Ni wangapi wanakumbuka jina la mwalimu wa darasa la kwanza?

Hongera sana mkuu, Mimi mamayangu alikua mwalimu wa darasa la tatu
Tena kipindi hicho huyo mwalimu mmoja ndio anakuwa wa masomo yote kwa chekechea, au la 1&2, basi mnamzoea hadi raha.

Mnaimba na kucheza pamoja, kuandika kwenye udongo, ukishindwa unashikwa mkono. Sijui kama haya bado yapo.
 
Kwa yule aliosoma shule moja toka la kwanza hadi la saba .anaweza kuwafahamu...ila kwa sisi tuliohamahama shule huwezi kumbuka..
Mkuu kiukweli ninawakumbuka WALIMU wangu wa masomo karibu yote wa shule za MSINGI 3 nilizo soma-:
Mwalimu Pili Simon Uhuru Pr Dodoma RIP
Mwl KABUNDUGURU Jamhuri Pr Dodoma
Mwl KITIA Jamhuri Pr Dodoma
Mwl Chimalaunga Jamhuri Pr Dodoma
Mwl Said Jamhuri Pr Dodoma
Mwl Mjasiri Jamhuri &K/Ndege Dodoma
Mwl Fue Jamhuri Pr Dodoma
Mwl Masiru Jamhuri Pr Dodoma-RIP
Mwl Magawa Jamhuri Pr Dodoma
Mwl Abdi Jamhuri Pr Dodoma
Mwl Alfred Jamhuri Pr Dodoma
Mwl Jafar Jamhuri Pr Dodoma RIP
Mwl Febronia Hincha K/Ndege Pr Dodoma
Mwl Chilewa " " RIP
Mwl Teu " "
Mwl Lwenje. ". "
Mwl Kiula. ". "
Mwl Mwala ". "
Mwl Kichawele Idhungo ". "
Mwl Chitabu ". "
Mwl Songoro. ". " RIP
Mwl Chifupa. ". "RIP
Na Kati ya hao ALIYE wahi kunichaoa Ni wawili TU Mwl Magawa na Mwl Chitabu
 
Darasa la kwanza nawakumbuka mabeste kama omari hamisi sufiani makando alikua na dadake mayasa makando na swahiba wangu mkuubwa iddi hassan aizari mwali muyava mamake na freddy ila freddy alikuja kuwa best yangu baadae sana std five rangitatu primary shule maarufu kuliko zote mbagala
 
Namkumbuka mwalimu wangu wa Chekechea Mwl. Nassoro - Ttc mpwapwa.

Sitamsahau Mwl. Temu darasa la kwanza, Nilikuwa wa kwanza darasani akanisindikiza nyumbani na report bahati nzuri alikuwa anafahamiana na mama, wote wachaga akamwambia mama anipikie mtori. Dah, nilivimba shule mwaka mzima pale Mtejeta Primary School. When education was education.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom