Ni wangapi wanasoma? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni wangapi wanasoma?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mutekanga, Feb 11, 2010.

 1. M

  Mutekanga Member

  #1
  Feb 11, 2010
  Joined: Aug 26, 2007
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kwamba Jamii forums, inaandika mambo mengi tena kwa uwazi.Pongezi kubwa sana. Lakini je, ni wangapi wanasoma? Ni wangapi wana uwezo wa kuingia internet? Wale wanaoingia, mbali na kubishana na kutoa hoja mbali mbali ni kiasi gani wanafikisha ujumbe kwa watanzania wengine?

  Kuna wakati ninasita kuweka mawazo yangu hapa. Ninafikiri kuna haja yakutafuta njia nyingine ya kufikisha ujumbe. Kuna haja ya kuwafundisha watanzania wakafika mahali pa kusema hapana. Mfano, waseme hapana hatutaki Foleni! Kuna mambo mengi yanawakera watanzania, lakini eti wao ni Amani na utulivu. Foleni ni kero, foleni ni usumbufu na muda mwingi unapotea. Badala ya kufanya kazi watu wanashinda kwenye magari. Leo hii hauna anayeongea namna ya kutanzua tatizo hili. Maana yake ni miaka mingine zaidi ya 5. Kama barabara za kupita juu hazijengwi leo, ni ndoto kwamba zitajengwa ndani ya mwaka mmoja.

  Tunaimba kilimo kwanza, kwa mvua zipi? Hakuna mpango wa umwagiliaji. tuna maana ya wawekezaji kuja na kulima? Kuja na kuchukua ardhi yetu?

  Nasikitika kuandika haya hapa, maana ningependa watanzania wengi wasikie na kujifunza kusema hapana!

  Watanzania waseme hapana kwa Bunge lao, waseme hapana kwa wabunge wasiofika kwenye vikao vya Bunge, waseme hapana kwa maamuzi ya kijinga kama tulivyoshuhudia leo hii; ni lazima wafundishwe! Ni lazima waelekezwe!
   
 2. c

  chennai Member

  #2
  Feb 11, 2010
  Joined: Aug 17, 2009
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wengi wanaosoma JF ni watu wenye ajira na elimu zao. Wengine wapo majuu na wengine nchini.

  Nachoamini mimi nikuwa ujumbe muhimu hauwafikii walengwa vijijini ambao kila uchaguzi mkuu ni dole kwa CCM wakati watu wa mijini na wengi wa JF hawapigi kura. Ndo mana hamna mabadiliko hata ya polepole.

  Hizo barabara za kwenda juu subiria kwa uwezo wa roho mtakatifu asubuhi tutazikuta zimewekwa.
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 43,176
  Likes Received: 27,169
  Trophy Points: 280
  Watu wengi hasa DAR hawapigi kura,hawa nao wanatuongezea matatizo.wanaopiga kura ni wale wale nambari wani.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...