Ni wapi mtoto atapata elimu bora zaidi ya Tanzania katika nchi ya Kenya?

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,520
Habari wadau,

Nina mwanangu yupo darasa la 3 shule zetu hizi za kisasa, English medium za kati.

Nimepata wazo la kumuhamishia Kenya. Kumtafutia shule nje ya nchi ni ili apate elimu itakayomuwezesha kujikomboa.

English Medium za Tanzania hizi naona kama zimekuwa magumashi sana. Ada inapanda bila sababu za msingi, walimu wenyewe wanaofundisha watoto English hawaijui hiyo English, hivyo hata masomo mengine kama science, mathematics wanafundisha hovyo hovyo,, na mtoto akirudi mtaani anacheza na wenzake au anaongea Kiswahili muda wote na dada.

Kuna mtu kaniambia syllabus ya Primary School ya Kenya ndiyo the best in East Africa kwa content nzuri. Mtoto aliemaliza elimu ya msingi Kenya ana uwezo wa kufanya mtihani wa form 4 na bado asipate div 0, sababu syllabus ya Kenya ina-cover vitu vingi katika primary school stage.

Kwa wenye experience naombeni ushauri. Taratibu za Mtanzania kusoma shule za Kenya ukoje, maisha ya boarding schools za Kenya yakoje kwa mtoto mdogo na shule zipi ni nzuri huko Kenya na zenye gharama nafuu mtu mwenye kipato cha kati anamudu.

Nimeamua kumpora mwanangu haki yake ya kuishi na mimi mwaka mzima kila siku kwa ajili ya future yake kuwa nzuri maana elimu yetu haieleweki na bongo shule zinazotoa elimu nzuri ni chache na ada zake ni kubwa sana na sana. Nimewaza akapate sylabus yenye content nzuri Kenya elimu ya msingi halafu sekondari ndiyo asome Tanzania.
 
Mpeleke Kenya.

Kama una pesa msomeshe Tanzania, Cambridge Curriculum
 
Mimi pia nimewaza kama wewe, ila nilichelewa kuamua hivyo nafikiri sekondari ndio wanangu wakasome Kenya kwa jirani zetu. Ngoja tupate maelezo ya wazoefu ila asije MK254 akaanza kunanga elimu yetu magumashi.
 
Inaonekana wewe uko interested sana na mtoto wako kujua Kiingereza na sio elimu bora, hiyo hela ya kumpeleka mtoto Kenya si bora ungemlipa Ras Simba amfundishe mwanao Kiingereza kilichotulia kwa muda mfupi huku akiendelea kupata elimu ya Kibongo ambayo haiko chini hivyo unavyodhania.
 
Naishi Kenya. Sijui kwanini Wabongo tunapenda kusifia mfumo wa elimu yao. Me naona ni wa kawaida tu, labda sababu wanatumia English as a teaching language, hata wenye uwezo huku wanapeleka watoto watoto Cambridge, meaning wao wenyewe hawatrust system yao.

Tafuta shule bora hukohuko sababu hizo gharama za ada na boarding school nazo heri umpeleke shule bora za huko. Na huyo mtoto bado ni mdogo sana kukaa mbali hivyo na wazazi.

Na pia tujue kujua English sio kuwa na akili coz naona hapo unasema hajui English anaongea Kiswahili. Hiyo ndiyo shida yetu Wabongo, yaani Mtoto akiongea English tunamwona bright wakati hesabu ana-fail.

Kuna watoto ukiwaweka wa kayumba na hizo English medium the only thing wa English medium atamshinda Ni kuongea English vingine vyote anaburuzwa. English ni lugha tu japokuwa kwa ulimwengu wa sasa ni muhimu kujua lakini siyo kipimo cha akili nyingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kweli mimi nilisomesha watoto english medium, Uganda n.k na boarding na sasa wamemaliza vyuo nilichojifunza watoto wana mapungufu mengi, mbaya tayari sasa ni watu wazima.

Kwa ushauri wangu, ukiweza kuhamia palipo na shule nzr km wahindi wanavyofanya lakini mtoto anatoka nyumbani na kurudi SIO boarding BORA SANA. Usipoweza hilo tafuta shule NZURI jirani au bora upate jamaa aishinae NYUMBANI.
 
Frankly speaking,

Kwenye masuala ya elimu na English medium Kenya wametutangulia sana.

Ndio kusema hata shule za Tanzania za english medium zilizoanzishwa mwanzo mwanzo waalimu walitokea huko.

Kwa shule zilizo nyingi hapa kwetu utakachokiona ni “inflated” school fees ila ubora wa elimu wanayotoa sio kivile. Chache ambazo ziko vizuri ndio zile ada mkasi.

Cha kufanya: Kama mtoto ana umri wa kujitambua chagua shule moja nzuri kwa watani jirani hutajuta mpeleke, ila ufuatilie maendeleo yake kwa karibu.

