa kufikiri na ametanguliza hamu ya madaraka.
 
Kila nionapo jina la Salva nakumbuka kampeni ndani ya CCM 2005, huyo alikuwa ni nyoka wa mdimu kajisemea kaka Mdhihir alikuwa anang'ata anakumaliza halafu hakuli yeye anaendelea zake kuuwa tu, waulizeni akina Mwandosya, Salim Ahmed, Sumaye, Tingatinga wanamjua ubaya wake na naamini hajaacha bado ana sumu ileile tena sasa ndio imekomaa kwani anao ukaribu wa kujua nyeti za taifa na anajua jinsi gani amdanganye JK kwani anamjua kuwa ktk mambo mengi huwaga hachanganyi na za kwake
 
Msisahau huko Hekaluni Magogoni kuna first lady. Salma ni miongoni mwa washauri waandamizi wa Jk.
 
The bucks stops with him,akichanganya na zake na matokeo ndo haya basi si washahuri wa kulaumu bali yeye mwenyewe,kwani yeye alimlaumu mgaya ama hao aliodai wanamshauri?
 
jk,salva,salma,jabir,na wale walioingizwa ikulu kwa maslahi ya jk..............
 
Bad news,hili swala JK angewaachia mawaziri husika walizungumzie,sasa amekwea treni kwa mbele tunaanza kuwatafuta wasaidizi wake,ingekuwa enzi za Mkapa or Mwalimu, waziri tu angetosha kulisimamia na kulizungumzia.
Manegment stlye ya JaaKaya ipo ki mujini mujini zaidi,watoto wa mjini wanaiita sha'sha. matokeo yake zikija lawama wanatafutwa wasaidizi wake.
kama msemaji wa awali,the Buck Stops on JK 's shoes, amedanganywa or hajadanganywa,ikibainika kuwa alituhubiria habari zisizo na ukweli,basi awatake Radhi viongozi wa TUGHE via the same media,na muda uwe ule ule wa jioni,na vipindi virushwe na TBC mara nyingi kama awali walivyofanya,
ila Salva mnamuonea bure tu,
na mama Salma msimweke ktk list kwani yeye hawajibiki/hana uongozi wowote ktk jamhuri ya Tz.
hapa ni Katibu mkuu wa wizara husika na waziri wake,kwani wao ndio waliotoa taarifa kwenda ikulu ,na Mh Raisi akaamini alichopatiwa mezani kwake na viongozi wa wizara husika.
 
Kwani mshauri wake mkuu katika masuala ya ajira na wafanyakazi ni nani? Kama kuna lawama huyo ndio azibebe!
 
Tatizo ni kuwa kajaza rafiki zake tu pale ikulu na ndio hao wanaomuangusha!
 
Salva Rweyemamu inawezekana ana madhambi yake lakini kumtaja hapa kwenye hili ni Kumuonea. Role ya director wa mawasiliano ni kutoa taarifa walizonazo. Usahihi na upungufu wa hizo taarifa haimaniishi kuwa aliyetoa ana mapungufu. Kuna watu wa tawkimu, sera na uhahasibu, na wengine wengi tu wale hasa wanao process hizi taarifa ikiwemo na yeye mwenyewe JK ndo wanamatatizo.
 
Jamaa wala asisingizie wasaidizi wake IQ yake naona iko chini jamani. Part kubwa ya brain haijaelekezwa kwenye kazi za uongozi.
huyu ni kumtoa madarakani tu na sio mtu wa kumdiscuss sana. Maana ni mzuri sana JK wa kulipa fadhira na kulipa visasi nadhani wengi mnamua. Yaani kama alikujua kabla ya u-president we umekula bingo na kama mlikuwa na bifu umelia .
 
Nadhani huyu jamaa anayeitwa J K
Kwanini asisiskilize kotekote ndo atoe Tamko
Malawama yooooooooote kwake yeye ndo kiini cha kila uchafu unaoendelea katika himaya yake
 
Salva Rweyemamu inawezekana ana madhambi yake lakini kumtaja hapa kwenye hili ni Kumuonea. Role ya director wa mawasiliano ni kutoa taarifa walizonazo. Usahihi na upungufu wa hizo taarifa haimaniishi kuwa aliyetoa ana mapungufu. Kuna watu wa tawkimu, sera na uhahasibu, na wengine wengi tu wale hasa wanao process hizi taarifa ikiwemo na yeye mwenyewe JK ndo wanamatatizo.
Hata yeye anahusika ina maana yeye ni kama loud spika wa ikulu anacholetewa anapayuka tu bila kuuliza au kutumia akili kwa hiyo akiambiwa atangaze rais kapinduliwa atatangaza kama hivyo basi hafai kuwa director wa mawasiliano wa ikulu.
 
Hata yeye anahusika ina maana yeye ni kama loud spika wa ikulu anacholetewa anapayuka tu bila kuuliza au kutumia akili kwa hiyo akiambiwa atangaze rais kapinduliwa atatangaza kama hivyo basi hafai kuwa director wa mawasiliano wa ikulu.


Kuna Mtu mmoja anaitwa YUSUPH MAKAMBA,ambaye ni katibu wa chama twawala,nadhani anatoa ushauri mbaya kwa MWENYEKITI wake wa hiki chama kuhusu namna chma kinavyopasawa kuendesha nchi
 
Back
Top Bottom