Ni wapi nitapata mwanamke wa kuoa?

Gudboy

JF-Expert Member
Aug 14, 2009
867
77
Jamani wandugu, heshima zenyu bana.

Mimi ni kijana mwenye maisha na kipato cha kawaida, naona umri unasonga kwa kasi ya ajabu, na hivyo kuifanya nafsi yangu inishawishi ya kwamba wakati wa kuoa umefika. Na kweli hata mimi mwenyewe nimegundua kuwa kumbe ni kweli wakati wa mimi kuwa na mwenza ni huu.

Maana jinsi ninavyoyaona haya maisha ni kama routine vile, hakuna cha zaidi kitakachonifanya nizidi kuchelewa kutafuta mwenza wa kuishi nae, zaidi ya yale yale ya kila siku (mfani, kwenda kazini, kurudi home, kula kwa mama lishe, week end kwenda kutembea na shughuli za hapa na pale kwa ajili ya kujiletea maendeleo).

Kutokana na haya yote naona nimebakisha mambo ya muhimu mawili tu katika maisha ya hapa ulimwengu nayo ni KUOA NA KUFA. Sasa kabla hili la kifo halija overtake hili la ndoa ndio nimeona ya kwamba wakati umefika ili nikamilishe maisha kamili.

Sasa huwa najiluliza je ni wapi naweza kupata mwanamke ambaye atakuja kuwa mke wangu? Nahitaji kuoa kwa nguvu zote bila ya kuchelewa au kupoteza muda. Wandugu je ni sehemu zipi naweza pata mke ambaye atakuwa na busara zote?

Nawasilisha
 
mwana naona kaa vile unakuwa na haraka kidogo...sasa hapa ndipo utakapojikuta unakosea katika uchaguzi wako....
 
La kwanza je umeshatambua ni mwanamke wa aina gani unahitaji?wa sifa zipi? then mshirikishe mungu ili aweze kukukutanisha na aliyemuumba kwa ajili yako,Unaweza kumpata popote pale mungu atakapopenda awakutanishe, yaweza kuwa Maeneo yako ya kazi, humu mmu,kanisani,barabarani,unaweza waomba wazee wakutafutie kijijin kwenu km unataka wa kutoka kijini,kwenye daladala n.k.hiyo ni kwa upeo wangu,subiri wengine watakushauri vp!
 
Kwani wewe una umri gani Gudboy?
Ni pm nikuambie pakumpata!

Jamani wandugu, heshima zenyu bana.

Mimi ni kijana mwenye maisha na kipato cha kawaida, naona umri unasonga kwa kasi ya ajabu, na hivyo kuifanya nafsi yangu inishawishi ya kwamba wakati wa kuoa umefika. Na kweli hata mimi mwenyewe nimegundua kuwa kumbe ni kweli wakati wa mimi kuwa na mwenza ni huu. Maana jinsi ninavyoyaona haya maisha ni kama routine vile, hakuna cha zaidi kitakachonifanya nizidi kuchelewa kutafuta mwenza wa kuishi nae, zaidi ya yale yale ya kila siku (mfani, kwenda kazini, kurudi home, kula kwa mama lishe, week end kwenda kutembea na shughuli za hapa na pale kwa ajili ya kujiletea maendeleo). kutokana na haya yote naona nimebakisha mambo ya muhimu mawili tu katika maisha ya hapa ulimwengu nayo ni KUOA NA KUFA. Sasa kabla hili la kifo halijaovertake hili la ndoa ndio nimeona ya kwamba wakati umefika ili nikamilishe maisha kamili. Sasa huwa najiluliza je ni wapi naweza kupata mwanamke ambaye atakuja kuwa mke wangu? nahitaji kuoa kwa nguvu zote bila ya kuchelewa au kupoteza muda. Wandugu je ni sehemu zipi naweza pata mke ambaye atakuwa na busara zote?

Nwasilisha
 
mwana naona kaa vile unakuwa na haraka kidogo...sasa hapa ndipo utakapojikuta unakosea katika uchaguzi wako....
mkuu inawezekana ikawa ni kweli kabisa hapo penye nyekundu, lakini kulikua na kipindi nikiambiwa swala la kuoa nakua mkali na sitaki kabisa kusikia habari hizo, lakini mwaka huu naona nafsi yangu yenyewe bila ya kushurutishwa na yeyote, inahitaji kuwa na mke, sasa ili nisikurupuke natakiwa kusubiri kwa muda gani? Maana wakati mwingine kuoa ni kama bahati nasibu, mathalani mwenzako anaweza akakurupuka na kuoa na maisha yakawa shwari, lakini wewe unayesubiri, miezi sita tu ndoa chaliiiii
 
Kweli swali gumu ila mke unaweza kumpata popote kwenye
daladala
kanisani
kazini
mtaami
chuo
harusi
au sherehe yeyote
club
msibani
anywhere mkuu endelea kusearch hata humu jf
 
La kwanza je umeshatambua ni mwanamke wa aina gani unahitaji?wa sifa zipi? then mshirikishe mungu ili aweze kukukutanisha na aliyemuumba kwa ajili yako,Unaweza kumpata popote pale mungu atakapopenda awakutanishe, yaweza kuwa Maeneo yako ya kazi, humu mmu,kanisani,barabarani,unaweza waomba wazee wakutafutie kijijin kwenu km unataka wa kutoka kijini,kwenye daladala n.k.hiyo ni kwa upeo wangu,subiri wengine watakushauri vp!
napenda nitoe shukrani zangu za dhati kwa ushauri wako mzuri, kwa kweli vigezi vya nimtakaye ninavyo, lakini wengi ninao kutana nao hawajatimiza hata robo yake. Naweza nikaa na mtu tukapiga story lakini nikimuuliza maswali ili kumjua, navunjika moyo kwa kuwa hana ninachohitaji
 
Kaka muombe mungu, hilo ndo swali kubwa kuliko yote linasumbua sana vijana wa kiume kila mtu anajiuliza "HATA NIKITAKA KUOA NITAMUOA NANI? tunakuwa kwenye mahusiano mara nyingi lakini ukifikiria kumuhalalisha uliye nae roho inasita maana NDOA NI ZAIDI YA KULALA PAMOJA
 
Jamani wandugu, heshima zenyu bana.

Mimi ni kijana mwenye maisha na kipato cha kawaida, naona umri unasonga kwa kasi ya ajabu, na hivyo kuifanya nafsi yangu inishawishi ya kwamba wakati wa kuoa umefika. Na kweli hata mimi mwenyewe nimegundua kuwa kumbe ni kweli wakati wa mimi kuwa na mwenza ni huu. Maana jinsi ninavyoyaona haya maisha ni kama routine vile, hakuna cha zaidi kitakachonifanya nizidi kuchelewa kutafuta mwenza wa kuishi nae, zaidi ya yale yale ya kila siku (mfani, kwenda kazini, kurudi home, kula kwa mama lishe, week end kwenda kutembea na shughuli za hapa na pale kwa ajili ya kujiletea maendeleo). kutokana na haya yote naona nimebakisha mambo ya muhimu mawili tu katika maisha ya hapa ulimwengu nayo ni KUOA NA KUFA. Sasa kabla hili la kifo halijaovertake hili la ndoa ndio nimeona ya kwamba wakati umefika ili nikamilishe maisha kamili. Sasa huwa najiluliza je ni wapi naweza kupata mwanamke ambaye atakuja kuwa mke wangu? nahitaji kuoa kwa nguvu zote bila ya kuchelewa au kupoteza muda. Wandugu je ni sehemu zipi naweza pata mke ambaye atakuwa na busara zote?

Nwasilisha

Kamanda umeadimika kweli ndo mambo ya kusaka jiko nini?
Nakushauri ukamate Mwalimu wa shule ya Msingi au wa O'Level
 
Kweli swali gumu ila mke unaweza kumpata popote kwenye
daladala
kanisani
kazini
mtaami
chuo
harusi
au sherehe yeyote
club
msibani
anywhere mkuu endelea kusearch hata humu jf
nashukuru sana, lakini je nawezaje kumtambua kuwa ndie sahihi? Na pia natakiwa nimchunguze kwa muda gani, mathalani ndio nimempata?
 
Kweli swali gumu ila mke unaweza kumpata popote kwenye
daladala
kanisani
kazini
mtaami
chuo
harusi
au sherehe yeyote
club
msibani
anywhere mkuu endelea kusearch hata humu jf

Umesahau bebii kuweka Bar vp tena jamani?
 
Pole Gudboy. Mi nishakuelewa vigezo unavyovitaka.
Wanawake wenye vigezo hivyo wako wachache sana. Ndiyo maana nakuambia ni PM acha ubishi mi najua wanakopatikana. Loh!

napenda nitoe shukrani zangu za dhati kwa ushauri wako mzuri, kwa kweli vigezi vya nimtakaye ninavyo, lakini wengi ninao kutana nao hawajatimiza hata robo yake. Naweza nikaa na mtu tukapiga story lakini nikimuuliza maswali ili kumjua, navunjika moyo kwa kuwa hana ninachohitaji
 
Kamanda umeadimika kweli ndo mambo ya kusaka jiko nini?
Nakushauri ukamate Mwalimu wa shule ya Msingi au wa O'Level
Ni kweli mkuu, nilikua kimya mana hata simu nilipoteza, ila bila shaka yangu unayo, kama vp tufanye mawasiliano basi. Nimechoka maisha ya ukapera kaka, unaonaje kama nikirudi kule Tanga kaka?
 
Kaka muombe mungu, hilo ndo swali kubwa kuliko yote linasumbua sana vijana wa kiume kila mtu anajiuliza "HATA NIKITAKA KUOA NITAMUOA NANI? tunakuwa kwenye mahusiano mara nyingi lakini ukifikiria kumuhalalisha uliye nae roho inasita maana NDOA NI ZAIDI YA KULALA PAMOJA
ni kweli kaka, hili jambo kwa vijana wa sasa ni gumu mno. huwa nawaambia watu sisi ambao bado hatujaoa tuna maisha magumu sana, lakini ukiangalia ni kweli, kumpata tu wa kuoa ni shughuli pevu
 
popote tu pale we kua mtu wa kujichanganya tu utawapata..................huh
Na hili ndio tatizo langu kubwa mkuu, mana nakua tight kiasi kwamba muda wa misele ya mara kwa mara sina, hata kwenye harusi nahudhuria chache sana. Na mara nyingi nakuwa safarini, hata kwenye usafiri kama sijakaa na mama mtu mzima basi ni mwanaume (hadi huwa naona sina bahati kabisa
 
Pole Gudboy. Mi nishakuelewa vigezo unavyovitaka.
Wanawake wenye vigezo hivyo wako wachache sana. Ndiyo maana nakuambia ni PM acha ubishi mi najua wanakopatikana. Loh!
cheki kwa inbox yako mkuu
 
Back
Top Bottom