Mimi ni mzazi na mtaalamu wa mambo ya elimu mchango wangu hauko biased.
 
Zipo shule nzuri Tanzania na kwa umri wa mtoto sio vyema akaenda kusoma nje katika umri huo...bahati mbaya sana watanzania wengi hatujui kutofautisha mitaala inayotolewa shule zilizopo TZ. WENGI TUNAWAPELEKA WATOTO ENGLISH MEDIUM TUNASEMA WAPO INTERNATIONAL SCHOOL.

Ipo hivi: watu wanafanya NECTA kwenye hizi English medium schools zilizopo Tz , lakini kuna mitaala kama ISEB moja ya mitaala bora kabisa inayofanya mtoto awe well equiped na inafundishwa kwenye International schools zilizopo Bongo.Ipo mitaala mingi inatolewa na International school though ipo mingine haimjengi mtoto mtanzania.

Kwahiyo kwanza tutofautishe English Medium na International School lakini pia tuzijue hizo shule zinatumia Mtaala upi kufundishia na je huo mtaala unalenga kumuandaa mtoto awe nani. Mwisho katika umri wa mtoto akiwa shule ya msingi anahitaji kulelewa na wewe mzazi, aende shule jioni arudi vinginevyo utakuja kujuta baadaye.
 
Watoto wengi wanaosoma Kenya huwa na tabia flani hivi za ajabu ajabu, wanakuwa wahuni

Hii ni kwa watu ninao wafahamu waliosoma na waliosomesha watoto Kenya. Fuatilia utagundua.

Tafuta shule nzuri hapahapa Tanzania ya day na ufuatilie maendeleo ya watoto kila siku.

Usikimbie majukumu yako mkuu.
 
Mh.. Utakua hujapata shule nzuri tu! Kuna shule nyingi tu Tanzania nzuri hata kwa upande wa lugha, hata ukiobserve utagundua siku hizi watoto wanaoongea English nzuri ni wengi!

Kumsaidia mtoto nyumban ongea naye kingereza wewe mwenyewe kama hamna mwingine wa kuongea naye.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama una HELA ya kumpeleka mtoto Kenya ni bora umpeleke hapa hapa Bongo, kuna shule nzuri na mwanao atajifunza sio tu English bali atapata elimu bora zaidi ya English. IST, Feza, DIS, HOPAC, Braeburn International, Al Muntazir, Dar International Academy, ni baadhi ya shule bora kabisa Dar Es Salaam. Pia fanya ufanyalo mtoto wako wa darasa la tatu ni vema ukakaa naye kwanza wewe mwenyewe hadi umri wake utakapozogea zaidi. Ni hatari sana kwa mtoto wa umri mdogo kama huo kuwa mbali na malezi ya wazazi wake kwa muda mrefu kiasi hicho. Hili ni kosa ambalo athari zake wengi wanakuja kuziona baadaye sana. Labda umpeleke Kenya kwa kiwango cha Chuo Kikuu atakuwa ameshakua na ameshakomaa kuliko sasa.
 
Frankly speaking,

Kwenye masuala ya elimu na English medium Kenya wametutangulia sana.

Ndio kusema hata shule za Tanzania za english medium zilizoanzishwa mwanzo mwanzo waalimu walitokea huko.

Kwa shule zilizo nyingi hapa kwetu utakachokiona ni “inflated” school fees ila ubora wa elimu wanayotoa sio kivile. Chache ambazo ziko vizuri ndio zile ada mkasi.

Cha kufanya: Kama mtoto ana umri wa kujitambua chagua shule moja nzuri kwa watani jirani hutajuta mpeleke, ila ufuatilie maendeleo yake kwa karibu.

Mimi ni mzazi na mtaalamu wa mambo ya elimu mchango wangu hauko biased.
Kenya unafata English Medium ? jwhat is English Medium ? come on English medium zipo bongo chungu mbovu na walimu ni hao wa Kenya na waganda ,,,Tuzungumzie mtaala wa Elimu sio Medium of instruction ya elimu....jamani tusichanganye mambo hapa,karne hii unampeleka mtoto Kenya kufuata English Medium came on ,zamani hapakuwa na English Medium Bongo kabla St marrys hazijaja tena kwa ushamba wetu tuliziita International school na wala hazikuua international ila ni sababu tunachanganya kati ya Lugha ya kufundishia na mtaala wa Elimu...TUSICHANGANYE HIVI NI VITU VIWILI TOFAUTI
 
Mm najipanga mwanangu atakapofika darasa la 6 nimuhamishuie Uganda akasome huko hadi chuo kikuu

Lengo no kukapture lugha na mengineyo

Lugha inatusumbua sana wabongo sio mchezo sio maraia Wa kawaida tu mpaka maprofesa kinawasumbua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom