NgugiAchebe
JF-Expert Member
- Jul 11, 2016
- 1,024
- 688
CHADEMA INA MANAIBU KATIBU WAKUU (BARA) WAWILI??
Na Charles Francis M,
Nianze kwa kusema, uchambuzi huu ni huru kabisa. Sijafanya uchambuzi huu kama mwana chama wa chama chochote cha siasa nchini. Narudia tena, sijafanya uchambuzi huu kama mwana chama wa chama chochote cha siasa maana ni kawaida ya “watu wenye matatizo ya kufikiri vizuri” kwamba kila wakati lazima ufanye uchambuzi kama mwana chama wa chama cha siasa, huo ujinga ufe!! Ukiona huwezi kuvumilia, puuzia au pita kimya kimya au ni-block. Tuendelee na mjadala wa msingi.....
Ni kanuni na taratibu kwa vyama vya siasa nchini kuwa na uwakilishi kutoka pande zote za muungano. Hii ni kwa lengo zuri la kudumisha muungano na ushirikiano lakini pia kukidhi matakwa ya kisheria. Kwa mujibu wa sheria za nchi, sheria ya vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992 kifungu cha 7, kinatambua chama cha siasa ili kisajiliwe ni lazima kiwe pande zote za muungano. Pamoja na sheria hizo, vyama husika ili kujiimarisha ni muhimu sana kuwa na nguvu pande zote za muungano. Kuna nadharia kuwa chama kikiwa na nguvu upande mmoja kinaweza kupata shida ya kiutawala baadae na hasa migogoro.
Chama cha demokrasia na Maendeleo (Chadema) kina manaibu katibu wakuu wawili?? Mjadala huu mpana naufungulia hapa. John Dalali Mnyika ni naibu katibu mkuu wa Chadema bara na pia ni mbunge wa jimbo la Kibamba kupitia chama hicho. Salum Mwalim ni naibu katibu mkuu Zanzibar wa chama hicho lakini amekuwa akifanya “shughuli nyingi za kichama bara”. Tarehe 30/08/2014 siku ya jumamosi mchana, Salum Mwalim alirudisha fomu ya kugombea ujumbe wa kamati kuu kupitia Zanzibar.
Kiongozi huyu mwenye taaluma ya habari ambaye pia amewahi kuwa meneja wa uhusiano wa nje wa “kampuni ya Vodacom” ambayo hivi karibuni ilikubali kutoa ushahidi dhidi ya kesi inayo mkabili mbunge wa Arusha mjini (Chadema) ndugu Godbless Jonathan Lema. Tarehe tajwa hapo juu, Salum Mwalim alinukuliwa akisema yupo tayari kubadili upepo wa kisiasa Zanzibar kwa maana ya kuipaisha bendera ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), yaani kwa tafsiri nyingine yuko tayari kukijenga chama hicho Zanzibar. Kwa sasa Salum Mwalim ni naibu katibu mkuu wa Chadema Zanzibar (siyo bara).
Kuna maswali mengi ambayo yanakosa majibu ya msingi, kwa mfano; kwanini kiongozi huyu amekuwa na ziara nyingi Tanzania Bara?? Anatumia fedha za chama ambazo ni ruzuku?? Kama anatumia ruzuku ya chama, je fedha hiyo ya ruzuku kwa nafasi ya naibu katibu mkuu Zanzibar inatumika wapi?? Yamkini tungesema ni aina mpya ya uongozi kama John Mnyika naye angekuwa na ziara nyingi Zanzibar, lakini sivyo!! Chadema Zanzibar kuna nini?? Je, Chadema Zanzibar iko chini ya nani?? Ni kwamba “Zanzibar ilitumika” kama sehemu tu ya kupata usajili wa chama ili chama kionekane kipo pande zote za muungano?? Je, ni kweli kwamba kiongozi huyu hakubaliki Zanzibar?? Je, ni makubaliano ya UKAWA kwamba Chadema iiache Zanzibar mikononi mwa CUF pekee??
Utendaji kazi wa Salum Mwalim Tanzania bara unazua mjadala mpana sasa. Ni kwa nadra sana kusikia naibu katibu mkuu wa Chadema bara ndugu John Mnyika akifanya ziara za kichama Zanzibar. Ni kweli Chadema haina mvuto Zanzibar?? Katika maswali yote ndani ya mjadala huu lazima kuna swali lina ukweli. Iko wapi ahadi ya Salum Mwalim kuipeperusha bendera ya Chadema Zanzibar?? Wapo wanao amini kwamba ujio wa Salum Mwalim Tanzania bara ni kuziba pengo la naibu katibu mkuu bara, John John Mnyika ambaye tangu ujio wa Lowassa amekuwa kimya sana ndani ya chama hicho.
Katika muktadha huu swali hili linaibuka; Chadema ina manaibu katibu wakuu bara wawili?? Umuhimu wa kuwa na naibu katibu mkuu Zaznibar uko wapi?? Ripoti ya utendaji kazi ya naibu katibu mkuu Zanzibar ina andikwa vipi ikiwa anawajibika sana bara?? Ni vema sasa Chadema ikatafakari umhimu wa kuwa na naibu katibu mkuu huyu wa upande wa Zanzibar. Ni ngumu sana kusikia viongozi wa vyama vingine vya siasa upande wa Zanzibar kuja Tanzania bara na “kupiga kambi” kwa lengo la kujenga chama wakati nafasi na majukumu yao walitakiwa “kupiga kambi zaidi” katika eneo moja la muungano yaani Zanzibar.
Karibuni sana kwa mjadala.
“Caytano Maytano”
Charles Francis M.